Tuiadhimishe kuwa siku ya MASHUJAA NA WAPIGANIA DEMOCRASIA Tarehe aliyokufa Hayati CHACHA WANGWE. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuiadhimishe kuwa siku ya MASHUJAA NA WAPIGANIA DEMOCRASIA Tarehe aliyokufa Hayati CHACHA WANGWE.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by William Mshumbusi, Jun 6, 2012.

 1. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Chadema muazimishe siku aliyokufa CHACHA WANGWE .
  Iwe ni siku maalumu kuwakumbuka wanaharakati wote waliouhawa au kufa vifo vya gafla wakipigania democrasia haki na ukweli kama

  1. Prf. CHACHAGE huyu alikuwa prf wa UDSM. Alipinga wizi kwenye ubinafsishaji kwenye hawamu ya mkapa kwa kuendesha midahalo mbalimbali. Alikufa kifo cha gafla Tanga kwenye kongamano baada ya kunywa maji ya chupa.

  2.CHACHA WANGWE alikuwa mbunge na mpinga ufisadi. Alikufa kwa ajali na dreva aliyemuua alikuwa katoka libya miezi miwili iliyopita na alifungwa mwaka moja.

  3.COLIMBA Alikua katibu mkuu wa CCM na alikufa kifo cha gafla baada ya kusema CCM haina dira alipoitwa kuhojiwa kwenye mkutano na kamati kuu ya CCM.

  4. KOMBE huyu ni afsa usalama aliyepigwa risasi na polisi wakizani jambazi. Alikuwa akidaiwa kumpa siri za wizi selikalini Agustin Lyatonga Mrema. Na mlema akawa anazifumua bungeni.


  Kuna wengine watatu nimewasahau majina.

  Aliyeshinda ubunge Shinyanga mjini ila Hakutangazwa na kufa kifo cha gafla wakati kesi ikiwa mahakamani

  1. Wakili wa kujitegemea aliyekuwa anaisimamia kesi ya mgombea binafsi na mtikila. Alipigwa risasi nje ya nyumba yake yeye na jirani yake na hawakuchukua kitu sikumoja baada ya kutangaza kukata rufaa kwenye mahakama za kimataifa kuhusiana na swala hilo.

  2. Aliyekuwa katibu mkuu wa wafanyakazi wa shirika la leli. Alifariki kwa ugonjwa wa moyo aliougua na kumuua hapohapo kwani hakuwanao kabla hii ni baada ya kuvutana na selikali kwa muda mrefu juu ya maslahi ya wafanyakazi na mustakabali wa shirika la leli.

  Wapo wengine wengi. Siku hii tuiazimishe kwa kufanya maandamano tukiwa tumevaa magunia na tumebeba picha zao na mabango ye ujumbe wa kuwasifu. Hii itasaidia kuwapa moyo wamaharakati tulionao na inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia vifo vya gafla.
   
Loading...