Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,667
- 149,839
Jumapili ya wiki iliyopita, mwanaharakati, Renatus Mkinga akiwa Star tv katika mjadala wa elimu, alikituhumu Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kwa kuanzisha kozi ya udaktari pasipo kuwa na walimu na badala yake alidai chuo hicho kinategemea kuchukua walimu kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili huku chenyewe kikiwa hakina walimu wa kufundisha kozi hiyo kitu ambacho si sahihi.
Kama ilivyokuwa wiki iliyopita,leo hii tena katika muendelezo wa mjadala huo wa elimu,bwana Mkinga amerudia tuhuma zake hizo kwa kumlaumu na kumshangaa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, Prof. Mukandala kwa kukubali jambo hili la kuanzisha kozi ya udaktari pasipokuwa na walimu na akaenda mbali kwa kuonya kuwa kuna hatari ya chuo hicho kuzalisha daktari ambae badala ya kuondoa appendix,yeye ataipasua.
Wahusika fuatilieni jambo hili na kama lipo mchukue hatua mapema kuepusha ya UDOM, St.Joseph, Kampala University na kwingineko.
Mliotazama kipindi hiki wilki iliyopita na asubuhi ya leo bila shaka mtakuwa mashahidi wazuri na zaidi mnaweza kuongeza yale mengine ya muhimu niliyosahau kuyaeleza hapa.