Tuhuma za rushwa BAVICHA zipelekwe TAKUKURU - Zitto

utapompeleka mgombea takukuru halafu unasema aunganishwe ndani chini ya Heche una maana gani?

attempt za kutafuta ushawishi huwa zipo katika chaguzi zote...zipo zinazojulikana, na nyingine zisizojulikana...ndio maana hata mtu akishindwa uchaguzi kwa tuhuma za rushwa huwa hafungwi??

cost benefiti analysis - - - hii chapter ifungwe, tuangalie mbele!

Mungu mbariki Heche, Mungu Ibariki Chadema
 
Mbona siwasomi kabisa wazee!
Hiki chama si kinara wa kupamabana rushwa? Si kinatakiwa kiongoze kwa mifano?
Rushwa ilikuwepo kwenye uchaguzi ndio maana watu wakawa-disqualified...

Sasa kwa nini mnataka kuuficha huo uozo?
Au rushwa kwa magamba pekee kwa magwanda sio rushwa?
 
CDM msiwe wanafiki mwaka jana mlikuwa mnashupalia CCM walipoalila TAKUKURU katika uchaguzi wao wa ndani. Kama mpo safi kwa nini mwaogopa kuialika TAKUKURU au kwa sababu rushwa ilitolewa kama njugu kwa uwezeshaji wa mwenyekiti wa Chama HIVYO mwaona so.Kuweni na UJASIRI pelekeni maombi kwa TAKUKURU ili ukweli ujulikane, ZK mpeni pongezi kwa wazo zuri![/I][/SIZE]
Kama mtu wa kwanza wakupelekwa takukuru ni Zitto maana kuna ushahidi wa M-Pesa alizotuma kwa nini usishauri Zitto apelekwe?
 
Huyu Zito aondoke tu ndani ya chama chetu asifikiri yeye ni ndio chama huyu ndio chanzo cha kutaka kuweka makundi ndani ya chama hivi ZITO nani tufuate matamko yake DR SLAA KATIBU au WEWE NAIBU WAKE kila mtu anaongea kivyake tumechoka jirekebishe unapoteza mvuto kwetu angalia sana.
 
Hapo umenena! Lakini nadhani kwenda PCCB ni mbali mno! Hao waliotoa rushwa waadhibiwe vikali na Chama ikiwa ni pamoja na kunyang'anywa uanachama. Chadema kama kinara wa kupambana na rushwa hawezi kutetea rushwa hata kidogo!!
 
Inaonekana ZItto alijiandaa kuharibu uchaguzi, lakini mbinu zake za mchangani hazikufua dafu mbele ya watu wazima wanaokimbia mbio za marathon.Hili liwe fundisho kwa ZT kuwa pesa za mafisadi-magamba haziwezi kupenya ukuta wa CDM sana sana zitaliwa tu kama zilivyoliwa alizotuma kwa M-PESA. ZT elewa CDM imejiandaa kuchukua dolla intelijensia ya hapo usipime, magamba wanakudanganya
 
Ndugu zangu Kabla sijajadili alichokisema kiongozi wangu Bw. Zitto, naomba niweke wazi bila unafiki kwamba uchaguzi wa BAVICHA umekwisha na mwenyekiti amepatikana LAKINI! Kiongozi tuliyempata kwa ninavyomfahamu mimi, kama hatutamsaidia na si kumlaumu au kumkomoa, CHADEMA tutarajie migogoro mikubwa, makundi ya vijana yatapatikana kama wenzetu wa upande wa pili.

Naomba nikiri wazi kuwa Bw. Heche kama binadamu ana mapungufu yake sawa na yeyote hata mimi lakini ndugu huyu kama yumo humu jamvini asipuuze ushauri tunaompa anaweza akafikiri labda tunamuonea wivu la hasha, tafadhali Bwana Heche acha tabia yako kwanza ya kupenda watoto wa kike kashfa nje nje, pili acha kabisa makundi sisi wote ni wako kwa sasa, acha zile tabia zako za kuona wewe ndo unafikiri kwa usahihi na si mwingine.

