Tuhuma za rushwa ya ngono kwa madaktari bingwa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya

Status
Not open for further replies.
nimesikitishwa sana na hizi tuhuma. Pole sana binti Pia nakusihi kumtanguliza Mungu mbele. Kupitia uzi wako naamini PCCB pamoja na watu wa usalama wataanza kulishughulia leo leo na wakithibitika kuhusika wafikishwe mahakamani wkapate haki yao
 
Pole Sana kwa masaiba hayoo.. Hopefully wahusika wanaoweza kuwawajibisha hawa madaktari wasio na maadili ya kazi wapo humu ndani..
 
Ahsante kwa kuwafumbua, ngoja tuingie kazini sasa!

Sasa daktari aliyepasishwa kwa rushwa ya ngono ataweza kuhudumia mgonjwa? Kuna mambo ya kuchezewa ila syo afya ya binadamu.
 
Takukuru ukireport wanamtafuta mhusika then wanaomba rushwa akiwapa ya maana wanakuzunguka so ndo hawafai kabisa
Usijali hilo nina agenda za siri yani mpaka huyo takukuru utasikia amedakwa kwa rushwa.
Stay tuned
 
Pole sana na Dada, ila Siku zote kila lenye mwanzo hua na mwisho wataswekwa ndani sio mda na ushenzi wao.
 
Teknolojia ya TEHAMA inaweza kusaidia katika hili.
1. CCTV camera Installation katika Public Offices
2. Tap mazungumzo kupitia Mobile phone.
Hii itasaidia Ku- support Evidences.
 
Naandika uzi huu kutoa experience yangu juu ya tuhuma za baadhi ya madaktari bingwa wa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya. Mimi nimemaliza internship hapo hivi karibuni.

Niseme tu, kati ya madaktari bingwa waliotajwa kuhusika, Dr. XXX wa Idara ya Medical ndie ambae naweza kumzungumzia, kwani alifanya maisha yangu kuwa magumu sana hapo wakati nafanya internship. Alikuwa akinisumbua kwa kunitongoza, na kunilazimisha nifanye nae mapenzi.

Mwanzoni alianza kwa kunibembeleza na kuniahidi vitu kibao kama vile kuniunganishia kazi sehemu baada ya kumaliza intern, na kuninunulia gari. Alipoona bado nimekuwa mgumu, ndipo sasa alipoanza vitisho na kuniambia kuwa atafanya maisha yangu ya internship yawe magumu kuliko ninavyofikiria. Ilifikia hatua ya kuongezewa wiki mbili zaidi Idara ya medical kwa madai kuwa siko competent, lakini sababu hasa ilikua ni kumkatalia penzi alilotaka kinguvu.

Huyu Dr XXX anapenda sana wanawake, na ana tabia ya kutembea na mabinti wanaopita hapo hospitali kama wanafunzi au interns, na ana vimada wengi ambao walipita hapo kama interns au wanafunzi. Baadhi yao amewaunganisha na ajira taasisi kama NIMRI kwa kutumia connections zake. Niwe mkweli kuwa pia baadhi ya mabinti hutumia udhaifu wake huo na kujipendekeza kwake, hivyo kuwa na mahusiano nae kimapenzi na kufanya maisha yao ya uanafunzi/intern kuwa ni mtelezo; lakini tunaokataa ndio ambao hupata shida na manyanyaso kutoka kwake.

Inasikitisha sana pale ambapo wasomi wa aina ya Dr XXX ambao wameaminiwa na jamii na serikali, wanapotumia nafasi zao kuridhisha matamanio yao ya kingono na kuwanyanyasa wale ambao wanakataa kuendana na matakwa yao.
 
Ukweli uatwaweka huru, naamini kama kweli ana tabia hiyo, kule kusikia tu amechanwa mtandaoni, nguvu za kiume zitamwisha ghafla mno!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom