Tuhuma za mh. Lissu dhidi ya majaji zifanyiwe uchunguzi wa kina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma za mh. Lissu dhidi ya majaji zifanyiwe uchunguzi wa kina

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teroburu, Jul 16, 2012.

 1. T

  Teroburu Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huku akijiamini na kuamini kuwa aliyokuwa akiyasema ni kweli na ukweli tupu, Mh. Tundu Lissu alitoa tuhuma nzito dhidi ya Mh. RAIS, WAHESHIMIWA MAJAJI, na MAAFISA WA SERIKALI.

  Nimefanikiwa kusoma taarifa ya Mh. Lissu (MB): “MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA, MH. TUNDU A.M. LISSU (MB.) KUHUSU MPANGO NA MI YA FEDHA YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA MWAKA 2012/2013.”

  Katika ukurasa wa 9, Mh. Lissu anasema:

  “Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, sasa watu wanateuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekeza na Tume Tume ya Utumishi wa Mahakama na- kwa sababu hiyo- hawajafanyiwa vetting yoyote na mamlaka hiyo ya kikatiba juu ya uwezo na ukjuzi wao kama wanafaa kwa kila hali kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu. Inaelekea watu hao- wengi wao wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma- wanapewa ZAWADI YA UJAJI ili kuwawezesha kupata mafao ya Majaji wastaafu ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni.”

  Tuhuma za Mh. Lissu zinaibua maswali kadhaa kuhusu mustakabali wa taifa letu:

  1. Ni kweli MAJAJI WETU wanateuliwa na Mh. RAIS bila kupata mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama?
  2. Ujaji nchini Tanzania ni zawadi?
  3. Je Mbunge anajiridhisha kwanza na usahihi wa taarifa anazopokea kabla ya kuzitamka BUNGENI KAMA UKWELI?
  4. Hatua gani zichukuliwe dhidi ya Mbunge anayetumia uhuru wa mbunge kuongea bungeni kwa kutoa TUHUMA ZA UONGO NA ZINAZOPOTOSHA dhidi ya Mihimili mingine ya Dola ?
  5. JE Chama Rasmi cha Upinzani Bungeni kilipata nafasi ya kuijadili hotuba ya Mh. Lissu na kuibariki isomwe Bungeni PAMOJA NA TUHUMA? Au ILIKUWA ni hotuba Binafsi ya Mh. Lissu ambayo haikupitia katika mfumo wa kimajadiliano na kimaamuzi (shadow cabinet) ndani ya kambi ya upinzani?
  6. Je wanachama binafsi ndani vya vyama ni bora kuliko uamuzi wa chama?
  7. Je Chama Rasmi cha Upinzani kina uwezo wa kuwadhibiti baadhi ya wanachama wao ambao ni « el-maarufu »?

  Kwa bahati mbaya, watu wengi wanaamini kuwa Mh. Lissu ni Mwanasheria bora kuliko wanasheria wote katika Jamhuri ya Muungano. WAtanxzania wengi wanaamini chochote kinachosemwa na viongozi kama Mh. Lissu ni sahihi na kweli tupu.

  Kwa bahati mbaya, hata Magazeti yalimnukuu huyu Mbunge bila kunukuu yaliyosemwa na wabunge wengine kuhusu tuhuma alizotoa Mh. Lissu.

  Je ni kitu gani kimeyazuia Magazeti kufanya uchunguzi wa kina na kubaini ukwel ;i kuhusu uteuzi wa Majaji ? Je uwezo wa magazeti na waandishi wa habari kufanya uchunguzi wao wa kina umepotea hapa Tanzania ?

  MHESHIMIWA SPIKA. Tuhuma dhidi ya Rais, Mahakama na maafisa kadhaa wa Umma zilitolewa ndani ya Bunge lako. Mh. Lissu anajua kuwa kama angetoa hizo tuhuma nje ya Bunge walioguswa na tuhuma hizo wangefuata utaratibu wa Kisheria kurudisha heshima yao mbele ya jamii.

  Ili kulinda utawala wa sheria na heshima ya Bunge, ili kulinda heshima ya Mahakama na pia heshima ya Rais na ili kulinda heshima ya watumishi wa umma waliotuhumiwa bila ya wao kujitetea: ninakuomba Mh. Spika uamuru uchunguzi wa kina ufanywe ili kujua ukweli wa mambo.

  KWA KUWA MH. ALITOA TUHUM ZAKE MBELE Y WATU WOTE WALIOKUWA WAKIANGALIA RUNINGA, NINAOMBA KUWA WAKATI WA UCHUNGUZI HUO SISI WANANCHI TURUHUSIWE KUHUDHURIA ILI HUO USHAHIDI WA MH. LISSU TUUONE BILA KUSUBIRI KUAMBIWA.
   
 2. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  chadema ni chama makini huwa hawakurupuki. hotuba b4 kuwa presented bungeni huwa inapitiwa na wahusika.
  haya mambo yapo na hdta waziri alikiri kwa kusema cdm wanaweza wakawa na point ila njia waliyotumia ni ya ukali zaidi.
   
 3. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  ukweli ni kuwa kajamaa ni kepesi kuongea huku kakiminya macho na kuonekana kako right, huyu jamaa kachemsha sana kwani anatumia mno habari za kuambiwa na kusikia bila kuchanganya na zake, ni kana kwamba ana ugovi na wanasheria wenzie, na kwa maantiki hiyo ni juu ya watanzania kutafakari juu ya yanayosemwa na wapinzani haswa wa nchi maskini na wanasiasa lofa wanaohangaika kuwakwamua watu wao kwa kuwagombanisha na si kuwaweka pamoja.
   
 4. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  mkuu naamini yapo ya msingi mengine tunaweza kuendelea kuongea lakini hili silo!!!! cdm bado.
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nyie endeleeni kujichuuza! Jadilini mnatekeleza vipi ahadi zenu, hivi unadhani kuna msomi ambaye hahoji kwa mfano weledi wa yule jaji (lwakibarila) aliyehuku kesi ya lema, aliyeshindwa kuoanisha hukumu na kanuni za adhabu kwa hukumu yake, macho tunayo, hatutatumia makengeza ya kova. TUNDU LISU YUKO SAHIHI.
   
 6. eumb

  eumb Senior Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania tukubali nchi yetu itabadilika kwa kupata watu kama Lissu watakao kuwa tayari kusimama na kusema ukweli kwa kujitoa mhanga ili maovu yafichuliwe. Jaribu kufikiri Mhe Tundu Lissu pia ni wakili anayetegemea taaluma yake hiyo kupata income kwa ajili ya maisha yake na familia. Kumbuka katika kazi zake za uwakili atakumbana na Majaji hao hao watakao amua kesi atakazo zitetea, je hata athirika na maamuzi? Mimi naamini mpaka kufikia kujiamini kusoma taarifa yenye kashfa kubwa kama hiyo ndani ya bunge huku akitazamwa na Watz kwa maelefu na vyombo vya habari ni lazima ana uhakika na kile alichokisema. Nchi yetu inazidi kuwa maskini kwa sababu ya kuogopana na kushindwa kusimamia haki na taratibu tulizoweka. Nitatoa mifano kadhaa;

  Mimi naishi kigamboni, kila siku natumia usafiri wa vivuko kwenda na kurudi kwa kulipia, ambapo naajua fedha hizo ndio zinazofanikisha kuendesha vivuko hivyo. Sasa utashangaa wapo wanaoitwa waheshimiwa, wanafuatwa nyumbani kwa gari za serikali, dereva wa serikali, mafuta ya serikali na wanalipwa mshahara mzuri pamoja na marupurupu kibao vyote hivo kwa kodi zetu, halafu hawalipii gharama za kuvuka wala kupanga foleni kisa ni watumishi wa serikali na wanavyeo vikubwa. Je ni haki watu hao kulipiwa na walalahoi, wasio na ajira, wanafunzi wa vyuo na wengine kuvushwa? Huo ndio uwoga wa kuambiana ukweli unapodhihirika!

  Dr Hosea alilidanganya bunge na kila kitu kikawa wazi na bunge hilo hilo likaweka maazimio kuwa aadhibiwe kwa kudangaya kuhusu Richmond, sasa jiulize kinasubiriwa nini mpaka leo!!

  Mhe Wazi Mkuu Pinda alikashfiwa na kudhalilishwa na Godbless Lema kuwa kadanganya bungeni, fikiria kwa cheo chake ilipaswa uthibitisho uwekwe hadharani ilikumsafisha au la, aombe radhi kwa kulidanganya bunge. Je sasa nani aliye tayari kumbana afanye hivyo?

  Kumbuka Waziri alitangaza kwa mbwembwe nyingi kuwa raia wa nje wasio na vibali wajisalimishwe au watakamatwa, nini kilifuata mpaka leo?

  Sheni wa Game Frontiers anasaini mkataba na kampuni ya kuchimba madini ya uranium ndani ya kitalu cha uwindaji alichopewa kwa mkataba wa kuwinda na serikali, lakini anasaini mkataba kinyume na sheria eti kwasababu ni kada na mfadhili wa CCM kwa hiyo anaweza kufanya lolote!!

  Yapo mengi ndugu, tusipopata watu kama Lissu hatutasogea daima!
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,773
  Likes Received: 6,105
  Trophy Points: 280
  ...

  Katika ukurasa wa 9, Mh. Lissu anasema:

  "Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, sasa watu wanateuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekeza na Tume Tume ya Utumishi wa Mahakama na- kwa sababu hiyo- hawajafanyiwa vetting yoyote na mamlaka hiyo ya kikatiba juu ya uwezo na ukjuzi wao kama wanafaa kwa kila hali kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu. Inaelekea watu hao- wengi wao wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma- wanapewa ZAWADI YA UJAJI ili kuwawezesha kupata mafao ya Majaji wastaafu ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni."

  Tuhuma za Mh. Lissu zinaibua maswali kadhaa kuhusu mustakabali wa taifa letu:

  1. Ni kweli MAJAJI WETU wanateuliwa na Mh. RAIS bila kupata mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama?

  Nukuu kutoka hotuba ya Mh. Lissu hii hapa:

  " ... Kuteua Majaji wengi wenye uwezo, ujuzi na wanaofaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu ni jambo jingine kabisa.
  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa na dalili zinazoanza kuonekana wazi kwamba baadhi ya Majaji walioteuliwa na Rais hawana uwezo, ujuzi na/au hawakufaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji ya Mahakama Kuu ..."; Ref. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/291680-tundu-lissu-afunguka-bungeni-2.html#post4230921


  Hebu linganisha nukuu hiyo hapo juu hasa mistari ya kijani ulinganishe na "nukuu" na tafsiri yako. Uongo, unafiki, na uzushi hautakusaidia wewe wala chama chako unachojaribu kukitetea.

  1. Ujaji nchini Tanzania ni zawadi?

  Hakuna mahali Lissu aliposema Ujaji ni zawadi. Anacholalamikia ni ukiukwaji wa taratibu za uteuzi na tuhuma na kueteua wasio na uwezo kwenye nafasi hiyo nyeti kwa taifa.
  1. Je Mbunge anajiridhisha kwanza na usahihi wa taarifa anazopokea kabla ya kuzitamka BUNGENI KAMA UKWELI?

  Kisicho sahihi alichokisema Mh. Lissu ni kipi? Kama huelewi ni bora kukaa kimya.
  1. Hatua gani zichukuliwe dhidi ya Mbunge anayetumia uhuru wa mbunge kuongea bungeni kwa kutoa TUHUMA ZA UONGO NA ZINAZOPOTOSHA dhidi ya Mihimili mingine ya Dola ?

  Hebu kwanza eleza kinaubaga uongo unaodai kusemwa Bungeni na Mh. Lissu. Alichosema Lissu ni "... dalili zinazoanza kuonekana wazi kwamba baadhi ya Majaji ...". Ni wapi Lissu anapomtuhumu Jaji yeyote? Kwani si kweli kwamba "baadhi ya majaji" hawana uwezo? Mbo huu ni ukweli ulio wazi! Propaganda hazitakusaidia.  1. JE Chama Rasmi cha Upinzani Bungeni kilipata nafasi ya kuijadili hotuba ya Mh. Lissu na kuibariki isomwe Bungeni PAMOJA NA TUHUMA? Au ILIKUWA ni hotuba Binafsi ya Mh. Lissu ambayo haikupitia katika mfumo wa kimajadiliano na kimaamuzi (shadow cabinet) ndani ya kambi ya upinzani?

  Si kazi yako kujua "Chama Rasmi cha Upinzani Bungeni" kinafanyaje kazi yake wala hupaswi kujua mikakati yake.
  1. Je wanachama binafsi ndani vya vyama ni bora kuliko uamuzi wa chama?

  Uamuzi wa chama wa kuwafundisha "wabunge" wao nini cha kuongea Bungeni? Huu ndio uamuzi wa chama (magamba style) unaomaanisha? Kama ndivyo, utaratibu huu na upotee milele.
  1. Je Chama Rasmi cha Upinzani kina uwezo wa kuwadhibiti baadhi ya wanachama wao ambao ni « el-maarufu »?

  Kinachofanywa na wabunge wa CHADEMA ambacho kinahitaji kudhibitiwa ni kipi? Kuwatetea wananchi na kusema ukweli? Badala ya kudhibiti waimba taarabu, mipasho, na watoa matusi unataka wasema ukweli wadhibitiwe! Akili za magamba sijui zimejikusanya sehemu gani ya mwili.  Kwa bahati mbaya, watu wengi wanaamini kuwa Mh. Lissu ni Mwanasheria bora kuliko wanasheria wote katika Jamhuri ya Muungano. WAtanxzania wengi wanaamini chochote kinachosemwa na viongozi kama Mh. Lissu ni sahihi na kweli tupu.

  Kwa maneno na matendo watu (Chama) huthibitisha ubora wake.

  Kwa bahati mbaya, hata Magazeti yalimnukuu huyu Mbunge bila kunukuu yaliyosemwa na wabunge wengine kuhusu tuhuma alizotoa Mh. Lissu.

  Jiulize kwa nini magazeti yalifanya hivyo bila hata kupewa bahasha za khaki! Au ungefurahi kama yangenukuu "utumbo" wa magamba kama ifanyavyo TBCCM?


  Je ni kitu gani kimeyazuia Magazeti kufanya uchunguzi wa kina na kubaini ukwel ;i kuhusu uteuzi wa Majaji ? Je uwezo wa magazeti na waandishi wa habari kufanya uchunguzi wao wa kina umepotea hapa Tanzania ?

  As above.

  MHESHIMIWA SPIKA. Tuhuma dhidi ya Rais, Mahakama na maafisa kadhaa wa Umma zilitolewa ndani ya Bunge lako. Mh. Lissu anajua kuwa kama angetoa hizo tuhuma nje ya Bunge walioguswa na tuhuma hizo wangefuata utaratibu wa Kisheria kurudisha heshima yao mbele ya jamii.

  Ili kulinda utawala wa sheria na heshima ya Bunge, ili kulinda heshima ya Mahakama na pia heshima ya Rais na ili kulinda heshima ya watumishi wa umma waliotuhumiwa bila ya wao kujitetea: ninakuomba Mh. Spika uamuru uchunguzi wa kina ufanywe ili kujua ukweli wa mambo.

  KWA KUWA MH. ALITOA TUHUM ZAKE MBELE Y WATU WOTE WALIOKUWA WAKIANGALIA RUNINGA, NINAOMBA KUWA WAKATI WA UCHUNGUZI HUO SISI WANANCHI TURUHUSIWE KUHUDHURIA ILI HUO USHAHIDI WA MH. LISSU TUUONE BILA KUSUBIRI KUAMBIWA.
   
 8. W

  Wimana JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Mbugi, waweza kuwa sahihi kwa sehemu ndogo lakini ukweli uko wazi, kuna ombwe na udhaifu mkubwa sana kwenye nafasi mbalimbali za umma.
  Njia rahisi ni kuangalia productivity za hao wateule, majibu utayapata hapo. Njia nyingine ni mrejesho wa jamii, ambapo leo, Watanzania hawaliamini Jeshi la Polisi na Mahakama, na ndio maana Mob justice zimekuwa za kawaida siku hizi.
  Hilo nalo linahitaji kuunda Tume? Hushangai siku hizi ati Polisi nao wanaunda Tume za kuchunguza uhalifu? Je, hawana kitengo cha upelelezi?
   
 9. n

  nhassall Senior Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani inasikitisha kuona nchi yenye vyama vingi ndani ya chama kimoja, inakuwaje ccm wakiambiwa ukweli wanakimbili kuhukumu na kutetea huo ukweli kwa nguvu zote? kwa nini wasichukue makosa yao na kujifunza? Inawezekana kabisa kuna ukweli kabisa ndani ya tuhuma hizi lakini wanavyopenda kupindisha ukweli kwa kutumiaubabe wao tutaendelea kusikia tu. Na ikumbukwe kikwete serikali yake imekuwa ya kishikaji mno kwa hiyo inawezekana tu akawa amewateua hao majaji bila sifa na hilo liko wazi sana.
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  threads zimekuwa ka tatu, Mods mziunganishe, thanking you
   
 11. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli mtupu majaji wengine walioteuliwa na JK wana mapungufu sana. It is simple, Tafuta hukumu walizozitoa na uzilinganishe na majaji walioteuliwa kwa sifa stahiki, utaona tofauti kubwa sana. hukumu zao zina mapungufu makubwa. Mfano mzuri ni ile ya Jaji Mwakibalira, ilikuwa na mapungufu ambayo hutegemei jaji ayaandike. Labda staili ya kutoa hoja kama haikuwapendeza wengi ambao wana mlengo wa CCM wa kulindana!!
   
 12. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huu ni ukweli,kipindi cha nyuma kuapisha Jaji ilikua inachukua muda mrefu,na hii si kwa bahati mbaya ilikua inafanyika vetting ya kutosha sana.siku hizi unashangaa wanaapishwa majaji kama mafungu ya pilipili hoho lazima ujiulize kwa nini?mafisadi wanajiandalia usalama wao kila mahali.Kuna makesi ya kagoda,richmond sasa unafikiri wataepuka vipi mikasa hiyo?Hii serikali itakapo toka madarakani , itabidi ifanyike asssessment ya wote waliochaguliwa na huyu jamaa.
  Angalia hata teuzi za viti maalum na ukuu wa wilaya,wengi ni vidosho na wabeba mikoba na pia watoto wao.Serikali hii kila kitu kinawezekana.
   
 13. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mengine anayosema lissu ni kweli..kuna jaji mmoja mwanamke sitamtaja lakini najua hana uwezo wa kua jaji maana history yake tunaifahamu na ingekua ni wakati wa mzee mkapa asingempa ujaji mwanamama huyo
   
 14. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Alichosoma Lissu ni malalamiko toka kwa majaji waandamizi
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Awamu ya kwanza mpaka ya tatu watu walikuwa wanachaguliwa kuwa majaji kwa kutimiza vigezo. Ameharibu Kikwete kuanza kugawa ujaji kama zawadi. Wakati Mkapa anamaliza muda wake,aliacha orodha ambayo tayari ilikwisha pitishwa ktk taratibu zote ikingojea kutangazwa,JK alipoingia madarakani akakata majina karibu yote akateua marafiki na maswahiba zake! Kuanzia hapo ni vurugu tupu!
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuuu tatizo la ccm huwa hawakosei wakati huku mtaani tunayaona makosa mengi sana!
  Mala mwenyekiti anapokea pesa za miradi ya ccm anakula yoote lakini wao wanataka waonekane wema!
  Kujisahihisha ndiko kutakakoiokoa ccm lakini kujifanya hawakosei kunaiua kabisaa!
   
 17. J

  Julian Emmanuel Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 6, 2007
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hii ndio sera yetu Tanzania ya mfumo holela

  hakuna mahali kunatendeka usawa, hata wanaolalamika mkiwapa nafasi watafanya hayohayo, sina maana ya kutetea serikali bali ninasema katiba mpya tuunde taasisi za juu kila moja imara hasa bunge likiwa imara likasimamia serikali tutapunguza mengi.

  waziri anatetea uteuzi kwa kusema raisi lazima ateue anaowajua? sasa nchi ni ya kwetu sote au ni ya raisi na anaowajua?

  mbunge anauliza kiasi anacholipwa kwa maana ya posho mjumbe wa kamati ya kukusanya maoni anaambiwa ni siri baina ya mwajiri na mwajiriwa sijui hawa ni wanasheria wa wapi hata hawatambui mamlaka zilivyo bali kujiona wao walopewa dhamana ndio waajiri
   
 18. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  Tanganyika law society ndio watu wa kwanza kulaumiwa wakati Godbles Lema akimkataa jaji aliyepangiwa kusikiza kesi yake kwa kumhusisha na kesi ya EPA pamoja na jaji kumtaka atoe uthibitisho sikusikia kauli yoyote toka Tanganyika law society kule zanzibar chama chao walijitokeza waziwazi kupinga uteuzi wa jaji mkuu pamoja na baadhi ya majaji kwa kuamini Dr.Shein alipotoshwa ingawa utuzi uliendelea lakini hawakuwa wanafiki ningefurahi kama Tundu Lissu angewakilisha malalmiko yake Tanganyika law society ili nao tusikie msimamo wao kwani hili swala si lakusemewa na mwanasheria mkuu au waziri husika inabidi kauli itoke sehemu nyingine ambako ni chombo huru
   
 19. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  my friend, majaji wangekuwa wameteuliwa kwa vigezo vya ujuzi na kufuata utaratibu sahihi, hakika yake wasingekuwa mambumbumbu namna hiyo. kwa wale wanasheria wanaoenda high court wanajua hili kuwa, kuna majaji kibao ambao kwanza hawana maadili, hawana historia ya maadili huko walikotoka (either kama walikuwa kwenye sector ya AG, mawakili wa kujitegemea au mahakimu). angalia kwa mfano yule jaji wa arusha wa kesi ya Lema, hauhitaji shule kujua kuwa asilimia kubwa ya majaji tz ni wa aina yake, na wapo kama vibaraka tu. hapo dsm wanakula senene ajabu (wengi wao wahaya hivyo kula rushwa kunaitwa kula senene pale dsm)....kuna kesi unajua kabisa hapa jaji amechukua hela, na kwa ujuzi wake amejitahidi kutengeneza maneno hadi kitu kikubalike kisheria. wana kiburi hao, kama huamini kaulize wasajili wa mahakama kanda mbalimbali,kwa hawa wanadamu, sina la kusema....hawana maana.
   
 20. M

  Mabala The Farmer Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! Kaka kichwa nimekukubali,nomba usiendelee kuwapa data maana wengi wao wanaobisha humu ni watoto wa hao Dhaifu ambao na wao wanahitaji hivyo vyeo vya kupewa bila taaluma,siwamezoea kupeana vijiti. Hv nataka niulize walalahoi mbona tumepiga book ila kazi hatuzioni,LISSU twende kazi
   
Loading...