Tuhuma za rushwa ya ngono kwa madaktari bingwa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya

Status
Not open for further replies.

Mleta amani

New Member
Joined
Dec 6, 2019
Messages
4
Points
75

Mleta amani

New Member
Joined Dec 6, 2019
4 75
Naandika malalamiko haya nikiwa ni mmoja wa wahanga wa hili.

Mimi ni daktari ambae nimemaliza mazoezi ya vitendo "internship" katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (Mbeya Zonal Referral Hospital).

Madaktari bingwa kutoka baadhi ya idara katika hospitali hii wamekua na tabia chafu ya kudai na kulazimisha rushwa ya ngono kutoka kwa madaktari wa kike wanaofanya mazoezi ya vitendo hospitalini hapo, ili waweze kuwapasisha wanapopita idarani kwao, na unapokataa kukubaliana nao, kinachofuata ni kufanya maisha yako kuwa magumu idarani kwao na hata saa zingine kukupa alama za kukufelisha.

Wanaofanya tabia hizi ni hawa wafuatao;
1.(Jina limehifadhiwa) wa idara ya medicine-Huyu binafsi alining'ang'aniza sana nimpe rushwa ya ngono, na alinihakikishia kuwa nisipompa penzi, alinihakikishia kuwa atanipa alama ya D kwenye idara yake.

Huyu daktari ni mshenzi sana na alifikia hatua ya kunifanyia sexual harrassment ofisini kwake kwa kunishika maeneo ya mwili wangu, lakini nilifanikiwa kumkimbia. Huyu daktari hii ni tabia yake, kwani kumekua na malalamiko ya aina hii juu yake hata kutoka kwa wanafunzi wa Chuo cha UDSM wa Medicine ambao hufanyia mazoezi ya vitendo hospitali hii.

2. (Jina limehifadhiwa) wa idara ya Upasuaji:Huyu nae ni mshenzi mwingine, kwani amekua akiomba rushwa ya ngono na hata kufikia kulazimisha na kuwapa 'alama chafu' wale ambao wanamkatalia ushenzi wake huo.

3.(Jina limehifadhiwa) wa Idara ya Mifupa (Orthopedics): Huyu ni kinara mwingine wa kulazimisha rushwa ya ngono kwa interns wanaopita idarani kwake na aliwahi kusikika akisema kuwa idarani kwake bila kutoa uchi mtoto wa kike hawezi kukupa alama nzuri.

4.(Jina limehifadhiwa) wa medical: Huyu pia huwa anashirikiana mwenzake katika kuwanyanyasa kingono interns wanaopita idarani kwake, yeye mara nyingi hupenda kuita interns wa kike ofisini kwake na kuwafanyia sexual harrassment kwa kuanza kuwashika maungo yao huku akitumia maneno ya kutishia kwamba wakiripoti basi wasahau kupata alama nzuri idara ya medical.

Pamoja na hayo, mkurugenzi wa hospitali hii Dr Godlove Mbwanji yeye amekua akifumbia macho tuhuma hizi, hata watu wakilalamika vipi, kazi yake ni kuwatetea tu hawa madaktari wake bingwa, badala ya kufanya uchunguzi wa ndani na huru juu ya tuhuma hizi, yeye ndiye amekua akiwakingia kifua madaktari hawa wahuni na washenzi wa tabia, na hivyo hata wakiwa wanafanya ushenzi wao, wengine huwaambia kabisa wahanga kwamba huna pa kukimbilia hivyo ni bora tu ukubaliane na mimi.

Naomba sana Serikali kupitia wizara ya Afya ifanyie kazi tuhuma hizi kwa kufanya uchunguzi wa wazi na huru, kwani hawa madaktari wana nguvu sana kutokana na nafasi zao, ni rahisi kuingilia taratibu za uchunguzi.


========

Moderator: Haya malalamiko, Uongozi wa JamiiForums umeyafikisha kwenye Mamlaka ya Serikali. Habari njema ni kwamba yameshaanza kufanyiwa kazi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU).

Tutazidi kutoa mrejesho kwa kila hatua inayofikiwa.

Tuendelee kutoa taarifa za rushwa ya ngono popote nchini kupitia hii thread hapa chini, nasi tutazifikisha na kufuatilia katika Mamlaka husika.


1576227436337.png
1576227479484.png
 

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Messages
1,837
Points
2,000

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2015
1,837 2,000
Kwanza nakupa pole sana maana mimi ni mdau mzuri wa pale hospitali inshort ni mkazi wa Mbeya mjini.

Peleka malalamiko yako ofisi ya takukuru kimyakimya au ikiwezekana nitafute mimi tusaidiane kuwawekea mitego pamoja na maafisa wa takukuru.

Mbona simple sana yani ulitakiwa kusema mapema maana mimi mwenyewe ni baba wa watoto 2 wakike wanasoma kwahiyo nimeumia sana.

Awamu hii ya 5 itawanyosha kama bado upo hapo rufaa nicheck inbox tuanze kazi.
 

logframe

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Messages
3,358
Points
2,000

logframe

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2014
3,358 2,000
Kwanza nakupa pole sana maana mimi ni mdau mzuri wa pale hospitali inshort ni mkazi wa Mbeya mjini.
Peleka malalamiko yako ofisi ya takukuru kimyakimya au ikiwezekana nitafute mimi tusaidiane kuwawekea mitego pamoja na maafisa wa takukuru.
Mbona simple sana yani ulitakiwa kusema mapema maana mimi mwenyewe ni baba wa watoto 2 wakike wanasoma kwahiyo nimeumia sana.
Awamu hii ya 5 itawanyosha kama bado upo hapo rufaa nicheck inbox tuanze kazi.
Haya ndio maneno.

Heko mkuu kwa hili, tukikaa kimya ni familia zetu zinaangamia.
Wanajifanya wapo bize kutongoza kwa ustaarabu hadi wawalazimishe kwa kutumia Taaluma zao.
What a barbaric mindset!
 

Mleta amani

New Member
Joined
Dec 6, 2019
Messages
4
Points
75

Mleta amani

New Member
Joined Dec 6, 2019
4 75
Kwanza nakupa pole sana maana mimi ni mdau mzuri wa pale hospitali inshort ni mkazi wa Mbeya mjini.

Peleka malalamiko yako ofisi ya takukuru kimyakimya au ikiwezekana nitafute mimi tusaidiane kuwawekea mitego pamoja na maafisa wa takukuru.

Mbona simple sana yani ulitakiwa kusema mapema maana mimi mwenyewe ni baba wa watoto 2 wakike wanasoma kwahiyo nimeumia sana.

Awamu hii ya 5 itawanyosha kama bado upo hapo rufaa nicheck inbox tuanze kazi.
Ahsante sana.
Lakini sio rahisi kama unavyosema, wakati bado nikiwa hapo hospitali tuliwahi ripoti TAKUKURU tukaweka na mtego vizuri, lakini mtego ulifyatuka,haukufanikiwa na inasemekana walikua tipped off na mmoja wa maafisa wa TAKUKURU aliekua anafahamu huo mchezo.

Kumbuka hawa ni madaktari bingwa,wamefanya kazi hapo Mbeya muda mrefu,wana connections za kutosha, kama ujuavyo tena kwa madaktari nadhani utaelewa kuwa ni rahisi wao kuwa na connections kiasi hiki. Inahitaji uchunguzi wa haki na wa uhakika na mipango dhabiti ili haki itendeke.

Nimeamua kulileta hapa nikiamini kuwa humu JF wahusika wa serikali na/au wizara ya afya wapo, wanaweza kufanya uchunguzi wao wa kimya kimya na kuchukua hatua.
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,390,031
Members 528,080
Posts 34,041,522
Top