Tuhuma za mauaji: Nimehojiwa na Polisi, nimetimiza wajibu wangu

Tatizo uliharibu,pale ulipogoma kutoa zile details za watu!!

Na ulikosea zaidi,ulipomfuta kazi informer Wao!!
Siku,hizi hawana Milango ya Kuingilia!!

Kwa,Ushauri
Jaribu kwenda na beats ila make sure
Hautuuzi!!!

Cc: Maxence Melo
Mkuu. kwenda na beat halafu asituudhi sidhani kama ita wezekana.

Yupo msukuma mmoja humu jf maarufu sana alitaka kufanya yote mawili kwa wakati mmoja, ila yamemshinda na amesha amua kwenda na beat tuu.
 
Ila@Maxence Melo una moyo wa kipekee...labda kwa vile ww mpole...!mie hata kwenda ningeenda saa9!

Jamàni hivi watanzania milioni 55 hakuna wa kumtuliza huyu Mwanaume alotolewa mahari na mwanaume mwenzake??

Alafu jitu jenyewe halina hata mvuto jamani...yaan mie nachefukwa....i wish siku nikutane jaman na huyo musiba...maneno nitakayomropokeaa!shenzy kabsa...laana ikamuandame yy na vizaz vyake vyt
 
Mkuu. kwenda na beat halafu asituudhi sidhani kama ita wezekana.

Yupo msukuma mmoja humu jf maarufu sana alitaka kufanya yote mawili kwa wakati mmoja, ila yamemshinda na amesha amua kwenda na beat tuu.



Hahahahaa..ninong'oneze huyo msukuma..kma namkisia...
 
Najaribu kuwaza sana kwamba kwanini JamiiForums na kwanini @Maxence @Melo ....!!??
Bilashaka kuna maslahi binafsi ya watu flani yanayo athirika pakubwa kutokana na mtandao huu kuyaanika madhambi yao.
 
Aisee sasa mi swali langu ni Je hao polisi kama watuhumiwa wao watahojiwa na nani??? kwa akili yangu yenye uweledi nilidhani kwamba polisi wangejitoa kwenye kuhoji watuhumiwa mana nao ni watuhumiwa.
 
Pole sana mkuu ''

Kwa hii statement Watesi wetu lazima wanune na kufura kwa hasira. .maneno yako yamejaa Nguvu ya Ukombozi kwa wa tanzania ambao mioyo yao inalia machozi kutokana na kutokubaliana na kile kinacho endelea katika taifa hili 'Huku macho yao yakiwa haya amini kuona Wimbo wa Tanzania ni nchi ya Amani uliokuwa unaimbwa masikioni mwao ukianza kutoweka '

Taifa lime Pata viongozi wanao tugawa wa - tanzania Tumeanza kuwa maadui na ile dhana ya U-ndugu tuliyo nayo inazidi kutokomea Gizani ' mahala tulipofikia nadhani hata shetani ana tu-shangaa

Naomba mniruhusu ni Mtukane Musiba tafadhali
 
Bila kuwa mnafiki..
Hapa wengi watakupa pole lakini huwezi shutumiwa hivyo ukakaa kimya laxma kunaukweli ndani ya matamko ya Musiba..

Tafuta njia sahihi kutushawishi otherwise itakua unatambaa na ile formula ya wapinzani "victimised"
 
Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!
Hii paragraph hata mimi niliielewa sana!
 
Gazeti lime toka asubuhi na wewe mpaka saa 3 asubuhi ikawa umesha pigiwa simu na kuitwa makao makuu ya Police ---

Musiba na Watu waliopo nyuma yake ni wapuuzi kweli hao 'Hiyo michezo ya kitoto Waka wafanyie baba zao na wafuasi wao wa Lumumba
 
Huyu Musiba kwa walio wengi ni MTU mbaya, LA hasha! Ni MTU anakusaidia wewe na Mimi hasa wanasiasa; ccm hata upinzani kwa upande mmoja na watanzania kwa ujumla. Kwamba anything bad to your brother or sister be him/she in different faith whatsoever never do bad to he/her. Inashangaza Leo Nape, Member, January, Nchimbi na wote was upande wa chama tawala siku wakiwa kwenye vikao vyao rasimi kwa mfano wawe katika kikao kitakacho amua Kuhusu Katiba mpya na umuhimu wa katiba utaona wanaunga mkono upande wa watawala hata kama nao wanaona na kujua kuwa ni katiba mpya tu iwezayo kuleta haki kwa kila MTU na sheria nzuri .......endelea ...ccm members hawaeleweki
 
Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.

Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.

Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).

Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.

Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.

Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.

Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!

Once again, asanteni sana na Mungu asimame nasi katika kuijenga nchi yetu, Tanzania.

Maxence
POLE MKUU!JEE ULIWAULIZA MUSIBA BINAFSI AMEFUNGUA KESI DHIDI YENU?MAANA TUHUMA ZA KUMUHUSU YEYE MUSIBA,POLISI HUSEMA HAKUNA KESI ILIYOFUNGULIWA.
Ila kiuhalisia Musiba ndiye atakayeivuruga hii nchi kwa kigezo cha kumlinda eti mtu mmoja madarakani.
 
Ukisema Musiba ni kwamba umemtaja Mburundi yuleyule.

Tanzania haiwajawahi wala haitakaa iwe na Takataka kama hii
Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi.

Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.

Musiba ni nani nchi hii ?
 
Musiba ni agent wa shetani Lucifer
Mungu mkubwa IPO siku atachukia kuwa agent maana Mungu atamwadhibu huyu kiumbe
 
Pole sana mkuu ''

Kwa hii statement Watesi wetu lazima wanune na kufura kwa hasira. .maneno yako yamejaa Nguvu ya Ukombozi kwa wa tanzania ambao mioyo yao inalia machozi kutokana na kutokubaliana na kile kinacho endelea katika taifa hili 'Huku macho yao yakiwa haya amini kuona Wimbo wa Tanzania ni nchi ya Amani uliokuwa unaimbwa masikioni mwao ukianza kutoweka '

Taifa lime Pata viongozi wanao tugawa wa - tanzania Tumeanza kuwa maadui na ile dhana ya U-ndugu tuliyo nayo inazidi kutokomea Gizani ' mahala tulipofikia nadhani hata shetani ana tu-shangaa

Naomba mniruhusu ni Mtukane Musiba tafadhali
Kwa Kinachoendelea sasa Taifa linapita wakati mgumu na busara isipotumika nadhani tutasambalatika.Kuna uadui na chuki zisizo kifani na chanzo ni huyu ndugu yangu na wanaomtuma. Atokee mmoja tu mwenye Hekima amwambie Msiba tumechoka sana na tunahitaji kujikomboa na anachokiamini na kukitumikia...
 
Back
Top Bottom