sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Wimbi la tuhuma za wizi wa kura katika chaguzi mbalimbali nchini limetanda zaidi ya miongo miwili, sasa.
Tuhuma hizi ni nzito sana,tena zina hitaji tafakuri na majibu ya kina kuliko vitisho.
Tume ya uchaguzi imekuwa ikituhumiwa kama mhusika mkuu kwa kushirikiana na CCM, lakini majibu ya tuhuma hizi zinajibiwa kiwepesi kuliko tuhuma zenyewe.
Unapoiba kura za wananchi, umeiba demokrasia. Umeiba uhuru wa wananchi kumchagua kiongozi wamtakaye, lakini pia una vuruga uvumilivu wa wapiga kura kwa kuwanyang'anya haki yao ya kuchagua wamtakaye kwa mujibu wa sheria.
Uwizi ni maandalizi kwa maana ya connection, viashiria vya wizi vimeanza kuonekana wazi, tusipo chukua tahadhari tunaingiza Taifa kwenye majanga makubwa.
Bahati mbaya sana anayelalamika mara kwa mara kuibiwa amegoma safari hii kuibiwa tena na tena, akisema sasa basi inatosha. Maanake nini, hatokubali ghiliba,upendeleo, vitisho na kila aina ya dhuluma inayo fanywa kutengeneza mazingira ya wizi wa KURA.
Tume ya uchaguzi iliyo teuliwa na Mwenyekiti wa CCM, kwa kuwateua makada wenzake kwa mwamvuli wa urais kusimamia uchaguzi ambao yeye anagombea ni zaidi ya mbinu chafu za wazi zenye malengo ya kulazimisha ushindi.
Mkurugenzi wa uchaguzi, ambaye ndiye msimamizi mkuu wa uchaguzi ni kada wa CCM kama video clip iliyo trend kwenye mitandao ya kijamii inavyo jieleza, kuteuliwa kusimamia uchaguzi wa ushindani dhidi ya mtu aliye mteua ni kuto kuwatendea haki wagombea wengine na kuufanya uchaguzi kuwa wa kimkakati na mbinu chafu dhidi ya demokrasia inayo heshimu uhuru wa watu kuwachagua viongozi wawatakao.
Kulazimisha tume kuendelea kuteuliwa na rais mgombea, bila kuidhinishwa na bunge na tena bila kuwa na makamishana wa uchaguzi kutoka vyama vingine ni maandalizi rasmi ya ubakaji wa demokrasia nchini.
Tume kuwa biased kwa kushindwa kukemea makosa ya wazi yanayofanywa na mgombea urais wa CCM kwa mwamvuli wa urais, akipingana na sheria na kanuni za uchaguzi bila kukemewa na tume hiyo, lakini wapinzani wakitishiwa kwa taharuki ya kuzuia mianya ya wizi wa kura ni zaidi ya UDIKITEKTA unapaswa kupigiwa kelele kwa nguvu zote na waumini wa demokrasia nchini.
Kuzuiwa kwa matokeo ya urais kuhojiwa wala kuthibitishwa mahakamani, kinyume na matokeo ya ubunge na madiwani, hii ni maandalizi ya kuibadili sovereign state kuwa monarchy state, lakini pia inatoa mianya ya uporaji matokeo usihojiwe na mamlaka yeyote ile.
Ili viashiria hivi na tuhuma hizi zipatiwe majibu ya kina, tume inapaswa kuacha upendeleo wowote ule kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Sheria ichukue mkondo wake ili dhana nzima ya uchaguzi wa kidemokrasia iwe na tija.
Haitoshi kuvikemea vyama mbadala kwa kauli zao za kukataa kuibiwa kura, huku ukifumbia kanuni na sheria za uchaguzi zikivunjwa makusudi na CCM, kwa kuwa ndicho chama kinachoongoza serikali.
Sheria na kanuni za uchaguzi zinakataza rushwa, lakini mgombea urais wa CCM anatumia influence ya madaraka yake kukiuka sheria hiyo kwa kuagiza utekelezaji wa ahadi zake kwa mgongo wa urais kinyume na sheria ya uchaguzi.
Wakati sheria hiyo ina tafsiri utekelezaji wa maamuzi yeyote kwa mgongo wa madaraka uliyo nayo ukaagiza yafanyike kipindi hiki kwenye jukwaa la kampeni ni rushwa, lakini tume ya uchaguzi imeendelea kufumbia macho ukaidi huu wa makusudi unaofanywa na mgombea wa CCM.
Pamoja na mbeleko hii kwa kutumia dola vyama mbadala vimetoa angalizo,kuwa hiyo tarehe 28 October, havita kubali matokeo yeyote yenye sura ya wizi wa Kura.
Vile vile tume inapaswa kujua kuwa nchi hii ni yetu sote, heshima hujengwa kwa mkubwa na mdogo, vitisho havisaidi au kukuza demokrasia, uchaguzi huu ni baina ya watanzania kwa watanzania, tume isimamie maamuzi ya haki tu, vinginevyo Taifa linakwenda kuangamia kwa kukosa maarifa.