TUICO: Ripoti ya kamati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUICO: Ripoti ya kamati

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by NGULI, May 14, 2009.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  TAARIFA YA MGOGORO KATI YA KAMATI NA TUICO NA WAJUMBE WA KAMATI YENYEWE no. 1

  Ndugu,
  Wafanyakazi wenzangu, tatizo lililopo na linalo tuzunguka kichama na kamati ya majadiliano yanapaswa kuwekwa wazi ili tuweze kuamua nini cha kufanya badala ya kuburuzwa tu.

  Matatizo yalianza miaka miwili iliyopita kwa kiongozi aliyepewa dhamana ya sekta ya fedha kuwa na matatizo ya kuwagawa wajumbe wa kamati pamoja na haya:-

  (i) Kutohudhuria mikutano ya majadiliano kwa makusudi.

  (ii) Kuhudhuria akiwa amechelewa.

  (iii) Kuhudhuria amechelewa na kisha kutoa udhuru na kuondoka wakati majadiliano yana endelea au kusitishwa kwa sababu hiyo.

  (iv) Kuto taka kuitishwa kwa mikutano ya wafanyakazi wote kwa mwaka wa 2008 huku akiunda kundi ili lidai mkutano na kuvunja kamati.

  (v) Kiongozi huyo alisha wahi kushawishi baadhi ya wajumbe wenye nguvu katika kamati ili kusitisha michango kupelekwa TUICO ili wagawane kwa sababu yeye :-
  (a) Yeye analipwa mshahara mdogo na anafanya kazi zetu
  Nyingi bila malipo.
  (b) Yeye anakutana na waajiri wenye pesa naye hana
  hivyo ni rahisi kurubuniwa.

  Ombi hili lilikataliwa na wajumbe hao ndipo mizengwe ya kuwaengua ilipoanzia.

  (vi) Mwaka 2008 kwa mwaka mzima kamati ilishindwa kufanya mikutano ya wafanyakazi wote. Kamati katika kipindi hicho mara kwa mara ilikua inaomba kufanya mikutanao hiyo kupitia ofisi yake kwa barua (hili limweza kuthibitishwa na aliyekuwa katibu wakati huo). Hakuna barua hata moja iliyojibiwa huku kiongozi huyo akitoa sababu za mdomo kuzuia mikutano hiyo.

  Kitu kilichotustua wenye akili ni pale Oktober 2008, makundi yasiyo rasmi walipotoa waraka kuomba mikutano na kamati mpya wakiongozwa na mwana mama aliyopo idara ya operation.
  Barua hizo zilijibiwa mara moja na mkutano ulifanyika Nov. 2008.

  Hapa wenye akili tuligundua kwamba kiongozi huyu alikuwa akizuia kufanyika mikutano, huku akiunda kundi lake ili liombe mikutano na pia waombe kuwepo kwa kamati mpya kwa madai kuwa kamati ya wakati huo haina mawasiliano na wafanyakazi na haiwawakilishi .
  Hata hivyo alisahau kuwa kamati ni pamoja na yeye ambaye ndiye mhimili, kama kamati mbovu basi na kiongozi wake pia ni mbovu.

  Yeye Kama mkuu alipaswa pia kueleza wanachama wa NBC LTD, kwanini mikutano haikufanyika kwa kipindi hicho badala ya kuunda kundi na kudai kamati haiwakilishi wanachama.

  Nini lilikuwa kusudio la mbinu hizi:-

  (i) Kuonesha wafanyakazi kuwa kamati haifai ili iondolewe madarakani.
  (ii) Suala zima, zito na muhimu la Job Grades lisijadiliwe kwa vile linagusa fidia kubwa ya pesa na kurekebisha grades za wafanyakazi.
  (iii) Kuhakikisha Wajumbe waliokataa mbinu zake za kula michango yetu wanaondolewa katika kamati maana wameshajua siri yake.
  (iv) Kuhakikisha majadiliano ya bonus na mishahara hayafanyiki ili mgawo uwe mbovu kwa manufaa yake
  (v) Kuhakikisha wale wafuasi wake wa itikadi zake wanaingia katika kamati mpya kama ilivyofanyika, ili awaburuze .

  Watu wengi katika kundi lake na walio mstari wa mbele kuomba kuvunjwa kwa kamati walikuwa wana sababu zifuatazo tu:-
  (i) kuonesha wafanyakazi kuwa kamati haifai ili iondolewa madarakani.
  (ii) Kuhakikisha wafuasi wake wanaingia katika kamati kama ilivyo fanyika.
  Hivyo basi ilikuwa rahisi kwao kuburuzwa bila kujua kwamba wanatengeneza kifo chao wenyewe kwa kukwamisha majadiliano ya aina zote.

  Mwezi Nov, 2008 kulifanyika mikutano miwili ya wafanyakazi wote katika ukumbi wa Korea na Star Light. Katika mikutano hiyo, mapungufu ya kiongozi huyu pamoja na TUICO yenyewe yalibainishwa, Katibu Mkuu na kundi lake akiwamo kiongozi huyu wa sekta ya fedha walikubali mapungufu hayo na waliahidi kuyafanyia kazi na kuyaondoa kabisa. Jambo la kuvunja kamati lilikataliwa na iliamuliwa kamati iendelea isipokuwa miswada itakayo jadiliwa igawiwe kwa matawi ili watoe maoni na mapendekezo yao na hili lilifanyika.

  Kikao kilichofuata kilikuwa cha Halmashauri ya matawi ya DSM na mikoa ya jirani kwa kusudio la kupokea maoni na mapendekezo ya matawi yaliyo tokana na miswada 19 iliyogawanywa katika mkutano wa Star Light Nov, 2008. Kikao hicho kilifanyika CryStal Place hotel , Ilala wakati Katibu Mkuu akiwa India kwa matibabu.

  Kabla ya kupokelewa kwa maoni, hoja ya kuvunjwa na kuundwa kwa kamati iliibuliwa tena na kundi la kiongozi huyu ambaye pia alikuwa anachukua nafasi ya Katibu Mkuu kwa wakati huo akiwa na mpambe wake Mheshimiwa ambaye zamani alikuwa mtumishi wa NBC ,walisimama kidete hadi hoja hiyo ilipokubaliwa na kamati ya awali ikavunjwa.


  Sababu kuu za kuvunja kamati ni hizi:-


  (i) Kuhakikisha Wajumbe waliokataa mbinu zake za kula michango ya wafanyakazi wenzao wanaondolewa katika kamati kwa njia ya kura na eneo la uchaguzi. Hii itawapa nafasi ya kutafuna michango yetu, ndiyo maana walichofanya kwanza ni kuzuia michango hata kama si ya chama chao.

  (ii) Suala zima, zito na muhimu la Job Grades lisijadiliwe kwa vile linagusa fidia kubwa ya pesa na kurekebisha grades za wafanyakazi wa NBC LTD.Suala hili lilikuwa linaongozwa na Said Mohamed na Magai ambapo uongozi wa benki umekiri kuwa umevunja shera no. 23 ya 1997. Hivyo ilionekana ni lazima jambo hili liwaondoe wajumbe hao katika kamati ili lisijadiliwe kabisa .

  (iii) Kuhakikisha majadiliano ya bonus na mishahara hayafanyiki kwani wajumbe wapya watahitaji muda kujiweka sawa wakati muda wa kufanya jambo hilo utakuwa unapita.

  (iv) Kuhakikisha wale wafuasi wake wa itikadi zake wanaingia katika kamati mpya kama ilivyofanyika, ili awaburuze .

  Siri hii walikuwa wanaifahamu wajumbe wachache tu katika kamati ,hivyo ni rahisi hadi sasa kuendelea kuburuzwa kiasi hicho bila wao kujua wafanyalo.
  Nawaomba kuamka maana tayari nimewapa siri.

  Jambo hili limethibishwa na AL- Haji mwenyewe katika taarifa yake kwa wafanyakazi wote ya tarehe 24.03.2009 iliyoambatana na tuhuma dhidi ya Said na Magai kwamba wana ng’ang’ania madaraka yake.

  Katika ukurasa wa kwanza fungu la tatu la taarifa yake amesema ni yeye aliye panga kampeni ya kuvunja kamati kwa kisingizio cha kuingiliwa madaraka yake bila kukumbuka kuwa alikuwa amekasimu madaraka yake kwa maandishi na kielelezo nimekimeambatanisha kwa ushaidi huo kwenu.

  Katika waraka huo yeye ana hitimisha kwa kusema tusitafute mchawi anaye tukosesha haki zetu ikiwa ni pamoja na bonus na hatimaye kima cha chini na nyongeza za mishahara ni yeye na kundi lake wamefanya hivyo na walitegemea hayo kutokea ili mradi Said Na Magai waondoke katika kamati kwa hilo ndilo muhimu kwao.

  Hata hivyo kama kweli alikuwa na tuhuma hizo , kipi kilimzua kuwasilisha hoja hizo katika vika halali ambavyo vilikuwa vinafanyika mara kwa mara ili kupata ufumbuzi ?.

  Mwaka 2007, tulipo toka katika majadiliano ya bonus, tulikubaliana kwamba uongozi wa benki ukatengeneze rates zitakazo tumika kugawa bonus na kasha watuletee tuzihakiki kabla ya kulipa.
  Tulishangaa kuona AL – Haji ametoa barua akidai amesha kubaliana na uongozi wa benki na hakuna atakaye lipwa chini ya Tshs 550,000 na kwamba amekwenda Iringa katika sherehe za Mei Mosi amechaguliwa na Uongozi wa NBCLTD.
  Siku ya pili Bonus ililipwa bila uhakiki wowote.

  Kwanza napenda mjue kwamba Mheshimiwa ambaye zamani alikuwa mtumishi wa NBC si yule mliye mjua na aliye kuwapo NBC Ltd, na si mtetezi wa haki zetu bali zake tu.

  Hivyo AL- Haji ni muongo na mnafiki mbele yenu, na sijui kwanini tunashindwa kufikiri kana kwamba hatuna akili wakati tunazo kwa imani yangu.

  Mimi naelewa bei ya AL- Haji ,naibu katibu mkuu na mjukuu wa Al-Haji imesha julikana kwa uongozi wa benki .
  Sasa bado wewe unaendelea kujaza form za chama kipya.

  Kama mabosi wenu wamenunuliwa nyie mtabakia vipi ?.

  Hata kwa akili ya kawaida tu , nielezeni ni chama gani hicho kina ushabiki na ushawishi wa mwajiri ?.
   

  Attached Files:

Loading...