Tuhuma za Mengi kwa jeshi la Polisi zilizimwaje?

Kuna kila sababu ya jeshi la polisi kujengwa upya!majambazi wengi ni marafiki wa polisi.Wauza gongo wengi ni marafiki wa polis.Wauza madawa ya kulevya wooote.Matapeli wote ni marafiki wa polis.VIBAKA wote ni maadui wa polisi.YOTE NISEMAYO,NDO NAYAONA HUKU NILIPO JAMANI.sina iman na jeshi langu milele daima aaamen!
 
Kesho kuna kipimajoto ITV kinachosema Tatizo la Raia kuua polisi, nini kifanyike? nahisi hii pia ni sehemu nzuri ya mchango kuwa umakini wa polisi katika kutatua migogoro na kuishi vizuri na jamii inaweza kuwa inachangia sana katika kuleta kutoelewana kati ya polisi na raia.Polisi mwadilifu hawezi kugombana na raia katika kuleta haki isipokuwa pale ambapo raia ametenda kosa.

Pia wako watu wengi katika mahabusu na magereza kwa makosa ya kubambikiwa au kuhisiwa visivyo. Jeshi la polisi umakini unaweza kuwa umepungua sana katika kuhakikisha inatenda haki na kufanya upelelezi wa kitaalamu.

Pia uadilifu wa raia katika kuhakikisha haki inatendeka kila mahali ni muhimu. Unapokuta Taifa la wahalifu ni rahisi kukuta polisi wasio waaminifu maana hao polisi ni "reflection" ya raia wa nchi hiyo.

Nafikiri ni wakati muafaka kama hatujaona tuanze kujiangalia upya kama jamii na kama mtu mmoja mmoja matendo na mienendo yetu ili iweze ku reflect uadilifu unaotakiwa na jamii kila wakati na kila mahali katika nchi yetu.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Nashanga wana JF na waTanzania tuhuma kubwa kwa jeshi la Polisi na maafisa wake waandamizi zilizotolewa na Reginald Mengi kuwa Polisi kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa Kiasia waliandaa mpango wa kumbambikia Mwanae madawa ya kulevya Airport, na akawataja kwa majina akasema kama wanapinga waende mahakamani, nashangaa jambo hili linataka kupita kimyakimya! Hivi hii nchi inaongozwa kwa nguvu za giza au? Tunaweza kweli kupuuzia tuhuma kubwa kiasi hiki? Kama IGP alishindwa kuchukua hatua anasubiri nini kwenye uongozi? Au naye hajui kujiuzulu na hana wa kumwajibisha? Hii ndiyo Bongoland! Mambo yanayofanyika hapa hakuna nchi yeyote yanaweza kuvumiliwa!

Si hilo tu ...mimi nashangaa yafuatayo
1. WAZIRI MKUU KUSEMA UWONGO BUNGENI NA USHAHIDI KUWAKILISHWA LAKINI KIMYAAAAAAAAAA................
2. WALIORUDISHA FAEDHA ZA EPA HAKUNA ANAYEWAJUWA ZAIDI YA WAO...............................
3. DHAHABU ILIYOKAMATWA PALE AIRPORT NA MREMA......KIMYAAAAA..........................
4. MEREMETA MTOTO WA MKULIMA ALISEMA HATA AKISURIBIWA HAYUKO TAYARI KUSEMA LOLOTE NA HADI LE .....KIMYAAAAAAA.....
5. LIST YA WALA RUSHWA WA BANDARI ANAYO RAIS LAKINI ANAIJUWA YEYE PEKEE NA WATU WAKE.KWETU SISI KIMYAAAAA.....
6. etc.......etc...............
 
Walio2humiwa na mzee mengi walikua ni zco charles mkumbo na mkuu unt drugs bwn nzowa cha ajabu nzowa kabaki palepale mkumbo katolewa central kapelekwa makao makuu akasome magazeti.
 
Kama chama tawala kinaongelea KUJIVUA GAMBA kwa nini taasisi za serikali kinachoiongoza nazo ZISIJIVUE GAMBA??? Ikitokea TAFADHALI JESHI LA POLOSI WAWE WAKWANZA.....
 
Inapokuja kwenye suala la maslahi ya wakubwa hali huwa ni tofauti sana, hakuna sheria wala hatua zinazochukuliwa! Kwani hamkumbuki ile kesi ya milioni 900 ya Mrema imeishia wapi?

Tunajifanya tunafuata utawala wa sheria lakini ukweli hiki ni kiinimacho tu, hakuna cha utawala wa sheria wala haki. Mi nadhani wananchi sasa waamke na kuchukua hatua kama zilizochukuliwa na wananchi wa Tunisia au Misri.
 
Kesho kuna kipimajoto ITV kinachosema Tatizo la Raia kuua polisi, nini kifanyike? nahisi hii pia ni sehemu nzuri ya mchango kuwa umakini wa polisi katika kutatua migogoro na kuishi vizuri na jamii inaweza kuwa inachangia sana katika kuleta kutoelewana kati ya polisi na raia.Polisi mwadilifu hawezi kugombana na raia katika kuleta haki isipokuwa pale ambapo raia ametenda kosa.

Pia wako watu wengi katika mahabusu na magereza kwa makosa ya kubambikiwa au kuhisiwa visivyo. Jeshi la polisi umakini unaweza kuwa umepungua sana katika kuhakikisha inatenda haki na kufanya upelelezi wa kitaalamu.

Pia uadilifu wa raia katika kuhakikisha haki inatendeka kila mahali ni muhimu. Unapokuta Taifa la wahalifu ni rahisi kukuta polisi wasio waaminifu maana hao polisi ni "reflection" ya raia wa nchi hiyo.

Nafikiri ni wakati muafaka kama hatujaona tuanze kujiangalia upya kama jamii na kama mtu mmoja mmoja matendo na mienendo yetu ili iweze ku reflect uadilifu unaotakiwa na jamii kila wakati na kila mahali katika nchi yetu.

Mungu Ibariki Tanzania!


Askari wetu hapa Tanzania wao hua akikuta mtuhumiwa moja kwa moja anakua treated kama muhalifu... Hapo utapigwa, utanyanyaswa, utashushiwa utu wako kabisa.... Yaani Askari police ni judge mtoto, hata akimuua mhalifu issue hua hafuatiliwi labda afanye hivyo mbele ya macho ya jamii na kusiwe na ushahidi kua marehemu ni mharifu... Wanachi wa Tanzania ni wapole saana, huruma nyiiingi - hivyo mpaka wamefika hio stage kweli jeshi la police litafakari kwa undani matendo yao na wachukue hatua....
 
Hivi ile issue ya Mtoto wa Mengi ya kutaka kubambikiwa Mihadarati na baadhi ya Askari polisi wa kitengo cha Madawa ya kulevya imepotezewa!

Nilichosikia mimi ni kwamba ile issue ilikuwa madawa yawekwe baada ya mizigo kupita katika mkanda wa kukaguliwa.

Kilichofanya siri ile kubumburuka ni mmoja wa askari ambaye alishirikishwa kuingiwa na tamaa na kwenda kuvuta mkwanja kwa Mengi pia kwa kumuuzia siri ile.

Askari huyu ameshahamishwa toka Kitengo cha Madawa ya kulevya Airport na sasa ni Askari wa Kawaida. Ilikuwa apigwe Transfer kwenda Dodoma, lakini kilichomwokoa ni kwasababu tu anasomea degree yake ya Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam Branch/Campus.

Nimemegewa na Mmoja wa Askari kitengo cha Madawa ya Kulevya Airport.

Hii ndio Tanzania zaidi ya Uijuavyo! Kwa anayebisha afanye Utafiti ataligundua hilo.
 
Asee huyo jamaa aliyemmegea mengi siri amehatarisha life yake kwa kiwango kikubwa,nji hii sasa watu wamekuwa makatili,kumtransfer ni danganya toto.wanakuhamisha af wanakuuwa katika mazngira ambayo haitakuwa rahisi kujulikana umeuwawa,ingekuwa mie kabla ya yote nasaka nji ya kuhamia af reginald namwomba mshiko wa kueleweka kisha nasepa zangu maisha matamu bwana.tene ndo ushashkishwa bora uende zako.heri nusu shari kuliko shari kamili
 
Said Bagaile!!!

Bado uko mgeni hapa jamvini kuwa makini kusoma kabla hujarukia misosi sijui source .Kila kitu si lazima kitoke nje wengine hapa ni source .Sasa jambo kama hili ulitegemea nani aseme maana hata magazeri ya Mengi hayaandiki na waandishi walisha sahau tuko wako wako tu .
 
ile kesi sijui imesihia wapi-na takukuru,polisi na wengineo wamesinzia kwenye hili swala
 
Hivi nyie mnaouliza source, ni lazima habari iandikwe gazetini ndio iwe na source!

Mie nimesema nimemegewa na mtu wa humo humo ndani. Na kisha nikasema kama unataka kupata uhakika zaidi fuatilia, je hakuna kijana aliyekuwa kitengo cha madawa ya kulevya akahamishiwa Polisi wa kawaida? Je hakupigwa transfer Dodoma kabla ya kurudishwa Dar kwa kuwa tu anasoma Tumaini University?

Na kama si kwamba hii kesi imepotezewa, Je hujiulizi katika shutuma kubwa aliyoitoa Mengi juu ya Maofisa wa Juu wa Polisi kama akina Nzowa na wenzake halafu hakuna aliyeondolewa wala Mengi kushtakiwa kwa kulichafua jeshi la Polisi?

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo wewe Mzee wa kutaka source lazima zitoke kwenye magazeti ya Annur.
 
Back
Top Bottom