Tuifundishe jamii kwamba ni utovu wa nidhamu mtoto kumdai mama ataje baba mzazi asiyejulikana

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
407
614
Waungwana watanielewa tu.

Kwakweli inawaumiza baadhi ya watoto kutomjua baba! Ila nashukuru watoto wengi hawaumii ktk hilo. Watoto wanapaswa kuwa na adabu ktk hili hata Kama inawaumiza! Na mbaya Sana ndugu wengine wanamtia mtoto ujinga eti hatendewi haki na mama yake. Wamama ambao wanashindwa kutambulisha baba huwa wamebeba Siri mzito inayomuumiza maisha yao yote hadi anaingia kaburini

Hebu zitafakari sinario zifuatazo:

1. Msichana mdogo anarubuniwa na baba yake, kaka yake, mjomba wake na anapata mimba anamzaa mtoto. Anawezaje kumueleza mwanae? Matukio haya Mara nyingi yanapelekea abortion. Mtoto akifanikiwa kuzaliwa kwenye mazingira haya, amshukuru Mungu!

2. Msichana ana matatizo ya akili, na wanaume washenzi wamemuingilia Kisha amezaa mtoto. Mwanamke mmoja mkarimu anamlea na kumwaminisha kuwa yeye ni mama mzazi

3. Mwanamke analiwa kimasihara safarini, matukio ambayo wahusika wamekutana kwa bahati mbaya na hawaonani tena. Mwisho wa siku mdada anajikuta mja mzito huko aendako.

4. Mdada anatembelea kwa shemeji yake mume wa ndoa wa dada yake, then mtu na shemu wanakula kimasihara. Mdada anarudi nyumbani anajikuta mja mzito

5. Mwanamke mgumba ameolewa Mara kadhaa na ameachika, mwisho wa siku haolewi Tena, Kisha anaamua kuasili mtoto yatima akiwa na makusudio aishi nae Kama mtoto aliyemzaa

6. Kuna wanaume washenzi ambao wanamiliki demu, na siku akiamua kuachana nae anawaita wavutabangi wenzake wanamwingilia kwa pamoja, wanamla na tigo kwa nguvu. Kumbe kwenye tukio hili anapata ujauzito

Yes, Kuna Mambo mengi ambayo mama zetu wametunza Siri zao. Hebu tuwapende mama zetu, tuwastahi, tuwavumilie. Wangeweza kutoa hizo mimba Ila maskini ya Mungu waliaminishwa kutoa mimba husababisha kifo wakaogopa!

Watoto tushukuru tu kuwa tumezaliwa! Tuache hoja ya kupambania haki eti mtoto ana haki ya kumjua mzazi wake. Baba aliyejitenga na mtoto ndiye anayemnyima mtoto haki ya kumtambua baba yake. Kosa hili asibebeshwe mama ambaye ametimiza wajibu wake wa kuzaa na anaendelea kutimiza wajibu wake wa malezi

Wanajamii tuwafundishe watoto kuwastahi mama zao. Tamthilia zenye maudhui ya kuwananga wamama waliohifadhi Siri zao, tuachane nazo
 

Kapeace

JF-Expert Member
May 26, 2017
16,625
38,785
Changamoto haikimbiwi,,hiki ulichoandika ni kama kukimbia kivuli chako, kila mwanadamu ana haki ya kujua asili yake na hasa wazazi wake asilia wa kumzaa,, mengineyo hutokea tu km kuokotwa ila haina baraka,, wanawake tuwaambie watoto wetu ukweli wa baba zao hata kabla ya kuulizwa
 

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
407
614
Changamoto haikimbiwi,,hiki ulichoandika ni kama kukimbia kivuli chako, kila mwanadamu ana haki ya kujua asili yake na hasa wazazi wake asilia wa kumzaa,, mengineyo hutokea tu km kuokotwa ila haina baraka,, wanawake tuwaambie watoto wetu ukweli wa baba zao hata kabla ya kuulizwa
Siku zote watu msiopitia magumu ya wenzenu muna haraka Sana kuyasemea!

Mshukuru Mungu aliyekuepusha na mabalaa haya ya Dunia

Wenzako ktk Dunia hii wanaumia na kuungua
 

Kapeace

JF-Expert Member
May 26, 2017
16,625
38,785
Siku zote watu msiopitia magumu ya wenzenu muna haraka Sana kuyasemea!

Mshukuru Mungu aliyekuepusha na mabalaa haya ya Dunia

Wenzako ktk Dunia hii wanaumia na kuungua
Asante kwa kunijua Sana zaidi ya ninavyojijua,,
 

Ivyblue

JF-Expert Member
Jan 5, 2022
946
2,299
Umenena vyema, lkn haki ya mtoto n pamoja na kujua chimbuko lake haijalish alipatkanaje.

Mtajie baba yake, usmuelezee alipatkanaje kwa njia gani haijalish ulibakwa ama vp.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom