Tuhuma za William Malecela dhidi ya Heche na Dr. Slaa - Nampa siku 3 Vinginevyo...

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Nimesoma uzi aliouanzisha hapa JF na Bw William Malecela akimtuhumu Mkiti wa Bavicha John Heche huku akimuunganisha Dr Slaa bila kutoa ushahidi wo wote. Na hii si mara ya kwanza wala ya pili au tatu kwa Bw W. Malecela kutunga story za uwongo na kuzileta hapa JF. Hili ni jambo lisilokubalika kuleta uwongo na uzushi ktk jukwaa la Great thinkers.

Kwa bahati nzuri ninamfahamu John Heche tangu akiwa Diwani hadi leo. Ninamfahamu mpaka baadhi ya ndugu na wadogo zake pia.
Na ni kwa sababu hiyo, Nitajibu hojo mmoja baada ya nyingine, then nitampa ultimatum.
Hoja yake ya 1.
Dereva wako anayeajiriwa na chadema ni mdogo wako mwenyewe.
Jibu; Hakuna mdogo wa John Heche aliyeajiriwa na Chadema makao makuu ya Chadema. Ifahamike, situmii ID ya kuchonga, kwa hiyo, ninasema kile ninachojua ambacho nina uhakika nacho tu. Sijibu kikasuku ili mradi nionekane ninatetea chadema.

Hoja yake ya 2

Wadogo zako wote kwa muda mrefu wamekuwa wakisomeshwa na Mbunge wa sasa wa Tarime.

Jibu;
Huu ni upuuzi mwingine ambao mimi ninaujua vizuri sana binafsi.
Mosi, John Heche hana wadogo wanasoma shule za msingi wala secondary, japokuwa mwenyewe hajafafanua anaongelea elimu gani.
Pili, Heche ana wadogo zake wawili ambao mmoja yuko chuo kikuu cha Dsm na mwingine yuko Chuo kikuu cha St Augustine. Wote wana mikopo ya serikali. Kwa hiyo, binafsi nina uhakika kuwa huu ni uzushi 100%.

Hoja yake ya 3
Hela za kodi ya nyumba yako inalipwa na Dr Slaa kwa muda mrefu.

Jibu;
Huu nao ni uzushi mwingine kwa 100%. Naomba nijibu kwa ufupi tu kwamba hakuna kitu kama hicho - Nina maanisha hakuna malipo toka ofisi ya mkurugenzi wa fedha wa Chadema na yaliyoidhinishwa na Dr Slaa kama katibu mkuu kulipia pango Heche.

Sasa naomba nimpe siku tatu Bw W. Malecela kufanya mambo matatu yafuatayo;.

Mosi, William Malecela aje na ushahidi wa malipo ya wadogo zake John Heche walioko chuo kikuu ambao wanalipiwa ada na Mbunge wa ccm wa sasa wa Tarime.

Pili Wiliam Malecela aje na ushahidi wa ajira ya mdogo ye yote wa kuzaliwa wa John Heche aliyeajiriwa makao makuu ya Chadema- eg mkataba au barua ya ajira.

Tatu, William Malecela aje na ushahidi wa malipo ya kila mwezi ya kodi ya nyumba ya John Heche iliyoandikwa na mkurugenzi wa fedha makao makuu ya Chadema ykaidhinishwa na Dr Slaa kama katibu mkuu.

Akiweza hilo, mimi nitakuwa mwongo na mzushi.

Akishindwa nitaanzisha uzi kumtangaza W. Malecela kuwa mzushi na mwongo baada ya siku tatu nilizompa na wanajf wote lazima wamwone kama Mwongo na Mzushi na asiyepaswa kuaminiwa tena hapa JF. Kwa kuanzia adhabu hiyo inamtosha.
Bila kufanya hivi, heshima ya JF itashuka maana itaonekana kama JF is NOT the home of great thinkers But the home of big lies.

Nasubiri ushahidi wa W. Malecela.

NB; Nimesoma pia story za Juliana Shonza dhidi ya Dr Slaa na Mbowe. Namsamehe kwa leo kwa kuwa najua yuko ktk wakati mgumu wa kupoteza cheo chake. Anaweza kusema cho chote wakati huu

Mchango wa Mohamed mtoi ktk uzi huu kuhusu jina la John Heche hapa chini.
Mohamedi Mtoi;5472564]Mkuu.
Binafsi sioni kuwa kuna hoja kubwa zenye kustahili majibu ya kuumiza vichwa kwa kufanya tafiti zenye tafakuri tunduizi.

Kuhusiana na majina ya heche kama moja ya shutma za mtoto wa kigogo na baharia muendesha majungu soma huu ufafanuzi wa kaka yeke John Heche.

"John Heche ni mdogo wangu kwanza naomba niweke wazi hilo...Sisi baba yetu alikua na wanawake 7 kati ya hao watoto tuko 42 wote wa baba mmoja ni marehem sasa( Mungu amweke pema) .
Mzee alikua anaitwa CHARLES HECHE SUGUTA...sasa ukiangalia hapo jina CHARLES ni la baba na pia HECHE Ni jina lingine la mzee, Jina la John la ukoo ni WEGESA na hilo JOHN ni la ubatizo,,sasa kwenye vyeti na shuleni alikua anatumia WEGESA CHARLES ambae CHARLES NI jina la mzee kama ilivyo pia HECHE,,,its not an issue kabisa ni ushauri wangu kwa vijana wa cdm wakue wajadili masuala ya Kitaifa ya kusaidia nchi sio kurukaruka kama njiwa na kusema vitu vya ajabu...jina hilo ni sahihi na la kwetu kabisa anayebisha aende Tarime aulize mzee HECHE/IMEKUBALIKA watu wanamjua baba yetu majina yote hayo ni yetu..na hilo John Heche/
- Wegesa Charlese yote ni majina ya ukooVs haya ya ubatizo lakini yote ya mtu mmoja simple...Suala lingne kuna mtu wa hao jamaa anasema eti wadogo zetu wanasomeshwa na Mbunge hilo sio kweli ni UONGO na UZUSHI mtupu sisi kama familia tunasomesha wale vijana wetu wote walioko vyuoni na secondary kwa kipato halali tulicho nacho".

Manchare Charles Heche Suguta.

Ufafanuzi huo hapo juu kwenye jukwaa la mabadiliko na ukiusoma katikati ya mistari hauna tofauti na ule ambao kamanda
Mwita Maranya
aliuleta.

Hoja nyingine za Shonza niza kipuuzi kama jinsi ufafanuzi huo hapo juu unavyo mvika taji la kipuuzi.

Kwa nini?
Angeleta ushahidi wenye vielelezo visivyo acha chembe ya shaka kuhusu madai na tuhuma zake angeeleweka kirahisi kuliko kuja a debe la maneno mengi ambayo mwisho wake badala ya kusaidika kiwango cha kudharaulika ndio kinazidi.[/QUOTE]


 
Mkuu Aweda nakupongeza katika hilo na nakuunga mkono 100%.Huyu Le Mutuz amezidi kuwa Mzushi inawezekana anatumwa na Magamba ila Nasikia ingawaje anatumika kama Condom lakini hata magamba wanamkwepa sababu ya ukurupukaji wake. Hata akigombea wanamtosa.

Nina wasi wasi nae hasa ubongo wake ingefaa Mzee wa Mixed feelings (John Malecela) akampeleka kupimwa akili.
 
Mkuu unajua kabisa kwamba umri alionao(miaka 52) Bwana W.Malecela is inversely proportional to his thinking capacity,kwahiyo ni vizuri kumchukulia kama mtoto mdogo ambaye anafanya mzaha wa kijinga.Kikubwa zaidi mtoto mwenyewe bado anahitaji maelekezo ya watu wazima, ni vema kumsamehe bure!
 
Huyu jamaa mambo anayo fanya hayaendani na umri wake kabisa.
 
Mkuu unajua kabisa kwamba umri alionao(miaka 52) Bwana W.Malecela is inversely proportional to his thinking capacity,kwahiyo ni vizuri kumchukulia kama mtoto mdogo ambaye anafanya mzaha wa kijinga.Kikubwa zaidi mtoto mwenyewe bado anahitaji maelekezo ya watu wazima, ni vema kumsamehe bure!

Nadhani P Aweda hana kazi za kufanya, watu mbona walishaacha kuzichukulia serious ishu zozote za W. Malecela???
 
Huyu W. J. Malecela si aliondoka kwa mbwembwe na matusi mengi hapa JF?

Mbona naona anaendelea kuposti maujinga yake?

Naona kichwani amevaa vazi la kuonesha kwamba amepewa degree marekani (sijui chuo kikuu cha kata!) japo kuwa mwita Maranya amedai huku kwamba jamaa alizungusha div 0 secondary.
 
Mkuu asante sana! Nadhani Mods watusaidie ikiwa jamaa hatathibitisha apigwe life BAN.

Kwa kuongezea katika hili, sasa huu ndio uwe mwanzo wa kuwashughulikia watu wote wanaopost thread za kizushi hapa JF kila kukicha. Sasa ni wakati muafaka kwa mods kuisafisha JF na msururu wa upuuzi unaoanzishwa hapa kila siku.

Ahsante sana kamanda Mikael P Aweda kwa ufafanuzi huu ambao naamini kabisa le mutuz hawezi kuthibitisha tuhuma alizozitoa.
 
Last edited by a moderator:
atadhibitisha vipi wakati amezoea kugeuza uongo kuwa ukweli na ni wale wale mawazo yale yale akili ile ile unatarajia kweli hapo kutakuwa na jpya ngoja tusubiri hizo siku.
 
Mkuu asante sana! Nadhani Mods watusaidie ikiwa jamaa hatathibitisha apigwe life BAN.

Tena kwa kukazia hapo apigwe IP permanent BAN ili ashindwe kabisa hata kuchungulia JF as a guest.

Huyu jamaa amekuwa na maneno yake mengi ya kizushi na kichokozi ili tu kutafutia member wengine BAN bila kukusudia.
 
Mkuu unajua kabisa kwamba umri alionao(miaka 52) Bwana W.Malecela is inversely proportional to his thinking capacity,kwahiyo ni vizuri kumchukulia kama mtoto mdogo ambaye anafanya mzaha wa kijinga.Kikubwa zaidi mtoto mwenyewe bado anahitaji maelekezo ya watu wazima, ni vema kumsamehe bure!

Siamini kama w.Malecela ana miaka 52 huku unakula na kulala kwa baba. mmh!!!. Maana ni karibu sawa na umri wa baba yangu. I can't imagine baba yangu mwenye elimu ya msingi kama anaweza kufanya vitu kama anavyofanya bw Malecela.
 
Huyo mwana haram huyo ana matatizo ya akili!
Uwezo wake wa kufiri na umri wake haviko proportional kabisa
kumbe ndiyo maana wamagamba walimchinjia baharin
 
Back
Top Bottom