ushoroba wa kati
Member
- Aug 12, 2019
- 88
- 98
Mazito sana hayaWapendwa Wana DKMS - KKKT, Salaam katika Kristo Yesu Mkombozi wa wanadamu = Redemptor Hominis!
SABABU ZA KUFANYA MATENGENEZO DKMS - KKKT.
"Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua"
Mithali 29:2.
Inawezekana wengi wenu hamjui kwanini kunahitajika kufanyika matengenezo ya haraka DKMS - KKKT; ni kwamba zipo sababu nyingi sana zilizopelekea jambo hilo:
1. Kuinusuru Dayosisi isiendelee kuongewa madeni.
Kwamba; Uongozi uliopo sasa ambao hauamini kuwa muda wao Kikatiba umemalizika unaendelea kulimbikiza madeni, na hawawezi kufanya muujiza wowote. Deni la SEKOMU tu ni kizungumkuti. Tumshukuru Mungu Ripoti ya Kamati ya Reweta imeshapatikana yote mtayaona kwa uso na macho; hamtaamini jinsi Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu cha Sebastian Kolowa kilivyohujumiwa na kuleta adha kwa Wafanyakazi na Washarika.
2. Kwamba pia Watumishi wengi wa DKMS - KKKT, wanaishi maisha ya dhiki sana, Mishahara na posho zao hawajapata kwa muda mrefu sasa, sijui na janga hili la Corona wataishije maskini ya Mungu. Watumishi hawa wanaogopa kupaza sauti zao; lakini Jipeni moyo Mtetezi wenu yu hai: Msiogope!
3. Kwamba Vituo vingi vya Dayosisi viko hoi(ICU). Vuga Press imefungwa, Bangala Seminary hoi, Lwandai hoi, Hospitali ya Kilindi yachechemea, Bumbuli Hospital nayo ni tia maji tia maji. Hali ni mbaya, kama husadiki tembelea Vituo hivyo utajionea mwenyewe.
4. Kuvuruga uhusiano wa DKMS na marafiki wa Ujerumani.
Hayati Baba Askofu Dkt Sebastian Ignatius Kolowa, ThD, alianzisha Urafiki baina DKMS na Makanisa ya Ujerumani, na mashirika mbalimbali ya Kitume ya Ulaya. Urafiki ulikuwa na manufaa makubwa sana katika Dayosisi hii. Marafiki hao walisaidia sana katika uwanja wa? huduma za kijamii; kama vile, Lutindi Mental Hospital, Irente School for the blind, Irente Children's Home, Usambara Technology Center, ATIFA, Irente, Irente Rehabilitation Center, Rainbow School. Vituo hivyo vilisaidiwa sana kutokana na Urafiki huo. Baada ya Kifo cha Mzee Askofu Kolowa, Dayosisi ikaongozwa na Mt Petro Baba Askofu Joseph Jally, tunamuita Mtume Petro kwakuwa hana makuu, ni? mpole, mnyenyekevu, mwenye upendo, ni mtu wa sala na maombi, alizifuata nyayo za Mtangulizi wake. Akaicha Dayosisi katika hali njema.
Sasa huyu baada ya Askofu Jally, ndio kaiweka Dayosisi kitanzini.
5. Mahusiano ya DKMS na Serikali.
Tokea enzi ya Askofu Dkt Sebastian Kolowa, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ilikuwa na mahusiano mazuri na Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wala hakukutokea chokochoko yoyote. Ushirikiano ulijengwa katika huduma za kijamii, kutembeleana, kushauriana na kuombeana kwa amani. Hata Mzee Askofu Jally, alidumisha mahusiano mazuri.
Sasa kiyangayanga ni kwa huyu Mwanaharakati Askofu wa DKMS asiyetaka kustaafu, kosoa weee Serikali, mapovu yakimtoka, huko yeye mwenyewe akiwa na boriti limemzinga, (Mathayo 7:5). Ukiishi kwenye nyumba ya vioo usiwarushie wengine mawe: Ona sasa kwa matumizi yako mabaya ya madaraka (Mr Mkuu wa Chuo SEKOMU, Mrs Makamu Mkuu wa Chuo, na huku Katibu Mkuu wa DKMS ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha SEKOMU, aah majanga): umeleta janga la kutolipa Kodi ambayo Dayosisi inadaiwa, mamilioni na mamilioni, ujanja wako uko wapi?. Ubadhilifu ndio ulioifikisha DKMS hapa, TRA, WFC, NSSF kote wanadai.
Usijidanye kulipa Kodi ni Amri halali tena ni agizo la Mungu: Soma Injili ya Luka 20:21 - 26.
