Tuhuma za ugaidi dhidi ya Mbowe zimeonesha picha kamili CHADEMA sio chama makini, kimejaa wapiga kelele

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kama kweli chama makini lazima kiwe na watu makini basi Chadema ni chama mfu. Hakina watu makini kimejaza wapiga kelele wasiojitambua.

Mwenyekiti wao amepata tuhuma, tena tuhuma nzito. Wao kama wanajumuia wa Chadema tulitalajia watupe mrejesho kuwa Mbowe kama chairman na mfanyabiashara mahiri ahusiki na kuprovide fund ili kudhamini ugaidi.

Wanachadema wamebaki kulalama na kuporomosha matusi, mara Igp ni mbambikiazi kesi, mara mama Samia ni dictator. Haya yanasaidia nini?

Kama hahusiki hebu njooni wazi na ushahidi kama hakufanya conspiracy na kutoa fund kwa ajili ya ugaidi. Njooni na hoja za kisheria kudisprove wanachotaka kuprove Jamhuri.

My take: Wanachadema acheni matusi na kashfa zisizo na kichwa wala miguu. Hoja za kisheria hujibiwa kwa hoja za kisheria.
 
Siku hizi wanachukua mabox wanaandika Mbowe siyo gaidi, tunataka Katiba mpya. Hayo mabox wanawapigisha nayo picha watu kama watano wasiojielewa wanayarusha kwenye mitandao ya kijamii na kujinadi kwamba Watanzania waandamana huko Morogoro wakitaka Mbowe aachiwe huru na kudai Katiba mpya, wanawapigisha tena picha na mabox tofauti watu wa eneo lile lile na kurusha mitandaoni eti Watanzania huko Tarime wanadai Katiba mpya na kusema Mbowe si gaidi. Chadema huo utapeli mtauacha lini? Sisi tunadhinda humu mijini mbona hayo maandamano ya wananchi hatuyaoni?
 
Kuhusu chanjo mmeufyata. Vipi umeshachanjwa Idugunde?
 
KWA HIYO WEWE NDIO SHERIA?

Kesi iko mahakamani Lakini tafsiri ya sheria ndio itatupa umma ukweli wa tuhuma dhidi ya Mbowe, Hata kama wanaotawala hawana haki katika kutenda kwao lakini Mungu wa haki anaenda kuuthihirishia umma kwa mara nyingine tena kwamba HADHIHAKIWI.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kama kweli chama makini lazima kiwe na watu makini basi Chadema ni chama mfu. Hakina watu makini kimejaza wapiga kelele wasiojitambua.

Mwenyekiti wao amepata tuhuma, tena tuhuma nzito. Wao kama wanajumuia wa Chadema tulitalajia watupe mrejesho kuwa Mbowe kama chairman na mfanyabiashara mahiri ahusiki na kuprovide fund ili kudhamini ugaidi.

Wanachadema wamebaki kulalama na kuporomosha matusi, mara Igp ni mbambikiazi kesi, mara mama Samia ni dictator. Haya yanasaidia nini?

Kama hahusiki hebu njooni wazi na ushahidi kama hakufanya conspiracy na kutoa fund kwa ajili ya ugaidi. Njooni na hoja za kisheria kudisprove wanachotaka kuprove Jamhuri.

My take: Wanachadema acheni matusi na kashfa zisizo na kichwa wala miguu. Hoja za kisheria hujibiwa kwa hoja za kisheria.
Wakuletee weye? Ili utoe hukumu? Mweeee 🤣
Labda ukienda kuwaelezea walioko Mirembe wataweza kukupokea kwa shangwe
 
Siku hizi wanachukua mabox wanaandika Mbowe siyo gaidi, tunataka Katiba mpya. Hayo mabox wanawapigisha nayo picha watu kama watano wasiojielewa wanayarusha kwenye mitandao ya kijamii na kujinadi kwamba Watanzania waandamana huko Morogoro wakitaka Mbowe aachiwe huru na kudai Katiba mpya, wanawapigisha tena picha na mabox tofauti watu wa eneo lile lile na kurusha mitandaoni eti Watanzania huko Tarime wanadai Katiba mpya na kusema Mbowe si gaidi. Chadema huo utapeli mtauacha lini? Sisi tunadhinda humu mijini mbona hayo maandamano ya wananchi hatuyaoni?
Umesema ukweli kabisa. Chadema ni wahuni. Mmoja anayefanya uhuni huo wa kupost picha na taarifa za hadaa na uongo ni Erythrocyte. Tumpuuzeni.
 
Kama kweli chama makini lazima kiwe na watu makini basi Chadema ni chama mfu. Hakina watu makini kimejaza wapiga kelele wasiojitambua.

Mwenyekiti wao amepata tuhuma, tena tuhuma nzito. Wao kama wanajumuia wa Chadema tulitalajia watupe mrejesho kuwa Mbowe kama chairman na mfanyabiashara mahiri ahusiki na kuprovide fund ili kudhamini ugaidi.

Wanachadema wamebaki kulalama na kuporomosha matusi, mara Igp ni mbambikiazi kesi, mara mama Samia ni dictator. Haya yanasaidia nini?

Kama hahusiki hebu njooni wazi na ushahidi kama hakufanya conspiracy na kutoa fund kwa ajili ya ugaidi. Njooni na hoja za kisheria kudisprove wanachotaka kuprove Jamhuri.

My take: Wanachadema acheni matusi na kashfa zisizo na kichwa wala miguu. Hoja za kisheria hujibiwa kwa hoja za kisheria.

Umebaki unashabikia siasa za kijinga na matumizi mabovu ya pesa za umma kwa kesi za kubambikia. iGP alisema atatoa taarifa ya mtu aliyejiunganishia bomba la mafuta ndani ya siku 7. Hajafanya hivyo na nchi imekula hasara ya kutosha. Badala ya ya rais na IGP kujishughulisha na wizi ule, wanatumia nguvu kubwa kwenye jambo la kutunga, huku pesa za umma zikitumika kwenye siasa za kipuuzi kabisa.

Na ww ulivyo mjinga unakuja na li uzi lirefu kudhani wote ni watoto wa kuamini huo upuuzi wa viongozi majizi ya kura. Eti cdm watoe ushahidi, watoe ushahidi kwenye siasa za kitoto?
 
UJUMBE KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, SERIKALI, JESHI LA POLISI, VYAMA VYA CCM, CHADEMA, ACT, CUF, NA VINGINEVYO.

Sisi viongozi wa kiroho kutoka madhehebu yote ya dini nchini tupatao 24,000 kutoka Wilaya na Mikoa yote ya Tanzania chini ya Kamati yetu ya Kitaifa ya pamoja kwa Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, wawakilishi wao tunakutana leo kwenye Kongamano la Dua Kijiji cha Bagamoyo, kilichopo Madale, Dar es Salaam kwa ajili ya Dua.

Pamoja na kazi yetu ya kufanya Dua ya kuiombea nchi yetu na Taifa letu, wajibu wetu pia ni kuonya, kukemea vitendo viovu, kutoa ushauri muhimu kama huu wa leo kwenu ninyi tuliowataja hapo juu. Kumbukeni kuwa mbele zake Mungu Mwenyezi, aliye Mungu wa wote wenye mwili, hakuna mkubwa wala mdogo, mwenye nguvu wala dhaifu, Rais wala Mjumbe wa Nyumba Kumi. Sisi sote tunamhitaji Mungu kwa ulinzi, afya na nguvu!

Hivi karibuni, tumeshuhudia mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa viongozi wa Serikali unaokwenda sambamba na uporaji wa mali za umma, maneno ya vitisho yasiyozingatia Sheria, umri, maadili ya uongozi, na kiburi cha vyeo. Mbaya zaidi, mambo hayo yanaligawa Taifa kwa kasi kubwa. Aidha vitendo vya kutowasikiliza wenye nchi vimerudi kwa kasi pia. Watu wanapiga kelele kulalamikia tozo kubwa kwenye Gesi na simu lakini wananchi hawajasikilizwa. Wamesema kupanda kwa Gesi kunahatarisha misitu kutokana na matumizi makubwa ya mkaa. Hili limekuwa butu kujibiwa. Hii ni ishara mbaya. Kama mwenye nchi hasikilizwi, anasikilizwa nani?

Tumesikia kauli kali zinazochochea hasira upande wa pili. Kauli hizi zinatoka kwa IGP Simon Sirro kwamba viongozi wanasiasa [wa CHADEMA] na wanachama wao wasiende Mahakamani siku ambayo Mheshimiwa Mbowe atafikishwa Mahakamani. Hili ni moja ya mambo yanayodhihirisha mmomonyoko wa maadili ya weredi wa kazi.

IGP Simon Sirro ameingilia mhimili usio wake kwani Mahakama inao utaratibu mzuri wa kutafuta eneo kubwa ili wananchi wanaofika kusikiliza wapate nafasi hiyo. IGP Simon Sirro alipashwa kushauri kwa kusema; Ndugu zangu, tupo kwenye mazingira ya ugonjwa wa Corona, hivyo tunawaomba mchukue tahadhari kwa kwenda wachache Mahakamani huku mkiwa mmevaa barakoa, badala ya kutoa matamko ya kuwaua na kuwavunja miguu.

Tumbuke Wosia wa Mwalimu Nyerere usemao: 'Moyo kabla ya Silaha'. Vitedo vyote vinavyolalamikiwa na Watanzania kuhusu Jeshi la Polisi vinatokana na kukikuka Wosia wa Mwalimu Nyerere. Ushauri wetu kwa IGP Sirro ni kuwa alirudishe Jeshi la Polisi kwa Wananchi ili liwe ni Jeshi la kulinda raia na mali zao na siyo Jeshi la kuua raia wasio na hatia na kuvunja miguu yao. Kwa kuwa yeye ni Mkristo, atakuwa anajua kwamba Mungu Mwenyezi ni Mungu wa Haki. Tazama, wote washikao upanga wataangamia kwa upanga (Mathayo 26:52). Hata wale wanaowatuma wengine kutumia silaha, watambue kuwa ipo siku ya kesho. Tunatarajia kuwa ujumbe, ushauri na maonyo haya yatazingatiwa na wote tuliowataja hapo juu.

Tunaagiza kuwa Waraka huu usambazwe ili kila Mtanzania ausome kwa lengo la kulinda ustawi wa nchi yetu.

Ni sisi Viongozi wa Dini nchini Tanzania:
Askofu William Mwamalanga
Sheikh Alhaji Abubakar Muhidin Ramadhani
Sheikh Salleh Mussa
Askofu Aizeck Mgaya Kimweri
Padre Dr. Maxwell Furahisha
 
Back
Top Bottom