Tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kumpelekea Dkt. Ryoba kubwaga manyanga

Ni eneo gani la serikali ambalo halina vijana wa TISS? Je hakuna ufisadi? watu wanachomoa pesa hadi benki kuu na TISS wamejazana kibao, mbona nilifikiri una akili kuzidi hii comment yako?

Na kwa taarifa yako kilichosababisha aombe kujiudhuru ni kutokana na mwenendo wa uchunguzi unaoenda kuwatia hatiani maana yeye kama msimamizi na pay master wa serikali lazima awajibike kwa uzembe uwe wa kujua au wa kutokujua.
Na nyie mlikuwa wapi? Kwa nini hamkufichuwa ufisadi huo hapo kabla ili kuonyesha kweli Ni wazalendo wa nchi hii. Ukianza kuweka mambo hadharani wakati huu wa uchunguzi huoni kwamba Kuna kitu unakitengeneza ambacho kimsingi kinaweza kuathiri uchunguzi wenyewe? Ninajaribu kuwaza tu.
 
Wale wanaodai wakati wa Magufuli alikomesha ufisadi na kumsifu kiasi cha kutamani kumuabudu waje hapa kumtetea yule mungu wao iliwezekana vipi kufanyika ufisadi kama huo?

Kila mara tunasema yule mtu alikuwa anatumia nguvu nyingi kuficha matendo maovu yaliyokuwa yakifanyika ili apate sifa nzuri lakini wapambe mlikuwa mnabisha.
Tatizo hatusomi habari na tunarukia tu kishabiki Magu hakuwa Mungu kuwa ajue kila kinachofanywa katika taasisi za umma hata ungekuwa wewe usingeweza ndio maana ya kuwa na wasaidizi na hapo kama umesoma vizuri kuna kampuni ipo kuanzia 1999 hadi leo, hakuna mtu peke yake ambaye anaweza kumaliza tatizo la rushwa duniani,hata huko kwa wenzetu ambako kila kitu kipo kimfumo bado tatizo la rushwa lipo, rushwa ipo kuanziakale sawa na biashara ya ukahaba, kinachofanyika ni juhudi za pamoja za kupunguza rushwa, Magu amefanya yake wacha apumzike ni raisi bora kabisa kutokea hapa Tanzania,upende usipende ndivyo hivyo, mnaojaribu kumchafua mnajidanganya bure kama akina february Marope na genge lake.
 
Mtoto wako anaumwa ETI baba yy hajui kama mwanae anaumwa? Wamezidia kete tu hapo
Ndo ushangae. Huyu Rioba anayajua yote haya na bila shaka ndo kamtuma mleta Uzi aje kumsafisha hapa. Hatudanganyiki,tunawajua CCM wote ni majizi hakuna cha Rioba ni msafi hapa.
 
... waliwezaje kufanya ufisadi wote huo kipindi cha "asiyejaribiwa; alfa na omega"? Kipindi ambacho iliaminika ni Tanzania pekee ambapo dhambi ya rushwa/ufisadi haikuwahi kufanyika chini ya Mbingu? Kwamba Bwana Mungu "akichungulia" kutokea Kiti cha Enzi ni Tanzania pekee ambapo hakuiona dhambi ya rushwa?
TBCCM.
Wenyewe kwa wenyewe aina madhara.
 
Macbook Pro 16" Laptop- Apple bei ya mtandaoni kwa sasa ni TZS 8,058,197.00. Kwenye orodha ya TBC ni TZS12 milioni na ushee! Na hiyo bei ya mwaka jana.
Mmezidi majungu. yaani, bei ya biashara hizi za ku tender mnataka ifanane na ya mtaani? Hamjui risk ya hizi biashara?
 
Kwa ufisadi huu mnaachiaje nchi kwa kura? Mnaachiaje nchi iwe na tume huru na katiba mpya?
 
BAADHI YA TUHUMA ZINAZODAIWA KUMPELEKEA DR. AYUBU RYOBA KUJIUZULU
  • Yeye binafsi hana tuhuma za moja kwa moja, anawajibika kwa matumizi mabaya ya ofisi yaliyofanywa na wasaidizi wake.
  • Wasaidizi hao kwa uchache ni Mkurugenzi wa Manunuzi na Mkuu wa Sattelite.
  • Tayari baadhi yao wamekuwa wakihojiwa na TAKUKURU.
  • Makampuni Zaidi ya matatu yamekuwa yakihusika katika kupata zabuni bila kufuata sheria.
  • Na Kampuni hizo zimekuwa zikiweka bei hadi mara tatu ya bei halisi za sokoni.
  • Kampuni hizo moja wapo ni ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA), JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES (TANZANIA).
  • Ipo miradi mingi imetekelezwa kwa mabilioni ya pesa za walipa kodi nab ado haifanyi kazi, nitajaribu kuelezea michache.
  • Pia Channel ya SAFARI imekubwa na matumizi mabaya ya pesa, yaani UFISADI.
Sote tunafahamu tetesi zilizosambaa juzi kati kuwa Mkurugenzi wa TBC, Dr. Ayubu Chacha Ryoba amejiuzulu. Ni kweli alijiuzulu na kuchukua likizo ya muda mfupi.

Sababu ya kujiuzulu ni kuwajibika kwa matumizi mabaya ya ofisi ambayo yamekuwa yakifanywa hasa na wasaidizi wake, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Manunuzi, na Mkuu wa Sattelite. Wawili hawa wamekuwa wakishirikiana na kampuni za ndani na nje katika kuibua miradi na kulipa mabilioni ya pesa huko ubora wa TBC ukiwa hauboreki licha ya serikali kuwapa mabilioni kila mwaka.

KUHOJIWA NA TAKUKURU
Baada ya Taarifa kumfikia Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa K. Majaliwa aliagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi katika baadhi ya Tuhuma walizopelekewa na katika baadhi ya miradi iliyotekelezwa na kampuni tatu: ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA), JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES (TANZANIA).

Katika mahojiano hayo kuna mambo kadhaa wameyabaini na bado wanaendelea kuyachunguza, nitajaribu kugusua hizi kampuni zao na uhusika wake kwa ufupi.

ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA)
Hizi ni kampuni pacha zinazoshirikiana katika kufanya kazi za kinyume na sheria TBC. Sheria ya manunuzi ya umma inakataza kampuni ambayo imeshiriki kuandaa tender nayo kuwa sehemu ya kuomba tender.

Ambacho wamekuwa wanafanya ni kuwa; TBC wakitaka kutekeleza mradi wanamuomba ONSET ENGINEERING kutoa pendekezo la mradi, huyu ONSET anatoa vifaa na bajeti ya huo mradi, tender ikitangazwa haombi kupitia ONSET bali anaomba kupitia washirikia wake wanaoitwa ENERGY & TELECOM na wanaweka bei kubwa sababu tayari wanakuwa wameficha Technical Specifications za vifaa, hivyo waombaji wengine hata wakiwa na bei chini wanaambiwa wameshindwa kwenye Technical Specifications na mwisho wa siku mradi unaoweza kutekelezwa kwa bilioni moja kwa uhalisia wa bei ya soko unaweza kutekelezwa kwa bilioni 2 hadi 3. Na wahusika wananyamaza sababu wanafaidika. Na huyu ONSET amekuwa akifanya miradi ya TBC toka mwaka 1999. Hivyo kwa kuongezea TAKUKURU ichunguze miradi yake yote na bei ambazo amekuwa akilipwa.

WAMEKUWA WAKILIPWA KABLA YA UTEJELEZAJI WA MIRADI
Nitaweka mfano wa mradi mmoja kati ya mingi, hii kampuni ilipewa mradi wa kutengeneza Community Radio Jijini Dodoma kwa gharama ya 1.74 bilioni, kabla ya kutekeleza tayari TBC ikawalipa 1.72B Ikabaki just 20,000,000. Mradi huu ulikuwa uzinduliwe na Hayati Magufuli May 2020, lakini ulisuasua kwa muda mrefu huku Muisrael na washirika wake wa Tanzania wakisingizia Corona.

Community Radio haiwezi kugharimu 1.74 Bilioni kama hakuna upigaji kwa bei za kawaida. Zaidi ya yote ilikuwaje walipwe kabla ya utekelezaji kinyume na sheria za manunuzi ya Umma? Nafikiri TAKUKURU wamekwisha ifanyia kazi na wana majibu Zaidi.

NB: Muhimu miradi yote chini ya hawa watu ichunguzwe na watendaji wanaowajibika wote wawajibishwe.

JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES LTD
Hii kampuni ni kampuni inayoendeshwa kijanja kijanja, nafikiri wengi mnajua hizi kampuni zinazojiita General Enterprise, kwamba wao kila kitu wana supply, na kuna wakati serikali ilizipiga marufuku.

Kwanza hii kampuni sio ya kitaalamu katika kufanya supply ya mambo ya Broadcasting, haina wataalamu, workshop wala ofisi nzuri, ana stationery ambayo anasema ndio ofisi yake.

Hii kampuni imeingizwa kiujanja na Mkurugenzi wa Manunuzi TBC na Mkuu wa Sattelite, ambaye ndio amekuwa kama mmiliki wa hii kampuni.

Moja ya kashifa yake kubwa ni kupewa mradi wa Tender Na: PA/084/2019-2020/G/33 (attached their delivery note).

Mradi huu ulikuwa unahusisha Supply, Installation, Training and Commisioning of Studio Equipments wenye thamani ya 855,000,000.

Kampuni hii haikuwa ma mtaji, hivyo Mkurugenzi wa Manunuzi akawalazimisha watendaji wake wa chini kusaini nyaraka kuonyesha huyu Jemo tayari kafanya supply, kafanya installation na kafanya training hivyo anastahili kulipwa.

Mkurugenzi wa manunuzi akahakikisha Jemo analipwa pesa 100% ndipo akaenda kunua vifaa hivyo. Sasa baada ya kununua sababu hana utaalamu na hana wataalamu alienda akavibwaga TBC bila installation na training na hadi leo baadhi ya vifaa viko stoo havifanyi kazi iliyokusudiwa ila wao tayari maisha yao yanaenda kwa kuchezea pesa za walipa kodi.

Lakini Zaidi ni kinyume cha sheria ya manunuzi kumpa mzabuni pesa ndio akanunulie vifaa. Huyu Jemo hadi leo mtaji wake aliosajiri Brela unaonyesha kuwa ana mtaji wa milioni 5 toka alipoanzisha kampuni mwaka 2013, ina maana mtaji wake haukui wala hafanyi annual retirement na msajiri wa makampuni brela.

UFISADI SAFARI CHANNEL
Uchunguzi pia umebaini kuwa katika hii Safari Channel kuna ufisadi mkubwa sana na unamgusa moja kwa moja Mkurugenzi wa Manunuzi na Msimamizi wa Hii Channel.

HITIMISHO
Mabilioni ya pesa ambayo TBC inatumia kila mwaka hayaendani na ubora wa picha wala maudhui, kuna miradi mingi sana pale wanaiita White Elephants Project. Ni kweli Dr. Ayubu Ryoba sio mtu corrupt lakini ameshindwa kabisa kujua kuwa watendaji walio chini yake wanamzunguka na kufanya vitendo vya kifisadi.

Hivyo kama anawajibika awajibike lakini hawa watendaji wanaohujumu Shirika pindi TAKUKURU wakikamilisha Uchunguzi wao basi wapelekwe mahakamani.

View attachment 2015188
View attachment 2015189
Hii sasa ndio ulikua JF. Shukrani sana mleta mada
 
Du............... wakereketwa wamemwaga mboga!
Kazi kwako PM Majaliwa!

Kuna watu suruali leo hazitawatosha.
Huyo Mkurugenzi wa Manunuzi na Sattelite si mumtaje tu jina?
Tusije kunywa naye bia nasi tukadakwa!
Unamuamini Majaliwa?
 
Mimi sio mtaalamu kivile, ila kutokana na uzoefu kiasi wa kuhusika na masuala ya media nachelea kusema mtoa taarifa una information lakini kuna kitu unakificha aidha kwa kutokujua au kutokuelewa umesema vifaa vineletwa na vimewekwa stoo kutokana na kukosa wataalamu wa kufanya training na istallation, nimejaribu kupitia orodha tajwa hapo juu karibu asilimia 80% mpaka 85% (ya ninavyojijua mimi) vinaweza kutumika bila ya ujuzi wa ziada wala training ya ziada kwa mtu ambaye anafanya kazi kwenye media.

na hizo asilimia 10% mpaka 15% ya vifaa vilivyobaki, nina uhakika graduate wa telecommunication Engineering anaweza kuvifanyiwa installayion bila kuhitaji upekee huo unaosema.(na TBC wataalamu hawa wanao!)

hivyo kama vifaa vimetunzwa kwa ajili ya taratibu zingine za kiofisi ni bora useme, ila kuniambia kisa training na Installation nakataa, hakuna kifaa cha ajabu hapo asilimia 90% ni vya kawaida sana
 
Ayoub Rioba Chaha ni mtu safi kbs huyu jamaa hajui rushwa na sio mrushwa kabisa. Hana hata chembe ya ufisadi. Rioba tatizo lake kubwa hapo TBC ni kuleta aina ya uongozi ambao ulipaswa kupandikizwa taratibu. Aliingia na kuona baadhi ya watu hawafai kuwepo TBC na kujaza timu yake. Mtu ambaye ni muadilifu kama Rioba alitakiwa kuwa sehemu tofauti na hapo TBC ni dude moja kubwa sana. Wengine tulijua hawezi kudumu ama kukaa na watu wachafu na wezi. Kuna mkasa wa Suzan Mungy ambaye alifanya kitu tofauti na maagizo ya MD Rioba alichokifanya majibu yake aliyapata na yupo hapo alipo. Ayoub hapo anapigwa vita sana tena sana. Kwa hili nami namlaumu kwa uzembe wake inakuwaje unaongoza taasisi kubwa hivi nyaraka za zabuni ama malipo zinapita bila ya yeye kusitisha huo mchakato! Hapa anatakiwa kuwajibika kwa kufanyakazi kizembe. Endapo serikali inaweza kufanya uchunguzi wa kina huyu Rioba mimi nipo tayari hata kwenda kuapa popote sio Fisadi na wala hana tabia hizo. Ayoub hana siri ukijidai unampa siri ya dili ukae ukijua kuna siku ataitema mbele ya watu. RIOBA UNAWAJIBIKA KWA KUFANYAKAZI KIMAZOEA. ILA KAPU LA UFISADI HAUWEZI KULIBEBA HAUNA TABIA HIYO. Pole walikukosa Kasulu kwenye ajali ya gari watakupata kwa uongo wao huu.
 
Ayoub Rioba Chaha ni mtu safi kbs huyu jamaa hajui rushwa na sio mrushwa kabisa. Hana hata chembe ya ufisadi. Rioba tatizo lake kubwa hapo TBC ni kuleta aina ya uongozi ambao ulipaswa kupandikizwa taratibu. Aliingia na kuona baadhi ya watu hawafai kuwepo TBC na kujaza timu yake. Mtu ambaye ni muadilifu kama Rioba alitakiwa kuwa sehemu tofauti na hapo TBC ni dude moja kubwa sana. Wengine tulijua hawezi kudumu ama kukaa na watu wachafu na wezi. Kuna mkasa wa Suzan Mungy ambaye alifanya kitu tofauti na maagizo ya MD Rioba alichokifanya majibu yake aliyapata na yupo hapo alipo. Ayoub hapo anapigwa vita sana tena sana. Kwa hili nami namlaumu kwa uzembe wake inakuwaje unaongoza taasisi kubwa hivi nyaraka za zabuni ama malipo zinapita bila ya yeye kusitisha huo mchakato! Hapa anatakiwa kuwajibika kwa kufanyakazi kizembe. Endapo serikali inaweza kufanya uchunguzi wa kina huyu Rioba mimi nipo tayari hata kwenda kuapa popote sio Fisadi na wala hana tabia hizo. Ayoub hana siri ukijidai unampa siri ya dili ukae ukijua kuna siku ataitema mbele ya watu. RIOBA UNAWAJIBIKA KWA KUFANYAKAZI KIMAZOEA. ILA KAPU LA UFISADI HAUWEZI KULIBEBA HAUNA TABIA HIYO. Pole walikukosa Kasulu kwenye ajali ya gari watakupata kwa uongo wao huu.
Ni kweli Rioba sio fisadi. Hawa wa chini yake ndio tatizo. Na naamini akiwachukulia hatua mapema ingekuwa vyema kuliko yeye kukimbilia kujiudhuru.
 
Back
Top Bottom