Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,578
Wanabodi,

Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya!, hivyo mtu akiwa ni Msukuma kweli, kamwe hawezi kuwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kikanda, labda jinsia, na hili sio kosa lao, ni mfumo dume wa jamii za kiasili za kiafrika.

Declaration of Interest.
Mimi Paskali Mayalla ni Msukuma, na jina la Mayalla ni jina la ukoo toka kwa mababu na maana yake ni mtu aliyezaliwa wakati wa baa la njaa ( ukame, famine, drought), na sio njaa ya tumbo, au njaa ya shibe kama wengi walivyoaminishwa!, mimi binafsi japo ni Msukuma lakini sio mkabila, na huu ni uthibitisho wa jinsi ninavyopinga ukabila, hata kama ni ukabila wa Wasukuma na 'Wasukuma'.
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na ...

Wasukuma Sio Wakabila.
Sisi Wasukuma sio wakabila wa ule ukabila m-baya kwa kufanya ubaguzi wa kikabila au kindugu, yaani undugunaization wa nepotism, Wasukuma ni watu poa sana, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wachapa kazi, ndilo kabila linaloongoza kwa upendo, ndilo kabila linaloongoza kwa ukarimu, ndilo kabila linaloongoza kwa unyenyekevu, ndilo kabila linaloongoza kwa viongozi ambao they are "men of the people", yaani watu wa watu na down to earth. Hivyo ninavyoandika hapa simtetei Magufuli kwa vile ni Msukuma, namtetea kwa vile mambo mengine, wanamsingizia bure tuu huyu Msukuma wa watu!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A of the People...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...

The General Rule And The Exception to the Case.
Kwa vile ukanda, udini, na ukabila ni vitu ambavyo ni kweli vipo, na as a general rule, kabila la Wasukuma, hawana ukanda, ukabila wala udini, ila kila kwenye general rule, kuna the exceptional , hivyo pamoja na Wasukuma kuwa sio wabaguzi wa ukanda, udini na ukabila, there are always some exeption to the case , wakatokea Wasukuma wawili watatu, wakawa ni wabaguzi, wakabila na wadini, these are isolated individual cases, zisichukuliwe kulinyooshea kidole kabila lote, au Wasukuma wote, tena kwenye, hizo individual isolated cases, unaweza kabisa kukuta, hao wanaofanya hivyo, in actual facts, sio Wasukuma halisi, bali ni just porpoted to be Wasukuma!.

Wana Jamii Forums, We Have a Duty, Kupiga Vita, Ubaguzi Wowote, Udini, Ukanda na Ukabila.

Sisi wanamitandao ya kijamii lazima tufanye a responsible social networking ikiwemo kulisaidia taifa lisiangamizwe na sentiments zozote za ubaguzi au kibaguzi ziwe ni za Ukanda, Ukabila, Udini, rangi au jinsia!.

Swali la Msingi ni Jee Tanzania Tuna Ukanda, Udini na Ukabila?.
Kwanza tukubaliane sote in principle kuwa siasa zozote za Ukanda, Ukabila na Udini ni siasa muflisi, na watu wowote wanaotumia kete ya ukanda, udini na ukabila, ni watu waliofilisika kisiasa, hivyo ukanda, udini na ukabila ni tatizo detrimental kwa taifa letu, ni ugonjwa mbaya kabisa unaoweza kuliangamiza taifa letu and infact ni sumu!, a very poisonous Vernon!, hivyo tupaze sauti zetu juu mpaka mwisho wa uwezo wetu kukemea na kusema No kwa ukabila, no kwa ukanda, no kwa udini, and a BIG NO kwa ubaguzi wa aina yoyote humu nchini mwetu.

Lini Tumeanza Kukemea Ukanda, Ukabila na Udini?.
Baada ya Mhe. Tundu Lissu, kuzungumzia ukanda, udini na ukabila, ndio watu wanaanza sasa kuuzungumzia saana as if umeanzishwa na Magufuli!, no!, tukubali tukatae, ukanda upo, ukabila upo na udini upo siku nyingi kabla ya Magufuli, na ni tatizo, sema kitendo cha kuzungumzwa na Lisu, ndipo sasa people pays attention. Tembelea nyuzi hizi, angalia zilipandishwa lini, but no body paid any attention!.
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni ...
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...
Makabila makubwa vs Makabila madogo | JamiiForums | The Home of ...

Tunaondoaje Huu Ubaguzi wa Udini, Ukanda na Ukabila?.
Hatua ya kwanza ya kuondokana na ubaguzi huu, kwanza ni by acceptance kwa kulikubali tatizo na kuwa ni kweli lipo na sio by denial, kama siku zote tunavyofanya. Dawa ya tatizo ni kulikabili kwa kulichimba kiini chake hadi kwenye mizizi kisha kuling'oa.

Mimi naomba kukiri wazi kabisa kuwa ni miongoni mwa wana jf ambao tulibaini tangu siku nyingi kuwa taifa letu linanyemelewa na sumu za siasa za ukanda, udini na ukabila na nilisema wazi hapa.

Mwezi August Mwaka 2014, nilipotajiwa kwa mara ya kwanza, jina la mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015, kuna kitu kama nilikisikia na nikakisema hapa
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ...
Who paid attention to this thread, who bothered hata kuzisikia tuu sababu zenyewe?.
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...

Kwenye hoja za udikiteta wa rais Magufuli, pia kuna kitu nilikisema hapa ambacho ndicho pekee, kinaweza kumzuia Magufuli asiwe dikiteta kamili.
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's ...

Jee Ukanda, Udini na Ukabila ni Mbaya Tuu?, Hakuna Udini Mzuri, Ukanda Mziri na Ukabila Mzuri?.

Sio kila ukanda, udini na ukabila ni mbaya tuu, kuna udini mzuri na udini mbaya, kuna ukanda mzuri na ukanda mbaya na pia kuna ukabila mzuri na ukabila mbaya, lets make good use ya ukanda mzuri, ukabila mzuri na udini mzuri kwa maendeleo ya taifa letu.

Mfano, kabila la Wamakonde ndio mabingwa wa kuchonga vinyago, wachongaji mabingwa kabisa ni Wamakonde walioko Tanzania, Wakenya, Waganda, Rwanda na Burudi, wanakuja kununua vinyago Tanzania na kuvi export, hivyo kama tunataka kumiliki soko la vinyago, tuwaendeleze Wamakonde, na sio kabila jingine lolote!.

Miaka ya 70s Tanzania ilisifika sana kwa kutoa wakimbiaji bora, wakimbiaji wazuri ni watu wa makabila ya wafugaji na wawindani wa milimani, hivyo kina Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamish Shahanga, Juma Ikangaa, Zebedayo Bayo, Zakaria Barie, John Steven Akwaari, Restituta Joseph, Simon Naali etc, wote hawa ni watu wa kabila moja au jamii za wafugaji wa milimani, hivyo Tanzania tukitaka kujenga timu imara ya riadha, timu ya ushindi, lazima tuwaendeleze watu wa kabila hilo au jamii hizo.

Wakati wa Nyerere, watu wa makabila fulani walifanya vizuri kwenye maeneo fulani kuliko makabila mengine, mfano Jeshini na polisi ni watu wa Musoma/Mara.
Hakuna ubishi kuna dini ni wazuri kwa kukariri, ikitokea mashindano ya kukariri, tuwatumie hao!. Kuna makabila ni wazuri kwa kucheza ngoma hadi mabinti wao lazima wachezwe, tukiunda timu ya wachezo ngoma tuwatumie hao!. Kuna makabilsa ni wavivu, hawawezi kazi za mtulinga, zikitokea kazi za mtulinga, tuwaepuke. Sii wengi wanaojuo kuwa ujenzi wa reli ya kati, makuli walitoka India, baada ya juhudi za kuwatumia Waafrika kushindikana, walikuwa wakilipwa tuu mshahara wakwanza, ndio kimoja!. Hawa Wahindi waliojenga Uhindini kila reli ilipopita, walikuwa ni makuli na hayo magahoroma ni pesa za mishahara yao!.

Wachina walipojenga Tazara, makuli walitoka China, ila wao walikuwa very strictly, hakuna kuoa, hakuna kuzaa, hakuna kubaki, ukiona kuna machotara wowote wa Kichina kama wale wa Uwanja wa Taifa, ujue mama zao walifanya siri, walipopata ujauzito, Wachina hawatakagi kabisa ujinga, afadhali ya Magufuli mara 100, mtoto akipata ujauzito, anafukuzwa tuu shule na kugeuka mzazi, ukishika ijauzito wa Mchina na akajua, hatua ya kwanza the kid can never survive, kama umechelewa kusema, both the kid and the expectant mother, na Mchina mhusika hurudisha kwao kupokea kitanzi!, just wipe the race!.

Ukabila Mzuri Katika Uteuzi.
Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa kabisa nchini Tanzania, ndilo kabila lenye watu wengi zaidi, hivyo automatically, tukifuata principals of proportionality, Wasukuma ni lazima wawe wengi kila mahali, hii ni halali yao na sio upendeleo!.

Ukitokea wewe ni mteuzi, ukaletewa majina matatu wote wenye sifa sawa na mmoja wao ni Msukuma, jee utaogopa kumteua huyo Msukuma kwa sababu ya kuchelea utaonekana ni mkabila?, zikitokea nafasi, halafu kati ya walioomba wote, wenye sifa zaidi ni Wasukuma, then let it be, hata Wasukuma wakijazana sana, as long as ndio wenye sifa, then huu ni ukabila mzuri, hivyo natoa wito kwa JPM, endelea kuteua Wasukuma, wajaze kila mahali as long as ni watu wenye sifa na ni wachapa kazi, then wewe teua tuu, wanaosema waache waseme, watasema mchana msiku watalala.

Na ikitokea wewe ni Msukuma, ukakuta kuna home boy wako alishateuliwa na mtangulizi wako, inapotokea anazingiziwa au kutuhumiwa, kuna ubaya kumsaidia kama hapa?
Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya ...

Ukabila Mbaya Katika Uteuzi.
Ikitokea kuna nafasi za uteuzi, then ukaamua kwa makusudi kutafuta mtu wa kabila lako, ambaye hana sifa, lakini kwa vile ni kabila lako, unampandisha haraka haraka ili kumjengea sifa, kisha unamteua. Huu ni ukabila mbaya!.

Au kunatokea nafasi ya uteuzi, wewe unatafuta mtu wa kabila lako, ukimkosa, unakasirika, unaamua nafasi hiyo huteui mtu, bali unaikaimisha na kusubiria hadi mtu wa kabila lako atokee!. Huu ni ukabila mbaya.

Facts Kuhusu Dominant Tribes. Wasukuma The Biggest Tribe, The Best, The Kindest!
Pamoja na kuwepo kwa ukabila mzuri na ukabila mbaya, kuna kitu kinaitwa dorminabt tribes, hii ni fact, hatuwezi kuipuuzia, Wasukuma ndilo kabila kubwa kuliko makabila yote nchini Tanzania, na wamesambaa katika mikoa mingi kuliko kabila jingine lolote, na ukiwemo Mkoa mmoja tuu Tanzania nzima, ambao mkoa wote ni kabila moja tuu, Mkoa wa Shinyanga, hakuna mkoa mwingine wowote ambao ni mkoa mzima una watu wa kabila moja!.

Sababu ya Wasukuma Kuwa Wengi Zaidi Kuliko Makabila Yote.
Wingi wa watu unatokana na kitu kinachoitwa population growth, Wasukuma ndio wanaoongoza kwa highest population growth, sisi nyumbani kwetu kwa mama yangu tumezaliwa 8!, hivyo mwanamke wa Kisukuma kuzaa watoto 10-12 its normal, na hapa mama hakuwa peke yake!. Sababu ya uwepo wa chakula bora, kingi na cha kutosha, ndio maana unaiona miili ya Wasukuma sio miili ya njaa njaa, wanaume wa Kisukuma wana nguvu sana za ku service zaidi ya mwanamke mmoja, elimu duni maeneo mengi, kuoa wanawake wengi, kuzaa watoto wengi bado ni sifa kwa Wasukuma, mimi mwenyewe ninao watoto 8 na sio mwisho!, na kufuatia kuwepo kwa lishe bora, rate ya procreation iko juu, watoto wanazaliwa sana, infant mortality rate iko chini, watoto hawa hawafi, deathrate Usukumani iko low, na kuishi maisha marefu kutokana na kula vyakula vya asili, kunafanya Wasukuma kuishi maisha marefu sana. Ingefanywa sensa ya wazee Tanzania, tungekuta ni Wasukuma pia ndio wanaoongoza kwa maisha marefu!

Kati ya watu milioni 50 walio Tanzania, Wasukuma ni milioni 10, hivyo hii ni asilimia 20% ya Watanzania wote, hivyo tungefuata haki bin haki kwenye kila ofisi yenye watu watano, mmoja ilipaswa lazima awe Msukuma, hivyo piga hesabu ya kila sekta ulinganishe na idadi ya Wasukuma waliopaswa kuwepo, mkimuita jamaa ni mkabila kwa sababu tuu ya kuteua Wasukuma wawili watatu, huko kutakuwa ni kumuonea!.
Matokeo ya sensa: Tanzania ina watu 44,929,002! | JamiiForums ...
Kwanini Wasukuma wanachukuliwa kama kabila la kipekee Tanzania ...
Sifa mbaya za makabila yetu | Page 7 | JamiiForums | The Home of ...
Swali Chokonozi: Hivi ni kweli Mwanza ni Maskini kuliko hata ...
Makabila yetu: Vijana na wanawake wa Kisukuma | Page 7 ...
Eti Kisukuma kina wazungumzaji wengi kuliko Kiswahili | Page 2 ...

Udini Mbaya
Nchi hii ina watu wa dini tofauti wenye sifa, lakini katika uteuzi, unaletewa wenye sifa wa dini zote, wewe unawachagua wale wa dini yako tuu. Huu ni udini mbaya!.

Ubaguzi wa Kuwabagua Wapinzani.
Nasisitiza tena na tena kuwa Tanzania ni yetu sote, CCM na wapinzani wote ni Watanzania, na Tanzania ni nchi yetu sote, ndio maana hata kwenye siasa, Mkapa na Kikwete, waliteua wabunge kutoka upinzani kwenye nafasi za ubunge, mtu anajiapiza kuwa kamwe hatateua mpinzani, huu ni ubaguzi mbaya!, Wasukuma hatuko hivyo!. Kwa maoni yangu, yule mama angefaa zaidi kwenda bungeni kuliko kumpa u RC!.

Hata lile katazo la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, ni tangazo la kibaguzi wakati chama kingine kikiendelea na mikutano.

Kwenye hili mimi nimeshauri tuu
Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri ...
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ..

Udini mbaya tumeuzungumza sana humu
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi! | Page 4 ...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na ukabila; Ukemewe na kila mmoja wetu ...
Pasco - Unawezaje kusema maneno kama haya ? | Page 5 | JamiiForums ...
Jee Magufuli Kweli ni Mkanda, Mdini na Mkabila?.
Hili naomba nilisilijibu ili nisiingilie uhuru wa mahakama, kwa sababu tayari kuna kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hizi ila nawaomba tuu tusimlaumu Magufuli kutokana na kauli zake.
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...

Conclusion.
Naendelea kusisitiza kwa dhati ya moyo wangu, ukanda, ukabila na udini ni sumu katika taifa letu, katika kupigana na vita hivi, ukweli usemwe, na katika kuusema ukweli huo, haki itendeke, hata kama kuna mnyonge, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.

