Tuhuma za upotoshaji mikopo ya Elimu ya Juu ni Uzushi. Ipuuzwe.!

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
Kuna habari inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kuwa mimi (Malisa), viongozi wa kitaifa wa Chadema na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi tumekula njama (conspirancy) za kufanya upotoshaji kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.

Baadhi ya viongozi waliotajwa kwenye andiko hilo ni Mhe.Freeman Mbowe (M/kiti taifa), Mhe.Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Ndg.Patrobas Katambi (M/kiti BAVICHA) na Ndg.Ben Saanane (Afisa wa chama). Mwandishi wa mwananchi ametajwa kwa jina la Tausi Mbowe.

Habari hiyo inadai mimi na mwandishi aitwae Tausi Mbowe tulikaa ofisi za Mwananchi na tukaandika taarifa potofu dhidi ya suala la utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, kwa kushirikiana na viongozi wa juu wa Chadema. Taarifa hiyo inaongeza kuwa Computer iliyotumika ni ya kwangu.

[HASHTAG]#UKWELI[/HASHTAG]:
1. Simfahamu mwandishi wa Mwananchi aitwaye Tausi Mbowe. Mimi na yeye hatufahamiani na hatujawahi kuonana.

2. Sijafanya mawasiliano yoyote (ama ya simu, barua pepe, au ya ana kwa ana) na viongozi wangu wakuu wa chama kuhusiana na suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

3. Tarehe inayotajwa katika andiko hilo sikuwepo ofisi za gazeti la Mwananchi.

4. Wiki hii yote sikuwepo Dar es Salaam (nimekua Kahama, Geita, Ngara na Tabora kwa nyakati tofauti).

5. Computer yangu haijawahi kutumiwa na Tausi Mbowe wala mwandishi mwingine yeyote wa Mwananchi kwa shughuli za kikazi au binafsi.

Naomba umma wa watanzania uelewe kuwa habari hiyo ni ya uongo, ya kutunga na yenye nia ya ovu (malice aforethought), iliyoandikwa kwa malengo yafuatayo:

1. Kuwaondoa watu kwenye mjadala juu ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

2. Kumgombanisha mwandishi wa Mwananchi Tausi Mbowe na Mwajiri wake (ili ionekane anatumika kisiasa kinyume na maadili yake ya kazi).

3. Kugombanisha uongozi wa juu wa Chadema na gazeti la Mwananchi.

4. Kupunguza imani ya watanzania dhidi ya gazeti makini la Mwananchi, na kuwaaminisha uongo kuwa gazeti hilo linatumika kisiasa.

5. Kujenga chuki dhidi ya Chadema na viongozi wake wakuu.

Hivyo basi naomba taarifa hiyo ipuuzwe maana haina ukweli wowote. Tafadhali wajulishe na wengine.

NB: Serikali itoe fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na iache kutafuta visingizio visivyo na tija. Nguvu zinazotumika kutunga uongo dhidi yetu, zingetumika tutafuta fedha za mikopo kwa wanafunzi waliokosa.

Malisa GJ
 
Tupo kwenye kipindi kigumu sana, serikali inakanusha, watu binafsi wanakanusha, hatujui tuamini lipi na tumwamini nani.

Siasa za namna hii kuukimbia ukweli na hali halisi hazitafika mbali.

Serikali ijikite kutatua changamoto na matatizo yanayolikabili taifa.
 
Usijali mkuu, mzushi wa habari hizo ni kinara wa uzushi hapa JF anafahamika kama Lizaboni. Huyu jamaa amebobea katika uzushi hadi ndani ya chama chake Ccm anafahanika.
Amewahi kuleta uzushi hadi wa kutaka kumgombanisha mwenyekiti wao mpya na Naibu katibu mkuu wao Luhwavi (jina naweza kuwa nimekosea kwani hakina umuhimu kwangu) kwa kumsingizia mambo mabaya sana akaouuzwa. Akamvamia Lukuvi akakwama. Kifupi ni mwongo na mzushi sana.
Wewe endelea tuu kutoa mchango wako achana na huyo ambaye hata Lumumba anaogopwa kama ukoma
 
Ni vema kuweka mambo sawa kama hivi; maana juhudi za hujuma za kutafuta wa kufa nae ni kubwa. Tusisahau teke la anayetolewa roho lazima jitihada za kufa na mtu zitamalaki.

Watawala wanasikia cha moto kwa kila jambo wanaloagiza kubuma, ubaya ni wamejiapiza kufa na mtu au kulipiza visasi kwa changamoto zilizothibitika zingetatuliwa na upinzani.

Ushauri wa bure; watawala wenye busara na hekima wanatumia human resource yo yote ili kufanikisha dira na dhamira ya taifa. Kwa bahati mbaya we do not share a national vission nor mission TUPO TUPO TU

ELIMU ELIMU ELIMU Inatuhusu
 
Swala lililopo ni umefichuliwa, vitu vingine havina haja ya kunyanyua kinywa bcoz ndio ujira wenu
 
Back
Top Bottom