Tuhuma za uchomaji wa makanisa, BAKWATA wamjia juu askofu laizer | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma za uchomaji wa makanisa, BAKWATA wamjia juu askofu laizer

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BigMan, Jun 13, 2012.

 1. B

  BigMan JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  BARAZA kuu la waislam nchini, BAKWATA, Mkoa wa Arusha, limemtaka Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri KKKT Dayosisi ya mkoani Arusha,Thomas Lazier, kuthibitisha madai yake aliyoyatoa hivi karibuni katika Vyombo vya habari ya kuwepo Vijana zaidi ya 300 wanaofanya mazoezi kwa ajili ya kuchoma makanisa na kuharibu mali mbalimbali zinazomilikiwa na makanisa mkoani Arusha vinginevyo Bakwata, itachukua hatua zinazostahili dhidi ya madai hayo.


  Kauli hiyo imetolewa na Shekh, wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Shaaba Juma,alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kufuatia taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari hivi karibuni zikimnukuu AskofuThomas Laizer, wa KKKT, akiwatuhumu Vijana zaidi ya 300, wa kiislam kuwa wanakusanyika kila siku na kufanya mazoezi ya Karate,kwa kujiandaa kuchoma na kuharibu makanisa mkoani Arusha.


  Shekh, Shaaban amesema Bakwata imeshitushwa na taarifa hizo za kuwepo kundi laVijana 300 wa kiislam,wanaofanya mazoezi ya Karate, katika msikiti ambao hakuutaja jina lake aliodai kuwa upo katika Eneo la Unga limited jijini Arusha, wanaofanya mazoezi kwa ajili ya kuchoma makanisa na kuharibi mali mbaklimbali zinazomilikiwa na makanisa..


  Alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa hiyo ya kusikitisha, aliitisha kikao na Mashekh , Maimam na walimu wa madrasa katika kata ya Unga limited ambapo viongozi hao walisikitishwa na taarifa hiyo ambayo walisema haina ukweli wowote na kama Askofu huyo anao ushahidi wakamtaka kutoa taarifa hiyo kwenye vyombo vya Ulinzi na Usalama ili ifanyiwe kazi.


  Shekh Shaaban, alisema kuwa amewasiliana na mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, ambae wamekubaliana kukutana siku ya Jumatano Julai 13 mwaka huu ili Askofu, huyo aweze kutoa ufafanuzi wa madai yake hayo mbele ya viongozi wa Dini na Serikali ili kupata ukweli wa madai hayo .


  "Mimi Shekh wa mkoa sina taarifa hizo ninaona taarifa hii ni ya hatari, inayolenga kuchafua Uislam na Waisam, nimefuatilia sijaona ukweli wowote kuhusu madai hayo, Kauli ya Askofu haifai kupuuzwa hata kidogo kwa sababu imetolewa na kiongozi mkubwa wa Kanisa" alisema Shehk shaaban.


  Shekh, shaaban, alisisitiza kwamba hakuna msikiti wenye Vijana 300 kama inavyodaiwa na Askofu huyo, wanaofanya mazoezi ya Karate,kwa ajili ya kuyachoma moto makanisa,na kufanya uharibifu wa mali kauli hiyo inalenga kuchonganisha Waislam na Wakiristo na serikali yao na hivyo kujenga Taswira mbaya dhidi ya Dini Kiislam.


  Akasisitiza kuwa Waislam na wasiokuwa waislam siku zote wameishi kama ndugu hivyo kauli hiyo isitumike kujenga fitina ya kuwagombanisha wananchi na kuvuruga amani na utulivu uliopo hapa nchini ambao umedumu kwa miaka mingi kwa kutambua kuwa kila mmoja ana uhuru wa kuabudu dini aitakayo.hivyo kama anazo taarifa sahihi aziwasilishe kwenye vyombo vya dola alisisitiza shehkh Shaaban.


  Hivi karibuni magazeti ya Habari leo la juni 4 na An –Nuur ya Ijumaa Juni 8 yenye vichwa vya habari tofauti yalimnukuu Askofu Laizer,ambapo gazeti la Habari leo liliandika Uamsho waibukia Dar es Salaam, wakati gazeti la An –Nuur ,likiandika Askofu Laizer, anawajua waliochoma moto makanisa hata hivyo baadhi ya viongozi wa makanisa wakiwemo mapadri, wamesema madai ya Askofu huyo yatapelekea kuwachonganisha waislam na dini zingne i kwa kuwa hakuifanyia utafiti.


  SOURCE: NIMEIKUTA KATIKA BLOG YA MWANDISHI WA HABARI WA NIPASHE INAYOFAHAMIKKA KAMA LIBENEKE LA KASKAZI
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Great Shekhe.

  Laziwa tuwape nidhamu hawa viongozi wa dini wanaochonganisha waumini.

  Too bad
   
 3. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,156
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280
  Nampongeza sheik Shabani kwa kufuatilia ili kuhakikisha kama hali hii inayosemwa na askofu ipo au la, ikiwa ni pamoja na kuvishauri vyombo vya dola kushughulikia hilo. Ninaamini atakuwa tayari kutoa ushirikiano wa kutosha endapo hali hiyo itabainika kuwa ni kweli. Hali kadhalika, ninaamini askofu laizer atakuwa tayari kuwajibika kwa alichokisema endapo itakuwa si kweli.
   
 4. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  udini unamea kwa kasi!
   
 5. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kauli chafuchafu za akina Ponda/Basaleh/Ilunga huwa zimetolewa na viongozi wadogo wa misikiti kwa hiyo haziihitaji kuthibitishwa?
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  Uchoche unaofanywa na magazeti yenu ya al nur,alhuda na redio imani mnaona sawa tu, wacheni hizo Tanzania ni ya wote Waslamu,Wakristo, waabudu mizimu na wasiokuwa na dini. Wacheni kucheza ngoma ya CCM ya kutugawa ili waendelee kutufisadi.
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Si kama propaganda zenu za magazeti ya msemakweli, na mengineyo dhidi ya uislamu pamoja na TV na redio zenu ambazo zimeshadidia propaganda ya kuchomwa makanisa hali ya kuwa wachomaji ni nyie wenyewe. Mlishazoea sana kuwa hii nchi ya kikristo wakati hii nchi yetu sote sasa wacheni moto uwake
   
 8. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wamezoea kuzusha hao sasa atatafuta pa kujificha
   
 9. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mods ondoeni hii kabla hamjatulima ban wenye haki ya kukasirika kutokana na uchokozi uliotuchosha wa mashetani hawa! ONDOA HII PLZ!
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Haya makanisa ndio yalikuwa kichocheo cha mauaji ya kimbari huko Rwanda. Huyu Askofu inabidi aoneshe ushahidi wa kauli zake.
   
 11. B

  Bob G JF Bronze Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwani serikali nayo imewakamata waliochoma makanisa? Bakwata hawana uwezo wa kumlazimisha Askofu Laizer Kuthibitisha, wao ndo wenyejukumu la kuwakamata waislamu wenzao waliochoma makanisa na kupora bia na kunywa
   
 12. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa dini wanahatarisha amani katika nchi hii na wanajua kama kusema uongo ni dhambi kwasababu itakuja kuchafua hali ya hewa na itamgusa kila mwananchi.Sisi wananchi hatujui kutafakari na kujiuliza ila tunaona ufahari kuingia ktk ugonjwa mbaya au sumu kali ya ubaguzi.Mwenyezi mungu atuepushe na majanga kwasababu jipu likipasuka basi ujue usaha na damu lazima zitatoka.

  GOD BLESS TANZANIA
   
 13. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145


  Katika kuhitimisha mizunguko ya kongamano za ki islamu mikoa yote Shehe Ilunga pale Diamond Jubilee aliwataka waislamu kote waliko kuacha kulalamika na badala yake kuanza kuwashughulikia viongozi wa kikristo, taasisi zao na maslahi yao mbali mbali popote yalipo. Alisema viongozi wa kiislamu wanabaki na jukumu moja tu la kushughulika na yatakayo tokana na kushughulika kwao. Alisema wanachoweza kushughulikia viongozi ni kama kutafuta mawakili n.k alitoa mifano ya sehemu ambazo waislamu tayari wameshughulika kuwa ni Mwanza (uchomaji wa makanisa) Mto wa Mbu (kuuwa kwa wachungaji 2) na Morogoro kwenye shule ya sekondari. Swali ni je unaweza kuchoma makanisa na taasisi za kikristo na kuua watumishi wa Mungu bila mazoezi ya awali?? aulizwe Shehe Ilunga anaweza kutoa ufafanuzi mzuri zaidi kuliko Laizer
   
 14. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  KENYA: TWO CHRISTIAN PASTORS BURNED TO DEATH AFTER VISITING MUSLIM FAMILY [Excerpts]

  "The umbrella body of evangelical churches and a human rights organization have condemned the lynching of two pastors at Jomvu in Mombasa early this week.

  Federation of Evangelical and Indigenous Christian Churches of Kenya asked the police to pursue the case up to the end, with the culprits arrested and charged in court.

  On Thursday, the federation's national chairman, Mr Joseph Methu, said punishment of killers of the two clerics in a case of mistaken identity should be used as an example to those who spearhead crime.

  "Time has come for the government to enforce the law and bring to book those who participated in the act that saw innocent pastors on a preaching mission burnt to death," said Mr Methu...

  As police continue with their investigations, there are conflicting reports by the church and Jitoni residents in Jomvu, where the two pastors were lynched.

  The pastor in charge of Melchidizek Church, Mr Samuel Wainaina, said the owner of the home the clerics visited was converted into a Christian a few weeks.

  His family, however, dismissed the conversion claim.

  Ms Mapenzi Abdalla, one of the members of Mr Mutana Nyandu's family, said they were all Muslims and no one had converted to Christianity as claimed by Pastor Wainaina.

  (Anthony Kitimo, [Kenya] Daily Nation, 5/17/2012)
   
 15. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Uzao wa 'kijakazi' unasikitisha sana...
   
 16. M

  Mngendalyasota Senior Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila ni hatari. MUNGU HUYU BWANA ALIUMBA WANADAMU NA KUWATOFAUTISHA KIFIKRA ILI WATAMBUE MEMA NA MABAYA!
   
 17. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,411
  Likes Received: 3,745
  Trophy Points: 280
  Wa jino kwa jino utawajuwa tu
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwani wana tofauti gani na wa sumu kwa sumu? Mnaleta propaganda zenu hapa mnadhani hatuwaelewi? Kizazi cha dot com kitawatoa jasho subirini tu!
   
Loading...