Tuiachie Serikali itoe majibu ya nani anahusika na shambulio la Lissu, msituchanganye wananchi

W. J. Malecela

Verified Member
Mar 15, 2009
14,056
2,000
EXTRA STRAIGHT TALK:- Unaporusha rusha maneno ya kichochezi kuhusu kushambuliwa kwa Mh. Tundu Lissu bakisha maneno na tafuta Facts kwanza ....

naomba nikukumbushe kwa FACTS .....Mauaji ya Waisilamu Mwembe Chai Mwezi May, Mwaka 1998 Rais hakuwa Magufuli!....Wakati wafuasi wa CUF Pemba wanapigwa mabomu Mwaka 2001 January na kuuliwa wafuasi wao 20 Rais hakuwa Magufuli ....Mwaka 2002 September 2, Muandishi wa Habari Daudi Mwangosi alipouliwa na Bomu Iringa Rais hakuwa Magufuli! ....January 5, 2011 Wananchi 3 waliuawa kwa Risasi za Polisi Arusha kuthibiti maandamano yasiyokuwa na kibali vipi Rais hakuwa Magufuli! ....June 28, 2012 Dr. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana akiwa Leaders Club anapata supu asubuhi Rais hakuwa Magufuli! ....Mwezi May, 2013 Muandishi wa Habari maarufu Absalom Kibanda alipotekwa na kupigwa vibaya Rais hakuwa Magufuli....na June/2008 Makamu wa Mwenyekiti Chadema aliyekuwa anataka kugombea Uenyekiti wa chama hicho na kuishia kufariki kwenye ajali ya ajabu Dodoma Rais hakuwa Magufuli ....October, 2013 Mwigamba alipopigwa mpaka kuzimia kwa kudai mahesabu ya Chadema Rais hakuwa Magufuli!


....please msijaribu kupandikiza chuki baina yetu wananchi tutaendelea kuwakumbusha kuwa hakuna ushahidi so far wa nani anahusika na kupigwa kwa Mh. Tundu Lissu ...wote tunamuombea apone haraka ila tutaendelea kupinga hukumu za bila Facts against Serikali ....kuhusu matibabu kwa utaratibu wa Serikali ili Mbunge akatibiwe nje ya nchi na kulipiwa na Serikali ni lazima ithibitishwe na Matabibu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwamba WAMESHINDWA na jana ni FAMILIA YA LISSU ndiyo iliyodai kutaka Lissu akatibiwe nje na sio Madaktari wa Muhimbili kama utaratibu unavyotaka na sababu walisema wanahofia usalama wake ...now Serikali ya Rais Magufuli haina cha kufanya isipokuwa kuwaruhusu familia yake wafanye wanachotaka ....Thanks tutaendelea kuwekana sawa kwa FACTS kuhusu kinachoendelea na some of us tutaendelea kusimamia Ukweli tu ...kushambuliwa kwa Lissu hakumfanyi anyone kuwa na haki ya kuhukumu wengine bila FACTS Taifa ni letu wote so relax guys ...kama hamna FACTS nyamazeni iachieni Serikali ifanye kazi yake STOP THE MADNESS! - le Mutuz
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,817
2,000
Ni watu wachache sana watakao kuelewa unamaanisha nini? watanganyika wamekuwa mainvestigator na madetective kichwani mwao na ktk ubongo space ya majibu kuko full wakati space ya facts na maswali kuko empty

Kuna vitu vinatia shaka sana kwa tukio la Lissu na siku zote upelelezi lazima uanzie kwa watu wa karibu wa aliyepata matatizo
Mi nahisi tupate independent inquiry committee kama CIA ili utata wote uishe
Ndugu hata waje nani mbinu na taratibu za investigation zinafanana kuanzia

1 DNA
2 CCTV cameras
3 Finger print
4Ushahidi wa Mazingira
5Ushahidi wa mawasilino

Huku njia za kiuchunguzi ni 6 zilezile si kwamba CIA wakija watakuja na njia zaidi ya hizi
1 immediate action
2 Plan investigation
3 Data collection
4 Data analysis
5 Corrective actions
6 Reporting

Ukiangalia njia karibu zote tayari jeshi la Police linazifanyia kazi toka siku ya kwanza kingne ambacho ujui huko huko kwenye NSA,CIA,FBI yani US ndio nchi ya kwanza kuongoza kwa mauaji ndani ya US na Marekani hakuna kesi zinazochukua muda mrefu kuwa solved kama kesi za mauaji kuanzia mauaji ya Mitaani au homicide rate ya mauaji kwa mwaka ni 16.3% ya vifo vyote vinavyotokea US ni vya mauaji hasa ya silaha za moto yani bunduki pamoja na kuwa na Technologia kubwa vyombo vya Ulinzi na usalama zaidi ya 17 lakini ndio nchi yenye rate kubwa ya mauaji ya kutumia silaha na kesi zake zinachukua muda mrefu sana
Kuanzia mwaka 1968-2011 kumefanyika mauaji zaidi ya 1.4 milion kesi ambazo zimekuwa solved yani wauaji kupatikana na hukumu kutolewa ni chini ya kesi 1.2 milion so bado kesi zaid ya laki mbili bado si solved hiyo ni mwaka 1968-2011 kumbuka ktk nchi zenye vurugu na mauaji ya silaha SA na USA zinaongoza

Mwaka 2010 68% of all homicides in the US were committed by firearms
Lakini kesi nyingi za mauaji zinategemea sana laboratory kusolve kuanzia DNA mpaka Finger print ambapo FBI wana
system ya Combined DNA Index System ( CODIS ) ambayo raia wote wa US DNA zao zinakuwapo so wanakuwa wanafanya matching na DNA ya kwenye Crime scene pia bado aitoshi kumfungulia mtu kesi kwani mtu anaweza kuua na kupadikiza DNA ya mtu mwingine kwenye Crime scene je DNA za raia wote wa Tanganyika zipo kwenye data base?? na katika uchunguzi watu wa kwanza kuchunguzwa juu ya swala hili ni Chadema wenyewe kwani kanuni ya uchunguzi inaanzia kwa watu wa karibu wa aliyepata matatizo je chadema wako tayari kuchunguzwa wao kwanza? pili wako tayari kupokea majibu ya uchunguzi utakapokamilika je ikitokea Chadema kuna mtu amehusika je wapo tayari kukubali je wanachama wa chadema wapo tayri pia kukubali matokeo ya uchunguzi huo??
 

Wanstechnical

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
266
250
We mwenyewe ulichoandika hapo ni kama una-implicate kwamba CHADEMA ndio wanaohusika, sasa ni facts gani ulizonazo zaidi ya kubwabwaja tu? Weka akiba ya maneno pia na viachie vyombo vya usalama vifanye kazi yake, wananchi wana haki ya kuconect dots wanazoziona na kama inalalia upande huo wanaouona we ni nani kuwabadilisha?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom