balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 14,427
- 12,542
pole sana MeloNdugu wana JF na watanzania kwa ujumla,
Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.
Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.
Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).
Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.
Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.
Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.
Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!
Once again, asanteni sana na Mungu asimame nasi katika kuijenga nchi yetu, Tanzania.
Maxence