Tuhuma za rushwa BAVICHA zipelekwe TAKUKURU - Zitto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma za rushwa BAVICHA zipelekwe TAKUKURU - Zitto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na Tumaini Makene

  NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Kabwe Zitto ametoa pongezi kwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vijana (BAVICHA), huku akisema kuwa atamwandikia barua katibu mkuu wake, kushauri tuhuma za kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa juzi, zipelekwe mbele kwa hatua zaidi.

  Akizungumza na Majira jana, Bw. Zitto alisema kuwa leo atawasilisha barua hiyo kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, kumwomba tuhuma za rushwa zifikishwe katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ili zifanyiwe uchunguzi, kisha hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika.


  "Nafikiri nitaiwasilisha kesho hiyo barua, nitamwomba katibu mkuu hizi tuhuma zifikishwe PCCB, nafikiri hiyo itakuwa ni hatua bora zaidi, PCCB wachunguze watakaobainika na makosa wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wote wanaojihusisha na vitendo vya namna hiyo ndani ya chama.


  "Nitatumia nafasi yangu ya Naibu Katibu Mkuu. Kwa sababu tusipofanya hivyo itaweza kujenga hisia za kuwa walioondolewa katika uchaguzi huo kwa tuhuma za rushwa wameonewa. Italeta hisia za upendeleo...kwa sababu mwenye haki ya ku-determine rushwa ni mahakama hivyo ni bora wachukuliwe hatua zaidi," alisema Bw. Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.


  Akizungumzia ushindi wa Mwenyekiti wa BAVICHA, Bw. John Heche, alisema kuwa changamoto kubwa aliyonayo ni kuwaunganisha vijana wote na kuwa kiongozi wao, wakiwemo wale waliokuwa washindani wake na watu waliokuwa nyuma yao wakiwasapoti.


  "Nampongeza sana Heche, kwa ushindi wake alioupata. Sasa hivi ni wakati wa kukijenga chama, uchaguzi umeisha si wakati wa kulalama tena...vijana wanamtegemea atakuwa mwenyekiti wao, mimi nafikiri moja ya changamoto zake kubwa ni pamoja na kuwaunganisha vijana, wote hata walioenguliwa," alisema Bw. Zitto.


  Juzi akizungumza na Majira juu ya uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa alisema kuwa vitendo vyote vilivyo kinyume na maadili ya kampeni kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha katiba ya chama hicho, pamoja na waliohusika, vitajadiliwa katika ngazi ya Kamati Kuu kwa maamuzi zaidi.


  Alisema kuwa baadhi ya wagombea, hasa walioenguliwa, walibainika kwenda kinyume na maadili ya chama hicho, hasa katika kupiga vita ufisadi wa aina yoyote kama vile kufanya hila katika uchaguzi, kujenga makundi yenye kuhatarisha chama na kutaka kuvuruga uchaguzi.
   
 2. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Big up Zitto!
   
 3. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ZT acha unafiki wewe!
  Kwa mtu mwenye akili za kawaida kabisa hashindwi kuona undumilakuwili uliofichika ktk hoja yako kaka. Uchaguzi umekwisha na sasa wajenge chama. Mambo ya kuita PCCB eti waje kuchunguza ili kuondoa manung'uniko tusiyape nafasi bali mpeni support Heche aunganishe wote walioshindwa na walioshinda ili Chama kisonge mbele mtu wangu! Acha uchonganishi wa hila!
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Yah ni mawazo mazuri mkuu zito ili kuondoa huu uozo kama upo!
   
 5. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Panapokuwa na Uchaguzi, minyukano haikosekani. Lakini kuiendeleza minyukano baada ya uchaguzi ni kutaka kuvuruga Chama tu. Sifikiri kama Zitto anayosema yanalengo la kushitaki waliotoa rushwa au kuwasafisha watuhumiwa.

  Naamini atakuwa upande mmoja wapo hapo juu. Yeye kama kiongozi alitakiwa kuwashauri wagombea walioshindwa kuunganisaha nguvu kujenga chama na wala siyo kuleta utengano wa kutafuta nani katoa rushwa au vipi. Nakuomba mh. Zitto uridhike na matokeo na hao wanaonung'unika washawishi wakumbali matokeo ingawa kila iliyeingia kwenye kinyang'iro aliamini atashinda, lakini anatakiwa mmoja tu.

  Naomba waeleshwe hao vijana hayo na kutumikia chama siyo lazima uwe mwenyekiti unless otherwise awe anatafuta kazi ya umwenyekiti na wala siyo cheo cha umwenyekiti.
   
 6. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ili kukomesha hiyo Tabia na iwapo ushahidi unajitosheleza Chama moja kwa moja kupitia wanasheria wake kiwafikishe Mahakamani ila hilo lakupitia Takukuru siliafiki kwanza hii Taasisi imeoza na haiaminiki pia hawana Historia yakushinda Kesi yoyote ya Rushwa ya Mwakalebela juzi tu hapa wamechemsha sasa wa nini hawa.
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mvutana wa makundi mawili ndani ya chama ndio huu, kundi la akina mbowe linadaiwa kutumia rafu kumpitisha mtu wao bache ili hali kundi la akina zitto mtu wao akipigwa chini kimizengwe.

  Zitto na kundi lake hawajakubali matokeo mioyoni na ndio maana anataka baraka ili liwasilishwe takukuru, lakini katibu mkuu wake amesha sema wazi matatizo yote ya uchaguzi yatajadiliwa na kamati kuu.
  kazi kweli kweli
   
 8. n

  ngurati JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Acha unafiki zitto, tunaomba na wewe uangalie kwenye simu yako tarehe 3 mwezi may 2011, hii kumbukumbu namba ya MPESA uliyomtumia mmoja wa wagombea aliyeenguliwa ilikuwa ni ya nini??? Kumb namba ni hii hapa - B66FE724.

  Ukiendelea nitaweka mpaka kiasi cha pesa ulichotuma. Najua ulikuwa humuungi mkono heche tangu uchaguzi wa mwaka 2009 ulioharibika. Tafadhali sana iache BAVICHA hii ya kwanza ya kitaifa ifanye kazi.
   
 9. n

  ngurati JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakuna mtu aneyeitwa bache, nahisi wewe ni mwana ccm na unafananisha heche na hussein bashe wa uvccm.
   
 10. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kujadili hoja ya Zitto, tujiulize. Mwaka jana wakati Fedrick Mwakalebela anatafuta kura za maoni za kugombea Ubunge wa Iringa Mjini na alipopatwa na tuhuma za kutoa rushwa katika minyukano ya kusaka kura za maoni, Je ni CCM iliyompeleka TAKUKURU au ni TAKUKURU ndiyo iliyomdaka?

  TAKUKURU kama taasisi ya kupambana na rushwa imesoma na kusikia kupita kwenye vyombo vya habari juu ya tuhuma za rushwa dhidi ya wagombea wa CDM. Wao ndio wanapaswa wawakamate wote wanaotuhumiwa na kuanza kufanyia kazi tuhuama dhidi yao. Au watuhumiwa wenyewe wajisalimishe TAKUKURU ili wakafanyiwe uchunguzi hatimae wasafishwe kama wanataka.

  Si kazi ya CDM kufanya kazi ya TAKUKURU unless tukubaliane kwamba TAKUKURU yetu ni SIKIO la kufa. Haisomi magazeti wala haisikilizi Radio na TV.

  Tuendelee kujadiliana!

  By TUMBIRI mtoto wa NYANI.
   
 11. b

  babap Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa kuwa ZITO anayo hiden agenda ya kutaka kuleta malumbano ndani ya chama. Haihitaji mtu kufika form four kuliona hili.
   
 12. G

  Galula Jr Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni vizuri lakini je, hao PCCB wanaaminika kwa lipi kaka Zitto? Tusije mpa mbu kazi ya kutibu maleria kaka yangu
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  I dont understand kwa nini Zitto anaongea as if hakuwepo kwenye uchaguzi. Huyu mtoto amekuwa na kasumba ya kuongea na vyombo vya habari mambo ambayo kimsingi ni Internal communications! Kama anataka kumuandikia barua kiongozi ndani ya chama chake kwa nini akasemee majira? Zitto is bad news kwa CHADEMA through & through!
   
 14. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sounds good, mature and credits for advocacy for the rule of law. But bearing in mind this TAKUKURU that I know,the level of democracy in this country and the credibility of our judicial systems; and amid the political mitafutano going on between the ruling party (practical the owner of PCCB and the judiciary) and our dear CDM.....BIG NO!! BIG NO!!!
  Kesi ya mbuzi unampelekea simba?
   
 15. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Ni hoja nzuri, lakini ukizingatia na historia ya PCCB katika miaka ya karibuni, sidhani kama hatua muafaka zitachukuliwa...
   
 16. P

  Paul S.S Verified User

  #16
  May 31, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Msiwe na wasi wasi kuhusu TAKUKURU, ikihudumia kesi za ccm inaangalia maslahi ya aliyowateua, lakini kwa cdm hawana maslahi yoyote hivyo watatenda haki
   
 17. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Kupeleka tuhuma TAKUKURU ni kupeleka kwenye Chama Cha Magamba....Takukuru ni sehemu ya vitengo vya CCM. Zitto fikiri kwa usahihi...usirukie umaarufu ukasahau kuwa sensible. Kama kulikuwa na rushwa...CDM wachunguzane wachukuliane hatua...TUKUKURU wakitaka waingie kivyao sio kuwapelekea....kijichama kichanga hiki hata GAMBA hakina....kitakula mweleka hicho...oooh!
   
 18. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Zitto acha unafiki wewe ulisusia uchaguzi sasa baada ya uchaguzi kinakuhusu nini kwa nini usiseme walioandaa uchaguzi watayashughulikia, katibu mkuu ameshasema matatizo yote yatashughulikiwa na kamati kuu sasa wewe kama hukuridhika tangulia mahakamani au Takukuru mwenyewe au wape hela tena za mahakama kama ulivyowapa za kampeni.

  Mambo ya chama kwa nini unayapeleka kwenye magazeti kwanini hiyo barua usiipeleke kwenye chama hadi utangaze magazetini, Zitto my friend tumekuvumilia sana na siasa zako za makundi karibu tutafika mwisho, uchaguzi wa Bavicha uliopita ni wewe ulisababisha kuvunjika leo wenzako wamefanikisha wakati wewe umesusa unataka tena kutuletea makundi jiangalie unakokwenda.
   
 19. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Zitto kama analeta uozo wa kimagamba nadhani hataweza, intelijensia ya CDM kwa sasa ni zaidi ya ile ya magamba, ZT yuko kwenye darubini tunamcheck vizuri, akithubutu tuuuuu atashughulikiwa kama alivyoshughulikiwa yule jamaa wa FIFA.CDM ni kama FIFA ya SEpp Blater.
   
 20. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CDM msiwe wanafiki mwaka jana mlikuwa mnashupalia CCM walipoalila TAKUKURU katika uchaguzi wao wa ndani. Kama mpo safi kwa nini mwaogopa kuialika TAKUKURU au kwa sababu rushwa ilitolewa kama njugu kwa uwezeshaji wa mwenyekiti wa Chama HIVYO mwaona so. Kuweni na UJASIRI pelekeni maombi kwa TAKUKURU ili ukweli ujulikane, ZK mpeni pongezi kwa wazo zuri!
   
Loading...