Tuhuma za rushwa ya ngono kwa madaktari bingwa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya

Status
Not open for further replies.
Mkuu, hili nalo neno. Ni vema tukasikia na upande wa pili (utetezi) kabla ya kutoa kauli za kuhukumu.

Pamoja na hayo, natoa pole kwa mhanga kwa masaibu yaliyompata (kama kweli)
Pole, unawajua wote,
Sema tuu ni wanoko , nawajua kwa sura na tabia hawapendi ujinga,,,
 
We jamaa nahakika unaongozwa na hisia tu kuliko ukweli, kumbuka hapo juu amesema pccb mbeya walipata na wakaanzisha uchunguzi so ndio maana kuna mahali nimemwambia aende HQ inafanyiwa kazi tokea juu sasa wewe unaleta habari za ujuaji
Hujui haya mambo! Kukusaida PCCB hata kitu kikiandikwa gazetini wao wanaanza kazi! Nina uhakikia kwa sasa watakuwa wamepata pa kuanzia si lazima upeleke malalamiko kama ilivyo Polisi.
 
hehe hatari.... bora hata nyie intern madaktari, kuna vile vibinti vinesi vyene diploma sijui certificate vikifika hospitali ndio vinachezewa na madaktari hatari, na vyenyewe vinavyoona sifa sasa kutembea na madaktari..,lakini madaktari wako safe sana. mkimaliza yenu mnakunywa PEP maisha yanaendelea
 
Hapa tungekuwa na media imara ilikuwa ndio muda wa kuchunguza kwa kina kisirisiri kama walivyofanya BBC kule Ghana na Nigeria hadi wale watuhumiwa wamekuwa suspended.
 
Hadi napata mawazo,mwanangu mpendwa wa kike maskini ndo anaanza form 1,cjui akijaaliwa kupataga ma chuo huko mbele watamfanya nini hawa majitu ya humo maofisini kwenye field,wacha nikomae mtt akitoka six salama aje kwa biashara yangu akae hapo na kk zake waendeleze mali,bora akubali kwa ridhaa yake kuliko kulazimishwa kisa tu eti apate alama nzuri
 
Hadi napata mawazo,mwanangu mpendwa wa kike maskini ndo anaanza form 1,cjui akijaaliwa kupataga ma chuo huko mbele watamfanya nini hawa majitu ya humo maofisini kwenye field,wacha nikomae mtt akitoka six salama aje kwa biashara yangu akae hapo na kk zake waendeleze mali,bora akubali kwa ridhaa yake kuliko kulazimishwa kisa tu eti apate alama nzuri
Ataliwa na mabaharia mtaani. Tena waendesha bodaboda .. hatari sana.
 
Mtoa maada Hongera kwa kuweka wazi.Ila Angalizo tu ni kwamba tayari umeshatangaza vita.maana kama hao uliowataja kwamba walikufanyia unyanyasaji tayari washakujua.Hivyo jihadhari kabla ya hatari.
Bila shaka atakuwa amesha hitimu utarajari, na hayo ndo kapitia.
 
Kuna mkuu mmoja wa s/m moja wilaya ya ilala alikuwa na hizi tabia ila serikali ilimnyoosha alikuwa anawapa shida sana walimu wa kike ukimkataa anakufanyia mambo ya ajabu uwapo kazini. Haya mambo yapo watoto wa kike wanapitia magumu sana hasa dunia ya sasa mpaka uje upate mke ujue
 
Take it a step further... Report TAKUKURU. Watakupa instructions za nini cha kufanya ili wakamatwe. Lakini hata wakikamatwa, siku hizi kuna kukiri mahakamani na kulipa faini ya mil 2 na kuyamaliza. Sad!
 
Hii ni habari ya kusikitisha sana.

Kwanza nimpongeze mleta mada kwa kuileta hapa na ameweka hadi majina ya wahusika. Ni imani yangu waziri mhusika ataliangalia hili kwa macho makali zaidi. Mabinti wana nyanyaswa-hata baada ya kusotea degree kwa miaka 5 mtu anawafanyia kitu mbaya. Cha kushangaza ni madakitari wenzao.

Je takukuru nayo itahitaji mtu akashitaki? Wangeweza kulifanyia kazi kimya kimya-naamini wana mbinu na stadi za kutosha kufanya hivyo.

Hili ni doa kubwa kwa referal hospital kubwa kama hiyo. Inaonekana kamchezo hako hakakuanza leo, hao lazima wadhibitiwe au sivyo mabinti wagome posting za huko waende kule walipo salalma. Na kwa vile interns ndio workhorses wa haya masipitali basi hospital itakuwa na shida. Hivyo ni wajibu wa board ya sipitali nayo kulifuatilia hili.

Kuna michango michache imejaribu kuhalalisha hivi vitendo. Supervisor wa intern anatakiwa awe mtu mwenye maadili na ajue kama ni mtego uko wapi. Kwa binti kujilengesha haihalalishi kuomba ngono. NI KOSA.

Baada ya hayo yote hivyo zile shutuma za UDSM ziliishia wapi? Au wakina baba wameteteana na kuzizika.

Mwisho kabisa nafikiri ni jukumu la kila chuo au training centre kuja na mikakati ya kukomesha vitendo hivi. Mbinu moja wapo supervisors na wahadhiri wasipewe nguvu kubwa ya kuamua peke yao ufaulu wa binti au kijana. Hii itapunguza haya mambo. Ukimpa madaraka makubwa ya maamuzi anakua mungu mtu.

Pongezi tena kwa mleta mada.
 
Hujui haya mambo! Kukusaida PCCB hata kitu kikiandikwa gazetini wao wanaanza kazi! Nina uhakikia kwa sasa watakuwa wamepata pa kuanzia si lazima upeleke malalamiko kama ilivyo Polisi.
Siko hapa kubishana na wewe au kuonyeshana kujua utaratibu, lakini naomba ufahamu iko tofauti ya kushughulikia malalamiko yaliyokuja kama taarifa na malalamiko yaliyoletwa na mlalamikaji kwamaana ya malalamiko yenye mlalamikaji uchunguzi wa awali unakuwa na ushahidi tofauti na malalamiko yaliyokuja kama taarifa ambayo watalazimika kufanya prior investigation, na pia malalamiko yasiyo na mlalamikaji lazima kutengeneza kwanza tuhuma yenye malalamiko so kama kwa ufahamu wako unadhani sio muhimu kureport pccb unajidanganya.

Hata hizo taarifa za magazetini kama mtoa taarifa gazetini ameweka mawasiliano yake anatafutwa ili kupata taarifa zaidi na ufafanuzi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom