TUHUMA za nyumba ya Gavana wa BOT na majibu yake

Che Guevara

JF-Expert Member
May 22, 2009
1,236
346
16badyu.jpg

xqhop2.jpg

BoT yatumia Sh1bilioni kukarabati nyumba ya Gavana Ndulu

Na James Magai

WAKATI tuhuma za matumizi mabaya ya Sh1.4 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za Tanesco zikiendelea kuchunguzwa, Benki Kuu (BoT) inadaiwa kutumia Sh1 bilioni kukarabati nyumba moja ya gavana wake, Profesa Benno Ndulu, Mwananchi imeelezwa.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa taasisi hiyo ya fedha imetumia kiasi hicho kukarabati nyumba ya gavana katika mradi wa ukarabati wa nyumba za vigogo wake wanne ambao ni gavana na manaibu wake watatu.

Kwa mujibu wa habari hizo, nyumba iliyokarabatiwa kwa fedha hizo iko Oysterbay eneo la Morogoro Stores, jirani na nyumbani kwa katibu mkuu wa mstaafu wa CCM, Philip Mang'ula jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini pia kwamba kigogo anayestahili kuishi kwenye nyumba hiyo (gavana), tayari amehamia na kuishi humo tangu Desemba Mosi mwaka huu.

Hata hivyo, habari zaidi za kiuchunguzi zinabainisha kuwa ukarabati wa nyumba hiyo umetumia gharama mara mbili zaidi ya bei ya kununulia nyumba hiyo. Nyumba hiyo ilinunuliwa kwa dola 400,000 za Kimarekani ambazo ni sawa na takriban Sh500 milioni.

Mbali na nyumba hiyo, nyumba nyingine zinazodaiwa kutafuna fedha za walipa kodi katika ukarabati wake ni ya naibu gavana wa kwanza, Juma Reli iliyo Masaki, Mtaa wa Chole. Nyumba hiyo ilikuwa ikitumiwa na gavana wa zamani, Dk Daud Balali.

Habari zaidi zinadai kuwa Reli alihamia kwenye nyumba hiyo baada ya Gavana Ndulu kuikataa kwa madai kuwa haina bwawa la kuogelea (swimming-pool).

Nyumba nyingine iliyo kwenye tuhuma hizo za kashfa ya ufujaji mamilioni ya walipa kodi ni ile inayotumiwa na naibu gavana wa pili (Bukuku), iliyo Oysterbay pamoja na ya naibu gavana wa tatu (Makila) iliyo Masaki.

Afisa uhusiano wa BoT, Emmanuel Mwero, alipotafutwa na Mwananchi kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo jana, hakutaka kujibu moja kwa moja na badala yake aliweka urasimu wa kutaka maswali yaandikwe kwenye karatasi iliyo na nembo ya gazeti hili ndpo aandae majibu.

"Ahh, kwa hilo, wewe lete maswali yako kwenye 'headed paper (barua yenye nembo)' ya Mwananchi hata leo (jana) au kesho (Leo) utajibiwa kiofisi," alisema Mwero.

BoT ni taasisi ya pili kutuhumiwa kuhusika na ufisadi huo katika mradi wa ukarabati wa nyumba za vigogo wake ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Tayari Tanesco imekumbwa na tuhuma kama hizo ambazo bado hazijapoa. Wizara ya Nishati na Madini imeeleza kuwa inaendelea kuzifanyia kazi.

Hata hivyo, tuhuma za ufisadi ndani ya BoT zinadaiwa kuwa kubwa na za kutisha ikilinganishwa na kiwango cha pesa kinachodaiwa kutumika kwa ukarabati kwa nyumba za Tanesco.

Wakati Tanesco inatuhumiwa kutumia Sh.1.4bilioni kwa ajili ya ukarabati wa nyumba saba za vigogo wake, taarifa za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zilizolifikia Mwananchi zinaeleza kuwa BOT imetumia zaidi ya Sh1bilioni kukarabati nyumba moja, kati ya nyumba nne zilizokuwa katika mradi huo wa ukarabati.

Kiasi hicho cha fedha unaweza kununua nyumba mbili mpya nje ya maeneo ya Jiji la London, Uingereza. Kwa sasa bei ya nyumba katika maeneo ya Cardiff ni Sh450milioni kwa nyumba moja.

Chanzo: Mwananchi 12/22/2009
 
Ukishangaa ya Dr. Rashid utaona ya Prof. Ndulu.

Tulisema huyu Ndulu ni "badder than the replacement killer" mwenyewe Balali, tukaambiwa aaaa, eeee.

Na bado, kidau kinapandishwa polepole, mpaka ukarabati wa nyumba utafika mara kumi ya bei ya nyumba.

After all uchaguzi unakuja na wao ndio wanakalia minoti, utawaambia nini? Rais mwenyewe nani, Kikwete? Sahau chochote muhimu kufanyika, watu wanapeta tu.
 
Huu ni uzushi mtupu na hauna ukweli wowote. Angalia ni gazeti gani limeandika. Naona hapa jamvini siku hizi wala hatufanyi utafiti. Tunabandua na kubandika. Hizi ni tuhuma tuu ambazo hazina ukweli wowote. Subirini bot wajibu pamoja na kutoa gharama halisi. Kwahili natetea bot na utawala wake. Tunaye gavana makini sana pale na uzuri record keeping zipo. Tusubiri wajibu ndiyo tulijadili hili. Haya mambo ya kucopy na kupaste kutoka magazeti ya rostam yanaua na kushusha hadhi ya forum hii.
 
Sometime katika salary slip yangu nikiona PAYE huwa napata hasira sana,kwani najua kiwango ninachokatwa kuna jamaa wanakifuja vilivyo...Ooh,in bongo everything z possible...Vigogo wapo busy na vi_epa vyao...After all ni shamba la bibi!
 
Kubabake walahi! Wachizi wanakula nchi hawa!

Wanaitafuna kwa kwenda mbele,halafu hapo ni kama good gesture tu,bado itabidi aanguke masaini mengine ya pesa za kampeni nk. Huo ni "ukarabati" wa nyumba peke yake....Sasa ki "note" kikitokea cha dili la ki "epa" atakataa?Balali sijui ni nani alimwaribia,lakini hawa hawakosi mbinu,ni kama mbwa mwizi,hata umpige vipi atarudi na kuiba tu,ile pleasure inazidi maumivu....Kama kweli wizi ulitokea,kuna wanaoamini kwamba hautatokea tena?Nadhani wanaoamini hivyo ni wale wanaoamini kuwa ccm itashindwa kwenye uchaguzi....Kwasababu haiwezi kushindwa kuendelea "kuiba" kama haitashindwa uchaguzi,hakuna sababu ya wao kuacha kuiba....Very sad indeed.
 
Huu ni uzushi mtupu na hauna ukweli wowote. Angalia ni gazeti gani limeandika. Naona hapa jamvini siku hizi wala hatufanyi utafiti. Tunabandua na kubandika. Hizi ni tuhuma tuu ambazo hazina ukweli wowote. Subirini bot wajibu pamoja na kutoa gharama halisi. Kwahili natetea bot na utawala wake. Tunaye gavana makini sana pale na uzuri record keeping zipo. Tusubiri wajibu ndiyo tulijadili hili. Haya mambo ya kucopy na kupaste kutoka magazeti ya rostam yanaua na kushusha hadhi ya forum hii.

Kumbe kuna magazeti huyapendi kwasababu yamesema uwapendao? lol

Swala si nani kasema issue ni kwamba wahusika wanawaibia watanzania wote!

Ndulu anastahili kujiuzulu kwa ujinga huu, kama itagundulika kweli anatafuna kihivyo
 
Hee mbona mnamlaumu Gavana, yeye ndiye mwenye jukumu la kutoa ruhusa hizo hela zitumike au ni Hazina?
 
Hee mbona mnamlaumu Gavana, yeye ndiye mwenye jukumu la kutoa ruhusa hizo hela zitumike au ni Hazina?

What? yaani hujui kwamba BoT ni independent institution na final executive power ziko kwa gavana? do your homework!

Mwizi tu huyu hana tofauti na wale Profesa Uchwara!
 
Huu ni uzushi mtupu na hauna ukweli wowote. Angalia ni gazeti gani limeandika. Naona hapa jamvini siku hizi wala hatufanyi utafiti. Tunabandua na kubandika. Hizi ni tuhuma tuu ambazo hazina ukweli wowote. Subirini bot wajibu pamoja na kutoa gharama halisi. Kwahili natetea bot na utawala wake. Tunaye gavana makini sana pale na uzuri record keeping zipo. Tusubiri wajibu ndiyo tulijadili hili. Haya mambo ya kucopy na kupaste kutoka magazeti ya rostam yanaua na kushusha hadhi ya forum hii.

Gavana makini si ndiye huyu aliyekuwa naibu gavana wakati Balali akicheza michezo yote ya EPA, umakini ulikuwa wapi sasa siku zote hizo?
 
hivi ma profesa waTZ wana matatizo gani???
Kenya maprofesa wawili moja waziri wa elimu na mwingine katibu mkuu wamekula pesa za watoto wa shule msingi msaada kutoka DFID shame on so called academicians!
 
Tuliwahi kuambiwa hapa kwamba Ndullu ni kichwa sana sijui kabla ya kuja BoT alikuwa WB..blah blah blah! kumbe naye ni FISADI TU! Kukarabati nyumba moja shilingi bilioni moja! Zingetoka nyumba ngapi hapo zenye thamani ya milioni 50 au kununua madawati ya shule za msingi. Bongo kweli IMEOZA! Tusubiri Kikwete kama atanena lolote kuhusu uporaji huu wa mchana kweupe.
 
Habari zaidi zinadai kuwa Reli alihamia kwenye nyumba hiyo baada ya Gavana Ndulu kuikataa kwa madai kuwa haina bwawa la kuogelea (swimming-pool).

Ninachofurahia kwa viongozi wetu ni kupenda kuishi kwa viwango vya juu katika nchi iliyojaa umaskini! Shame on you!
 
acheni uzushi, Gavana anastahili kuishi kwenye nyumba yenye hadhi. Swimming pool ni muhimu. Hadhi ya Gavana mkuu na ya mtumishi wa kawaida wa serikali kuna tofauti kubwa mno. Acheni kumponda Prof. Ndulu, he is a genius...
 
Ukishangaa ya Dr. Rashid utaona ya Prof. Ndulu.

Tulisema huyu Ndulu ni "badder than the replacement killer" mwenyewe Balali, tukaambiwa aaaa, eeee.

Na bado, kidau kinapandishwa polepole, mpaka ukarabati wa nyumba utafika mara kumi ya bei ya nyumba.

After all uchaguzi unakuja na wao ndio wanakalia minoti, utawaambia nini? Rais mwenyewe nani, Kikwete? Sahau chochote muhimu kufanyika, watu wanapeta tu.

Ni pamoja na wewe watu wanapiga kelele Rashid we!!!!!!!!!!!!!! haya Ndulu nyumba moja ya Billion 1 unanunua mtaa mzima Uingereza nyumba zote mtaa moja wa uingereza
 
acheni uzushi, Gavana anastahili kuishi kwenye nyumba yenye hadhi. Swimming pool ni muhimu. Hadhi ya Gavana mkuu na ya mtumishi wa kawaida wa serikali kuna tofauti kubwa mno. Acheni kumponda Prof. Ndulu, he is a genius...

Wewe ni mjinga wa mwisho. Billioni moja ingelijenga hospitali ngapi Tanzania??? Ingelijenga shule ngapi Tanzania??? Kwani hawezi kujengewa nyumba ya hadhi ya gharama nafuuu hadi Bilioni 1?

Unamuona genius peke yako wewe hujui kwamba kuwa na akili nyingi ukakosa hekima ni kama chakula kizuri kilichokosa chumvi utakula wewe!!!!!
 
Back
Top Bottom