Tuhuma za Polisi kubambikiza kesi, kunyanyasa, kutesa na kuua watu, zinahitaji hatua madhubuti

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Kumekuwa na tuhuma nyingi zikielekezwa Jeshi la Polisi kuhusu kubambikiza kesi, kunyanyasa raia ambao ndio wanapaswa kuwalinda, utesaji wa watuhumiwa hadi wengine kuuwawa, kama ilivyotokea kwa mdogo wa mh. Heche, aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CHADEMA. Huyu alikamatwa na polisi, na akiwa kituoni, polisi mmoja alichomoa singe kutoka bunduki yake na kumchoma nayo kijana huyo kifuani hadi alipokufa.

Polisi wetu pia wanakabiliwa na tuhuma za kutesa watu.

Hivi niandikapo, kulikuwa na kipindi kinaendelea Redio Tumaini, (Alhamisi saa 11:40 jioni) ambapo imetolewa taarifa kwamba huko Handeni, Tanga, Polisi wameripotiwa kuvamia sehemu za starehe wakiwa na silaha, na kuchukua mabinti wawatakao kwa nguvu. Binti anayegoma, anaswekwa ndani na kuteswa.

Imeripotiwa pia kwamba Polisi wamekuwa na kawaida ya kuwashikashika na kuwapapasa mabinti kwa nguvu.
Imeripotiwa pia kwamba Mkuu wa Wilaya ya Handeni aliitisha kikao na kukawa na upigaji kura kuwatambua polisi wanaotuhumiwa kufanya vitendo hivyo.

Maelezo ya kipindi hicho cha Redio Tumaini, yanaendana na tuhuma nyingi ambazo hutolewa mara kwa mara na watu mbalimbali. Kwa kweli Rais Samia mwenyewe mara kadhaa ameongelea vitendo vya polisi, pamoja na Ubambikizaji kesi.

Licha ya watu mbalimbali kukutana na ubabe huu wa Polisi, viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani wamekuwa ndio wahanga wakubwa wa ukatili hui. Pengine kwa sababu serikali za ccm hutumia kigezo cha kutesa wapinzani, kama moja ya vigezo vya kupandisha vyeo polisi.

Tatizo moja kubwa ni uelewa mdogo wa haki na sheria zinazomlinda mtuhumiwa, pale anapokabiliana na vyombo vya dola. Hilo linahitajika kufanyiwa kazi na vyombo mbalimbali, mfano vyama vya kiraia na taasisi mbalimbali.

Haitoshi kwa viongozi wetu, tukianzia na Amiri Jeshi Mkuu, kuwa nao ni walalamikaji tu.

Tunahitaji kwanza iundwe tume ya Jaji anayeheshimika, kuchunguza kwa kina tuhuma hizi. Kukutana na wahanga wa ukatili wa Polisi, na kufanya uchunguzi wa kina. Wakutane na makundi mbalimbali kama wanawake, watoto, vijana, viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani, nk. Ripoti iwekwe wazi na Serikali ichukue hatua stahiki

PIA, SOMA:
- Handeni, Tanga: Polisi wadaiwa kushika nyeti za wanawake kwa nguvu bila ridhaa
 
😁😁😁
AUYZ3t.jpg
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwenye thread kama hii yenye facts hautakuta comments nyingi maana wanaopenda kufuata mkumbo na kuunga mkono ujinga hua hawachambui issues,wanakujaga tu ku support nonsense
 
Back
Top Bottom