Tuhuma za Mengi kwa jeshi la Polisi zilizimwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma za Mengi kwa jeshi la Polisi zilizimwaje?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mafie PM, Apr 14, 2011.

 1. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Nashanga wana JF na waTanzania tuhuma kubwa kwa jeshi la Polisi na maafisa wake waandamizi zilizotolewa na Reginald Mengi kuwa Polisi kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa Kiasia waliandaa mpango wa kumbambikia Mwanae madawa ya kulevya Airport, na akawataja kwa majina akasema kama wanapinga waende mahakamani, nashangaa jambo hili linataka kupita kimyakimya!

  Hivi hii nchi inaongozwa kwa nguvu za giza au? Tunaweza kweli kupuuzia tuhuma kubwa kiasi hiki?

  Kama IGP alishindwa kuchukua hatua anasubiri nini kwenye uongozi? Au naye hajui kujiuzulu na hana wa kumwajibisha? Hii ndiyo Bongoland! Mambo yanayofanyika hapa hakuna nchi yeyote yanaweza kuvumiliwa!
   
 2. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona tuhuma za Mengi zilishajibiwa kwa vitendo siku nyingi mkuu? Walipeleleza walikuta ni kweli wakahamua kuchukua hatua za kistaarabu kwasababu wote ni vigogo. Hatua zenyewe ni hizi...........
  1. Wamemhamisha yule kamanda Nzowa ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha unga pale airport na kumrudisha central
  2. Mkumbo aliyekuwa mkuu wa upelelezi k'ndoni (ambaye anadaiwa na Mengi kwenda na Rav 4 kuchukua pesa) aliondolewa kwenye post hiyo na kurudishwa central
  3......mwenye data zaidi atujuze............
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  eeeh mkuu rahisi kiasi hicho eeh!
   
 4. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Yap, serikali ilishikwa pabaya wakaizima kistaarabu, waliwahamisha vituo wakapiga kimya.
   
 5. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  nadhani hiyo haikutosha peke yake, walipaswa kuchukuliwa hatua zaidi
   
 6. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hii nchi imelaaniwa hakika! Mtu akiharibu hapa anapelekwa pale! Si walitakiwa watueleze kama ni kweli na mtu aliyetenda kosa kama hilo huwa anafanywaje? Tutaliheshimu vipi na kuliamini jeshi la polisi?
   
 7. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tuhuma za Mwakyembe dhidi ya wauaji wake zilikuwa so specific and detailed kuliko labda hata hizi za Mengi. Ungetegemea kuwa labda kesho yake asubuhi watu wangeanza kuwa arrested, lakini wapi watu wandunda tu. Unafikiri kuna anayeshtuka?
   
 8. k

  kamimbi Senior Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukisikia kujivua gamba ndo kama hivyo, hii ndo tz na hawa ndo viongozi wetu.
   
 9. kinja

  kinja Senior Member

  #9
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kweli mkuu, iba kuku ufie jela
   
 10. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ndo silikali ya wadanganyika unahalibu ubungo unasogezwa mbagara iba kuku uone sheliya inavo fanya kazi
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Marekekebisho kidogo mkuu
  1.Nzowa alikuwa mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya
  2.Mkumbo alikuwa ZCO(Zonal Crime Officer)
  Wote wapo bench pale makao makuu ya jeshi la polis.hizo ni hatua za kinidhamu za jeshi lakina za kiraia nadhani hawajachukuliwa,na zingefanyika iwapo wangevuliwa uaskari na kushtakiwa.pengine inahitaji zaidi msukumo kutoka kwa mlalamikaji
  Ndio TZ ilivyo mambo kulindana...aargh!
   
 12. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Huyu ni Mengi amefanikiwa kiasi kwa kutoa tuhuma hadharani na kutaja majina na kiasi cha fedha. Je angekuwa mtu wakawaida si angebambikiwa madawa na kufungwa kabisa jela, watu wangeamini kuwa huyo alikuwa anafanya biashara ya madawa ya kulevya.

  Hata hivyo Mkuu wa Polisi amechukuwa hatua laini sana licha ya kupata ukweli hata baada ya kuunda tume yake. binafsi nilitegemea wangefukuzwa kazi kabisa
   
 13. wakusoma

  wakusoma JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 949
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 180
  aliyeandaa mpango mzima ni kiongozi anayejihusisha sana na yanga.inasemekena alimwaga hela chafuu,huenda hata IIGP alivuta cha juu
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,171
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Ndugu watanzania
  Leo nimekaa nikaikumbuka lile sakata la mtoto wa mengi kutaka kuwekewa dawa za kulevya pale uwanja wa ndege wa julius nyerere....nimekuwa kwenye toba tukikumbuka mateso ya YESU kristo kufa kwa kumwaga damu yake na kujiuliza je mkuu wa kituo cha madawa ya kulevya anaweza kutupa sababu kuu za kuliamini jeshi la poilizi tena kwa mtaji huu

  1))MPAKA SASA AKUNA ALIESEMA CHOCHOTE UPANDE WA JESHI LA POLISI ZAIDI YA USANII NA KIZURI MENGI AKUSITA KUTAJA MAJINA AKIWEMO HUYUU MKU WA MADAWA YA KULEVYA BW GODFREY NZOWA..SASA ANAWEZA KUTUAMBIAA NI WANGAPI WAMEWEKEWA MADAWA YA KULEVYA NA KUFUNGWA MIAKA 20 NK????

  2))MKUU WA MADAWA YA KULEVYA ANAWEZA KUTUELEZA UKWELI HALISI YALE MANENO YALIISHIA WAPI PAMOJA NA USANII WA KUTANGAZA KUFWATILIA NA JESHI LA POLISI KUTOA MAJIBU HARAKA IWEZEKANAVYO

  3))ANAWEZA KUTUELEZA ZILE DAWA ZINAZOPATIKAANA ZINAPELEKWA WAPI NA KAMA ZIPO ATUELEZE ZILE ALIZOKUWA ANABAMBIKIZWA MTOTO WA MENGI ZILIKUWA ZINATOKEA WAPI???JE JESHI LA POLISI LINALINDA DAWA ZA KULEVYA??

  4))WATANZANIA WENGI WAMEAMUA KUAMKA JE HUYO GODFREY NZOWA MKUU WA MADAWA YA KULEVYA ANAWEZA KUTUAMBIA ZILE KG 70 ZLIIZOPATIKANA TUNDUMA NA MWENYE MALI KUKIMBIA ZIKAAMBIWA ZINAKUJA DAR KWA UCHUNGUZI BAADA YA HAPO ZIKAFIKA DAR KG 40 MBAYA ZAIDI KATI YA PKT KADHAA ZIKAKUTWA NA UNGA WA NGANO BADALA YA MADWA NA WAMEKAA KIMYAAA ANAWEZA KUTUMBIA ZIMEENDA WAPI NA WAHUSIKA WAMECHUKULIWA ATUA GANI???

  JESHI LA POLISI LIJIVUE GAMBA MNATIA AIBU KABISA AKUNA AJA YA KUONEANA AIBU IFIKE WAKTI MTU AKIRI AJIUZULU KWA UPUUZI WAO
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh! Aisee
   
 16. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Haikosi, ila Wahindi kama hawajajua uadui tunaotengenezewa na huyu jamaa pamoja na ccm hakika wasubiri kidogo watajua kuwa India siyo mbali hata kama wamezaliwa hapa.
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180  Habari hizo ni kweli kua zinatolewa hadharani na wananchi tunaweza bahatika kusikia, lakini si kwamba yanaishia hewani. Haya mambo hua yanaendelezwa kujadiliwa na kutatuliwa mijengoni, wewe Mengi kama kaongea hivyo katika vyombo vya habari, do you think hawakumtafuta? ila sasa waandish wako more interested na yale ambayo yanauza magazeti - ni wachache wenye guts za kufuatilia mwanzo wa habari hadi the final outcome. Wengi kazi yao kumwaga habari lakini si kumwaga taarifa ya habari wanazotoa
   
 18. k

  kifuniboy Senior Member

  #18
  May 2, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  NAMPENDA SANA MENGI..ILA KWA HILI NA YEYE NI KAMA PUMBAVU WENGINE TU...MBONA ALIKURUPUKA KUUAMBIA UMMA TENA KWA KISHINDO,,.LAKINI HAJAWIHI KUTOA HATA FEEDBACK KUHUSU KINACHOENDELEA,,KAMA HABARI IMEPOTEZA LADHA KWA VYOMBO VYA HABARI JE HATA KWAKE NI HIVYO HIVYO...AU NA YEYE NI MTU WA KUTISHWA KAMA MAKONDOO WENGINE...!!!!!!!!!!.
  Tanzania bila kuchinja mtu haiendi..........
  ni kautani kabaya haka lakini katakuwa ka kweli....
   
 19. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Acha kumkosea adabu Senior Citizen wa ukweli, yeye hakukurupuka kwani alielezea kila kitu in detail. Kwa vile jambo hilo waliohusika ni wafanyabiashara wakubwa wa kihindi wakishirikiana na viongozi wakubwa wa jeshi la polisi, hakuwa na namna nyingine la kulielezea. Kama ange toa taarifa polisi kimya kimya bila kuutangazia umma, huwenda makubwa yangemkuta mtoto wake na kuathili wasifu wake mbele ya jamii! Lakini baada ya kugundua hatari iliyopo ndo maana aka amua kulitangazia Taifa ili chochote kikitokea basi watanzania wawaelewe wahusika.

  Kwa nia njema kabisa Mengi alitimiza wajibu wake na asingefanya hivyo, huwenda leo historia na wasifu wake vingebadilika kabisa..
   
 20. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  tatizo kubwa kwa Tanzania Police Force Official ni kulinda maslahi yao hivyo kujikuta wanaingia katika mitego ya chambo kama huo.amini nawaambia wahalifu na matapeli wote wakubwa ndo marafiki wakuu wa viongozi wa ngazi za juu za polisi
   
Loading...