6. Kuvuruga uhusiano wetu na Madayosisi mengine.
Kama hujui Askofu, DKMS imekuwa na mahusiano ya kihistoria na kindugu; nikuingize darasani kidogo pamoja na hiyo PhD yako, kwa kukupa mfano wa Madayosisi ya Kanda ya tu: Tumekuwa ndugu, udugu wetu ulijengwa na Mababa Askofu Moshi, Askofu Kolowa, Askofu Kweka na Askofu Mshana wa Pare, Askofu Jally na Askofu Msangi. Jamii yetu imechanganyika mno, tunaoshirikiana mno. Uliza siku mwili wa Mzee Askofu Kolowa, uliposafirishwa toka KCMC kwenda Lushoto, mji mzima wa Moshi na Pare ulisimamisha shughuli zao kwa kumuenzi Mzee Askofu Kolowa, walimwona kuwa ni Baba yao. Sisi Waumini wa DKMS hakuelewi kwanini unamshambulia Mkuu wetu wa Kanisa? Halafu unawaeleza washarika Kanisani ili iweje?
Ukome kabisa na uache tabia hiyo. Tena Baba Askofu Charles Mjema wa Dayosisi usimfuate Askofu Munga atakuingiza chaka.
7. Kuwafukuza na Kuwasimamisha Uchungaji baadhi ya Watumishi.
Kama Baba Askofu Kolowa asingemsihi Mkuu wa Chuo cha Makumira Mch Dkt Hans Mwakabana asikufukuze Chuo cha Uchungaji kutokana na uliyoyatenda ukiwa usingefikia hapo ulipofikia (kisa chenyewe tunakitunza).
Umefukuza Mch Dkt Kopwe, Dean Mch Mwamboza, Mch Crispus Kanju, umewasimamisha Mch Peter Zakaria na Mch Dickson, bila sababu za msingi . Aliyekuwa na Katibu Mkuu Mch Godrey Hermann umemfanyia figisu figusu, akaamua kukuachia ofisi. Ulishamsimamisha Mch Shekifu na Dean Mmaka pia. Wote hao umewaumiza, tunajiuliza ni jiroho gani lililokukamata.
8. Kutowathamini Watumishi Wastaafu.
Hivi Askofu Dkt Stephen, unapata muda wa kuwajulia hali Wastaafu pamoja na wajane!. Huna muda huo uko bize. Pension pia huwapi, wakati unataka maslahi makubwa.
9. Mafao ya Askofu Munga atakapostaafu.
Ulipeleka madai ya mafao ya kustaafu kwako kuwa:
a.Ujengewe Nyumba kubwa ya kuishi,
b.Ujengewe Nyumba ya vyumba vitatu (3), kwa ajili ya Watumishi.
c.Uwekewe Watumishi wataolipwa na Dayosisi yaani Dereva, walinzi, wapishi na mfanyakazi wa bustani.
d. Ununuliwe gari kubwa la kifahari V8 au VX
e. Ujengewe bwawa kubwa la samaki, ili uepuke kula RED MEAT(nyama nyekundu), aloo rahaa utamu!
f. Alipwe mshahara unaotosheleza, na kutunzwa hadi ukamilifu wa dahari.
Je, watangulizi wako walifanyiwa hivyo? Wafanyie kwanza halafu wewe ndio ufuate.
Mwisho Wachungaji, Watumishi na Washarika wote wa DKMS msidanganyike; Muda wa kipindi cha Uaskofu wa Munga umemalizika, hana mamlaka ya kuongoza Mkutano Mkuu wala Kikao chochote kabisa.
Bado anaendelea kutumia Gari la Kanisa na Posho, yuko DSM na Wasaidizi wanapanga mkakati wa kujinasua.
FAHAMUNI KANUNI YA 6 ya Katiba ya DKMS - KKKT ya Mwaka 2000:
E.
1. Askofu
c. Askofu atatakiwa kustaafu Kikatiba akiwa na umri wa miaka sitini na tano (65) ya kuzaliwa, lakini anaweza kustaafu kwa hiari yake akiwa na miaka sitini (60).
Habari ndiyo hiyo.
Tena Kanuni hiyohiyo ya 6:
F. Ukomo wa Uongozi.
Kiongozi anaweza kuacha kazi, kuachishwa, kujiuzulu ama kufukuzwa ikiwa;
1. Hatatimiza wajibu wake au akivunja Kanuni na Sheria za Dayosisi.
4.Kustaafu akitimiza umri wa kustaafu kisheria.
5. Kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe.
6. Kujiuzulu kwa kuwajibika.
Jiulize anatokaje hapo?
Ni jukumu lake kutafakari na kuchukua hatua kwani Neno la Mungu lasema:
"Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;
Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
Mithali 22:3
Wakatabahu,
+++ Sauti ya Kijito Kedroni.
Jr
Sent using Jamii Forums mobile app