Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 13,677
- 26,997
Nimegundua kuna madudu na ubabaishaji mkubwa sana wa malipo ya fedha za Kijikimu(Meals and Accomodations) kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha ST. AUGUSTINE MWANZA, ambazo kimsingi ni fedha wanazokopeshwa wanafunzi Ili baadae wazilipe.
Serikali inaingiza hela kwenye account ya chuo mapema tu, alafu chuo kinatafuta namna ya kukaa na hizo hela kwa muda mrefu Ili wazizalishe na wapige Faida ndefu kupitia benki ya CRDB ambao ni wabia wao wakuu (Mwanafunzi wa SAUT ni marufuku kufungua account nyingine tofauti na CRDB☹️).
Wanafunzi wanalazimishwa kujisajili kwa mfumo wa kuchukua hela kwa finger print(ambalo ni jambo zuri), lakini unaambiwa kila hela ikiingia mwanafunzi analazimika kukwatwa Sh 15000tsh,hii hela ukizidisha kwa idadi ya wanufaika wa mikopo hapo chuoni ni hela ndefu sana,ambayo nayo hugawanywa Kati ya chuo na benki husika.
Mimi ninasomesha mwanangu wa nne wa kiume hapo SAUT, course ya Electrical engineering mwaka wa kwanza, ila tangu apokee boom lake la kwanza mwezi wa 12,ambalo kimsingi alitakiwa alipokee mwezi wa 11, mpaka sasa unaelekea mwezi wa tatu hajapokea boom la pili ilihali vyuo vingine wanafunzi wamepewa tangu mwezi wa kwanza. Kimsingi sioni Sasa faida ya hio mikopo maana kama mzazi inanilazimu kutoka fedha ndefu tu Ili kumsaidia mwanangu ambae yupo mbali na nyumbani. Kimsingi sishindwi kumhudumia mwanangu, ila leo aliponipigia simu kuomba hela za matumizi, imenifanya nifikirie mengi sana juu ya huu ukiritimba unaofanywa na hiki chuo cha kipumbavu juu ya watoto.
👉🏿Hivi mtoto (tuchukulie wa kike) ambae anatokea familia masikini, anaesoma mbali kabisa na nyumbani kwao, asiekuwa na ndugu huko anaposomea, unapomcheleweshea fedha kwa muda mrefu hivyo(zaidi ya mwezi mmoja na nusu), unamtengenezea mazingira gani, kama sio kuandaa kizazi cha watoto wanaotegemea ngono Ili Kijikimu kimaisha? Na ndiomaana vyuo vingi vimekuwa vitovu vikubwa vya shuguli za ukahaba. Watoto wadogo hawana namna nyingine ya kujisaidia mwisho wanaangukia kwenye tabia za ajabu.
👉🏿Mwanafunzi anapata wapi muda wa kuweka mawazo yake kwenye masomo ikiwa mfukoni hata hela ya kula tu, hana?
Hili tatizo sijawahi kulisikia kabisa kwenye vyuo vingine isipokuwa SAUT,hii inaonyesha kuna ushenzi mkubwa sana hapo.Naanza kupata hata Wasiwasi juu ya kiwango cha elimu kinachopatika kwenye hicho chuo,huenda ni cha chini sana.
NB: Uongozi mzima wa ST. AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA badilikeni haraka iwezekanavyo, hiki mnachokifanya ni swala la kipumbavu sana. Yaani fedha zenyewe wanafunzi wanalewa kama mikopo, Ili baadae waulipe alafu tena upatikanaji wake unakuwa ni mpaka baadhi ya watu fulani wabembelezwe,huu ni upuuzi usiovumilika.