Acha kuropoka tulia fanya tafiti ongea, afu kuwa flexible kuna mood na makee ya jukwaani na kuna mood tofauti unapokuwa umealikwa mathalani kwenye vyombo vya habari mf. TV, Redio n.k Tafadhali kiongozi wangu usichanganye mambo haya kumbuka umebeba image ya vijana wote wa Taifa hili, haipendezi hata kidogo tunakutazama kwenye TV tunakuwa tunatamani kubadili kwa ajili ya aibu, na Mwisho Bw. Heche acha zile tabia zako za kupenda sifa, umaarufu utakuja tu wenyewe cha msingi zingatia ushauli wetu.

Wanajamvi, kwa hili analosema Zitto kwa mwenye akili timamu hapati shida kuelewa huyu bwana ana kinyongo na sio kwamba anawahitaji TAKUKURU kwa nia safi kutoka moyoni ili waje watende haki tafadhali kiongozi wangu kuna msemo unasema "Failure to prepare is preparing to fail.." ("kushindwa kujiandaa ni kujiandaa kushindwa..") sote tunajua unayo malengo makubwa katika kushika madaraka makubwa katika nchi hii je, hayo ndo maandalizi yako?

NAWASILISHA.
 
Jamani wana CHADEMA kwa nini huyu ngugu Zito asipigiwe kura ya kutokuwa na imani naye then tukaachana naye?
 
Bwana Kabwe, ni vema sasa wewe kama kiongzi (naibu katibu mkuu) ndani ya chama ukampa ushirikiano Bwana Suguta kutekeleza majukumu yake sawasawa kuliko hivi unavofanya kwenda kwa vyombo vya habari kuzungumza uliyoyazungumza. Hakuna point ktk kuanza mitafutano hiyo unayosema, kwangu mm inakuja kama una ajenda yako ya siri zaidi ya kutafuta hicho unachosema ambacho apparently c kwa mstakabali mwema na kuboresha chama
 
ZT acha unafiki wewe!
Kwa mtu mwenye akili za kawaida kabisa hashindwi kuona undumilakuwili uliofichika ktk hoja yako kaka. Uchaguzi umekwisha na sasa wajenge chama. Mambo ya kuita PCCB eti waje kuchunguza ili kuondoa manung'uniko tusiyape nafasi bali mpeni support Heche aunganishe wote walioshindwa na walioshinda ili Chama kisonge mbele mtu wangu! Acha uchonganishi wa hila!

wakifuata ushauri wako ndugu Paulo kutakuwa hakuna tofauti kati ya chadema na ccm kwani sasa hivi ugomvi mkubwa na ccm ni katika hili unalolipendekeza wewe yaani kufukia maovu kwa jina la mshikamano, chadema lazima ionyeshe mfano kwa kuwashugulikia waovu wote na kisheria pia ni makosa kushuudia criminal offence being committed halafu ukaamua kukaa kimya you are basically enabling by ignoring to take appropriate measures. in this case i agree 100% with zito.
 
Dr Slaa amekuwa mtu wa kukurupuka sana na kuonea watu hasa akitumiwa na Mbowe kukata wagombea ambao hawawataki! Hoja ya Zitto inaleta usawa na kuondoa hisia za watu kuonewa na itamuumbua Slaa!
 
Mhe Dkt Zitto anasahau kitu kimoja kwamba utamaduni wa rushwa na ufisadi umejichimbia mizizi katika jamii ya Kibongo kiasi kwamba ni vigumu kila tuhuma ku-qualify kushughulikiwa na TAKUKURU ili kuthibitisha iwapo haki imetendeka.

Kama kweli tuna nia ya kudhoofisha na hatimaye kutokomeza utamaduni huu, kilam kikundi, chama, nk hakina budi kisimame kidekete kuhimiza MAADILI (kv kamati za maadili) baina ya wanakikundi au wanachama wake. Kila ikitokea harufu ya rushwa au ufisadi inazimwa papo hapo badala ya kusubiri TAKUKURU. CCM wenyewe waliwasambaza TAKUKURU nchi nzima hadi vijijini wakati wa kura za maoni lakini ni kesi ngapi zilizopelekwa mahakamani? Mnafikiri rushwa haikutolewa?

Ninaupongeza uongozi wa CHADEMA kwa kuchukua hatua kama waliyochukua - ukisikia harufu ya rushwa izime papo kwa papo - kwa mtindo huu rushwa katika kununua uongozi itatokomea taratibu japo kwa hali ilivyo itachukua kizazi kizima kutokomezwa!!!

Mhe. Dkt Zitto umekuwa ukinichanganya: wakati mwingine huwa unatoka na hoja nzito, wakati mwingine unaibuka na hoja nyepesi sana. Jaribu kujiangalia na kujisahihisha kama kweli unataka kuandika historia nzuri ya wasifu wako wa kisiasa. Niko mbioni kuanzisha ka-consultant firm ka kuwashauri wanasiasa wa Bongo jinsi ya kujenga wasifu wao. Wao ni mteja mtarajiwa.

Nitakupa taarifa pindi kakiishasajiliwa.:A S 103:
 
Jamani wana CHADEMA kwa nini huyu ngugu Zito asipigiwe kura ya kutokuwa na imani naye then tukaachana naye?

Kwani kule Bagamoyo wabunge na wajumbe wengine walipiga kura ya nini? Walimwomba apime uzito kwani kambi anayoiongoza haina imani naye. Kwa vile ni king'ang'izi ndo maana unamuona amekalia madaraka hayo.
 
Binafsi hoja ya Zitto mi naona haina utashi wa kweli wa kuleta "Reconciliation" ikiwa ule mnyukano umeacha majeraha, ila hoja yake hiyo mi naona kama iko kwa ajili ya kukomoana kama si kudhalilishana na pengine Bw. Zitto ni muumini mzuri wa sera ya "Ukimwaga mboga namwaga Ugali" mi nadhani tufike mahali hii tabia ya huyu ni kundi langu na yule si wa kundi langu itafutiwe tiba ya kudumu ni hatari sana na hili lina mlolongo mkubwa wa watu wa kulaumiwa si viongozi wa kitaifa, mikoa, wilaya wala mtaa peke yao.
 
ZT acha unafiki wewe!
Kwa mtu mwenye akili za kawaida kabisa hashindwi kuona undumilakuwili uliofichika ktk hoja yako kaka. Uchaguzi umekwisha na sasa wajenge chama. Mambo ya kuita PCCB eti waje kuchunguza ili kuondoa manung'uniko tusiyape nafasi bali mpeni support Heche aunganishe wote walioshindwa na walioshinda ili Chama kisonge mbele mtu wangu! Acha uchonganishi wa hila!

Haijalishi motives za Zitto ni nini. Ukweli ni kwamba rushwa ni kosa la jinai na siyo ishu ya chama tu. Kama kweli kuna ushahidi wa rushwa kwa nini mtuhumiwa asipelekwe mahakamani? Asipo pelekwa mahakamani tuna fuga mafisadi wa baadae kwa maana kama kweli ni mla na mtoa rushwa huko mbeleni hatosita kutumia njia hiyo tena akijua mara ya mwisho hakuna kilicho fanywa zidi yake. Fikiri nje ya mistari ya chama na weka maslahi ya taifa kwamza.
 
Haijalishi motives za Zitto ni nini. Ukweli ni kwamba rushwa ni kosa la jinai na siyo ishu ya chama tu. Kama kweli kuna ushahidi wa rushwa kwa nini mtuhumiwa asipelekwe mahakamani? Asipo pelekwa mahakamani tuna fuga mafisadi wa baadae kwa maana kama kweli ni mla na mtoa rushwa huko mbeleni hatosita kutumia njia hiyo tena akijua mara ya mwisho hakuna kilicho fanywa zidi yake. Fikiri nje ya mistari ya chama na weka maslahi ya taifa kwamza.

Rushwa ni kosa la jinai toka lini?
 
Back
Top Bottom