Tanzania ni yetu sote, kila mmoja wetu, ana wajibu wa kuhakisha Tanzania inapa ustawi na maendeleo kwa kujengwa, kulindwa na kustawishwa na sisi Watanzania wenyewe, and it can be done if kila mmoja wetu, will play his part, this is my part
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni.

Wasalaam.

Paskali
 
Msukuma kuamua kesi dhidi ya wasukuma ni sawa na kesi ya nyani kumpelekea ngedere.

Hakujawi kutokea ukabila mzuri hata uupake rangi nzuri kiasi gani. Hata kipindi cha Nyerere kuwa na wanajeshi wengi kutoka Mara haikuwa sawa na haikuwa na maana kuwa watu wa Mara ndio wanafaa zaidi kuwa wanajeshi. Kila mtanzania awe na haki sawa bila upendeleo.Mbona leo hii kuna wanajeshi kibao kutoka kila kona ya nchi na wanafanya vizuri?

Mifano yako mingi uliyotoa haina tija kabisa. Kwa mfano umetolea mfano wa kuendeleza wamakonde na wanariadha kutoka jamii za wafugaji na wawindaji wa milimani eti kisa wengi wao wana historia ya kufanya vizuri kwenye maeneo hayo.

Mifano hii ni old fashioned ,kwa dhama hizi ambazo tunaamini any one can be anything he/she want as long as he/she works on it. Siku hizi kipaji sio kila kitu, watu wanaamini sana katika bidii na kujifunza, mengine yote yatakuja kama maji yanavyotiririka mtoni.

Hiyo mifano yako haifanyi kuwepo kwa ukabila/ukanda mzuri ilimradi kila mtu akipewa fursa akitia bidii anaweza kufanya lolote bila kujali anatokea wapi.

Nenda kajipange na wasukuma wenzio ndio urudi tena.
 
Raisi aambiwe ukweli aache kuteua viongozi kwa kuangalia dini na ukabila hakuna dhambi mbaya kama ubaguzi. Tanzania ni yetu sote siyo mtu mmoja anajiona anaweza kufanya anavyotaka nchi hii inaongozwa kwa kufuata katiba siyo matakwa ya mtu mmoja ambaye ameshalewa madaraka.
 
Raisi hateui viongozi kwa kuangalia dini au kabila. raisi anateua viongozi kwa kuzingatia sifa na uwezo wa kazi
 
Wanabodi,
Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila mbaya!.

Sisi wanamitandao ya kijamii lazima tufanye a responsible social networking ikiwemo kulisaidia taifa lisiangamizwe na sentiments zozote za ubaguzi au kibaguzi ziwe ni za Ukanda, Ukabila au Udini.

Kwanza tukubaliane sote in principle kuwa siasa zozote za Ukanda, Ukabila na Udini ni tatizo na ni detrimental, ni ugonjwa mbaya Kabisa kwa taifa letu and infact ni sumu!, a very poisonous Vernon!.

Watu wanaizungumza sasa kwa vile imezungumzwa na Lissu, lakini tukubali tukatae, ukanda upo, ukabila upo na udini upo na ni tatizo.

Hatua ya kwanza ya kuondokana na ubaguzi huu, kwanza ni by acceptance kwa kulikubali tatizo na kuwa ni kweli lipo na sio by denial, kama siku zote tunavyofanya. Dawa ya tatizo ni kulikabili kwa kulichimba kiini chake hadi kwenye mizizi kisha kuling'oa.

Mimi naomba kukiri wazi kabisa kuwa ni miongoni mwa wana jf ambao tulibaini tangu siku nyingi kuwa taifa letu linanyemelewa na sumu za siasa za ukanda, udini na ukabila na nilisema wazi hapa.

Mwezi August Mwaka 2014, nilipotajiwa kwa mara ya kwanza, jina la mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015, kuna kitu kama nilikisikia na nikakisema hapa

Hivyo ni kweli kabisa kuna udini mzuri na udini mbaya, kuna ukanda mzuri na ukanda mbaya na pia kuna ukabila mzuri na ukabila mbaya, lets make good use ya ukanda mzuri, ukabila mzuri na udini mzuri kwa maendeleo ya taifa letu.

Mfano, kabila la Wamakonde ndio mabingwa wa kuchonga vinyago, wachongaji mabingwa kabisa ni Wamakonde walioko Tanzania, Wakenya, Waganda, Rwanda na Burudi, wanakuja kununua vinyago Tanzania na kuvi export, hivyo kama tunataka kumiliki soko la vinyago, tuwaendeleze Wamakonde, na sio kabila jingine lolote!.

Miaka ya 70s Tanzania ilisifika sana kwa kutoa wakimbiaji bora, wakimbiaji wazuri ni watu wa makabila ya wafugaji na wawindani wa milimani, hivyo kina Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamish Shahanga, Juma Ikangaa, Zebedayo Bayo, Zakaria Barie, John Steven Akwaari, Restituta Joseph, Simon Naali etc, wote hawa ni watu wa kabila moja au jamii za wafugaji wa milimani, hivyo Tanzania tukitaka kujenga timu imara ya riadha, timu ya ushindi, lazima tuwaendeleze watu wa kabila hilo au jamii hizo.

Wakati wa Nyerere, watu wa makabila fulani walifanya vizuri kwenye maeneo fulani kuliko makabila mengine, mfano Jeshini na polisi ni watu wa Musoma/Mara.

Ukabila Mzuri Katika Uteuzi.
Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa kabisa nchini Tanzania, ndilo kabila lenye watu wengi zaidi, hivyo automatically, tukifuata principals of proportionality, Wasukuma ni lazima wawe wengi kila mahali, hii ni halali yao na sio upendeleo!.

Ukitokea wewe ni mteuzi, ukaletewa majina matatu wote wenye sifa sawa na mmoja wao ni Msukuma, jee utaogopa kumteua huyo Msukuma kwa sababu ya kuchelea utaonekana ni mkabila?, zikitokea nafasi, halafu kati ya walioomba wote, wenye sifa zaidi ni Wasukuma, then let it be, hata Wasukuma wakijazana sana, as long as ndio wenye sifa, then huu ni ukabila mzuri, hivyo natoa wito kwa JPM, endelea kuteua Wasukuma, wajaze kila mahali as long as ni watu wenye sifa na ni wachapa kazi, then wewe teua tuu, wanaosema waache waseme, watasema mchana msiku watalala.

Ukabila Mbaya Katika Uteuzi.
Ikitokea kuna nafasi za uteuzi, then ukaamua kwa makusudi kutafuta mtu wa kabila lako, ambaye hana sifa, lakini kwa vile ni kabila lako, unampa

Inaendelea....
Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila mbaya!.... Paskal nadhani ni kwa vile wasukuma siyo wasomi, hawako katika makabila yenye wasomi; hawakuwa na opportunity ya kufanya ukabila. Now the opportunity has offered itself! One is making an effective use of it.
 
Siku na sisi tukiingia tutawajaza ndugu zetu......
 
Raisi hateui viongozi kwa kuangalia dini au kabila. raisi anateua viongozi kwa kuzingatia sifa na uwezo wa kazi
Kwa hiyo wateule wote kwenye ngazi za juu walioteuliwa hakuna kabila lingine ambalo lilikuwa na sifa na uwezo isipokuwa ukanda wa huko kwake? Ameteua ndugu mpwa zake wawili kwenye wizara moja ndo hao walikuwa na sifa tuu? acheni kutetea upuuzi.
 
Unashauri wamakonde waendelezwe kwenye stadi za kuchonga vinyago na Wairaqw/Wabarbaig waendelezwe kwenye riadha hata kama wanataaluma za kutosha lakini wasukuma ambao kimsingi ni wakulima wa majaruba ya mpunga/pamba na wafugaji wasiendelezwe katika secta hizo badala yake wawe wanateuliwa katika nafasi zote nyeti serikali kwa kuwa tu Rais ametokea ukanda huo? Real? Kwanini na wao wasiendelezwe kwenye ufugaji na kilimo?
 
Back
Top Bottom