YanguHaki
Senior Member
- Oct 11, 2010
- 129
- 9
Mara kwa mara navutiwa na jinsi majirani zetu Kenya wanavyoendesha mambo yao ya utawala hasa baada ya kupitishwa katiba mpya. Kwa sasa kuna zoezi linaloendelea la kuwachuja yaani "kuwa-vet" majaji 44 na mahakimu zaidi ya 300 wa mahakama za Kenya.
Leo hii nimekuwa nafuatilia kwa karibu jinsi wanavyomfanyia "vetting" mwanamama jaji Koome wa mahakama ya kuu.
Kwa nini nasi tusiige mazuri haya hapa nchini kwani kwa hali ninayoiona mahakama zetu haziminiaki mbele ya umma. Mchujo wa majaji utatuhakikishia tuna watu wanaofaa na kustahili kusimamia utoaji na usimamizi wa haki mahakamani. Kuna hisia za wazi kwamba zipo "pro-government" na haziko kamwe huru.
Wakati umefika tuachane na uteuzi usiowazi wa majaji tulionao kwa sasa. Nashangaa mtu alikuwa wakili kwa muda mrefu kesho anakuwa jaji! Au ni msomi wa sheria tu anateuliwa jaji! Hii si sawa kwa maoni yangu majaji watokane na mahakimu wazoefu wanaokidhi vigezo vya uteuzi. Hii itasaidia kuwa na majaji makini na wenye uzoefu pia.
Tuwe makini na hili vinginevyo mbele giza nene!