Tuhuma za mauaji: Nimehojiwa na Polisi, nimetimiza wajibu wangu

Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.

Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.

Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).

Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.

Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.

Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.

Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!

Once again, asanteni sana na Mungu asimame nasi katika kuijenga nchi yetu, Tanzania.

Maxence
pole sana mkuu, mungu akulinde, akuepushe na mabalaa na watu wabaya
 
lisu kapigwa risasi ili afe, lakini miaka kadhaa baadae bado tunaambiwa anasubiriwa yeye na Dereva warudi wahojiwe ndio uchunguzi uanze.

lakini kwa Mwingine wale aliowataja kutaka kumuua wameitwa na kuhojiwa immeadiately.

Hakika tuna jeshi lenye weledi wa hali ya juu.
 
Pole Max,
Napenda kukutaarifu kuwa huo ndiyo UHURU USIOKUWA NA MIPAKA.Tuyaishi maeneno yetu. Hakuna habari isiyoumiza upande fulani. Hata Humu JF jua kuwa kuna watu wanaumia kama ulivyoumia kwa taarifa za kweli au za uongo zinazochapishwa hapa. TUVUMILIANE na Siyo TUVUMILIWE tu.

Tulitarajia mtajitokeza wenye huo mkakati. Ila mkakati wenyewe upo kizee sana. Dunia ilishaamka nyie ndio bado mmelala na ndio maana mna matumizi makubwa ya nguvu kuliko akili.
 
Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.

Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.

Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).

Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.

Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.

Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.

Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka.
Musiba amelalamika rasmi polisi kwamba kuna watu wanapanga kumuua au amelalamika kupitia hayo majerida yake? Kama amelalamika, maelezo yake yamechukuliwa kwenye kituo gani cha polisi? Isiwe unahojiwa bila shitaka rasmi dhidi yako polisi.
Mkuu wasamehe bure hawa watendaji wetu kwani wasipofanya hivyo watapokea pumbavu za kutosha.
 
POLE SANA KIONGOZI MUNGU ATAKUWA PAMOJA NAWE NAONA WANATAFUTA KITU KWA KUKUWEKA WEWE CHAMBO KUWA MAKINI
 
Yani mtu anakuhisi kuwa unataka kumuua badala ya yeye kuhojiwa na police kwa niñi anakuhisi unahojiwa wewe,aisee yani kama kuna mtu mwenye akili timamu anamlinda musiba basi
 
Tulitarajia mtajitokeza wenye huo mkakati. Ila mkakati wenyewe upo kizee sana. Dunia ilishaamka nyie ndio bado mmelala na ndio maana mna matumizi makubwa ya nguvu kuliko akili.
Dunia ilishaamka wakati bwana wenu Trump ana-block watu na kushindwa mahakamani.
Dunia ilishaamuka wakati waingereza wanamtia ndani Julian Assange wa Wikileaks kwa kukosoa na kudukua taarifa ovu za mabwana zenu.

Acha ushamba wewe na ulimbukeni wewe Wakina Edward Snownden wamekimbia nchi zao wewe unapiga kelele hapa.

Unapiga Kelele wakati wenzako wanapiga dili la siraha na Saudia Arabia na ripoti ya Khashogi wameweka kabatini.

Kwa taarifa yako wewe ni mbumbumbu unayefuata upepo ukiambiwa nyuma geuka wala hushirikishi ubongo upoupo tu kama speciemen. Dunia haipo hivyo. Mnatumika bila kujijua.
 
Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.

Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.

Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).

Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.

Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.

Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.

Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!

Once again, asanteni sana na Mungu asimame nasi katika kuijenga nchi yetu, Tanzania.

Maxence
Pole sana , it was planned move, kwa nini wasimhoji mhariri wa hayo magazetii?
 
Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi.

Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.

Musiba ni nani nchi hii ?

Tatizo anaowatuhumiwa hawaripoti Police kuhusu tuhuma husika ili Bwana huyu aweze kuchukuliwa hatua stahiki.
 
Dunia ilishaamka wakati bwana wenu Trump ana-block watu na kushindwa mahakamani.
Dunia ilishaamuka wakati waingereza wanamtia ndani Julian Assange wa Wikileaks kwa kukosoa na kudukua taarifa ovu za mabwana zenu.

Acha ushamba wewe na ulimbukeni wewe Wakina Edward Snownden wamekimbia nchi zao wewe unapiga kelele hapa.

Unapiga Kelele wakati wenzako wanapiga dili la siraha na Saudia Arabia na ripoti ya Khashogi wameweka kabatini.

Kwa taarifa yako wewe ni mbumbumbu unayefuata upepo ukiambiwa nyuma geuka wala hushirikishi ubongo upoupo tu kama speciemen. Dunia haipo hivyo. Mnatumika bila kujijua.

Alisikika mpuuzi mmoja.
 
Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!

Kwa hiyo sentensi kwa mimi nimekuelewa mna sana tuu.... ila habo kwenye kumwomba Mungu ndio nasema hivi Nia tunayo nguvu tunayo.......... Week end njema

Eeeee Mungu uchaguzi wa mwaka 2020 fanya miugiza yako Africa tumechoka kabisa, akili zetu zii gizani oko baba oko sio nia yako kulanzisha bara la Africa na fikra hizi za viongozi ..
 
Back
Top Bottom