Tuhuma ya DPP kwa wabunge: Tutegemee nini kutoka kwa Spika?

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Hivi majuzi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Ndg Biswalo Mganga alitoa tuhuma kuwa baadhi ya wabunge wanapokea rushwa. Baada ya kali hii kutoka, nilitegemea Spika Ndugai amshukie DPP kwa kulidhalilisha bunge kutokana na kauli yake.

Kwa hakika kama ukipima kauli za CAG na DPP kuwa ni za udhalilishaji kwa kipimo ambapo kiwango cha chini ni 0 na kiwango cha juu ni `100 naona kauli ya CAG ni 5 na ya DPP ni 90 lakini sijasikia Spika akilipuka! Kulikoni?
 
Hivi majuzi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Ndg Biswalo Mganga alitoa tuhuma kuwa baadhi ya wabunge wanapokea rushwa. Baada ya kali hii kutoka, nilitegemea Spika Ndugai amshukie DPP kwa kulidhalilisha bunge kutokana na kauli yake. Kwa hakika kama ukipima kauli za CAG na DPP kuwa ni za udhalilishaji kwa kipimo ambapo kiwango cha chini ni 0 na kiwango cha juu ni `100 naona kauli ya CAG ni 5 na ya DPP ni 90 lakini sijasikia Spika akilipuka! Kulikoni?

embu nogeshea kidogo kwa kuweka ki video clip cha yule DPP anaeongea kishamba shamba 😊
 
Hivi majuzi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Ndg Biswalo Mganga alitoa tuhuma kuwa baadhi ya wabunge wanapokea rushwa. Baada ya kali hii kutoka, nilitegemea Spika Ndugai amshukie DPP kwa kulidhalilisha bunge kutokana na kauli yake. Kwa hakika kama ukipima kauli za CAG na DPP kuwa ni za udhalilishaji kwa kipimo ambapo kiwango cha chini ni 0 na kiwango cha juu ni `100 naona kauli ya CAG ni 5 na ya DPP ni 90 lakini sijasikia Spika akilipuka! Kulikoni?
Nadhani Kuna utofauti wa kauli Kati ya DPP na CAG
DPP yeye amewatuhumu wabunge mmoja mmoja na CAG yeye alilituhumu Bunge kwa ujumla wake
Nadhani hiyo tofauti yake.
 
Wabunge hasa members wa zile kamati uchwara wanakula rushwa vizuri tu. Kangeee Lugoola na wenzake waliwahi kupandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo. Nadhani Chama kiliingilia kati kuwanusuru
 
Hiyo kauli haishushi hadhi ya bunge kama taasisi bali hao wabunge walarushwa,kuna mapadre/wachungaji na mashehe wanabaka lakini makanisa/misikiti yanahadhi ya juu bado...
 
Kwani CAG na DPP wanafanana?

DPP ana mamlaka makubwa " kiuhalisia" kuliko Spika wa bunge!
ndiyo maana anaenda mwenyewe kwenye case ya dhahabu kule mwanza na kuongea na press kila baada ya case kuahirishwa hahahaa anaielekeza mahakama cha kufanya.
 
Kazi ya DPP ni nini sasa. Ameona au ameambiwa wabunge wanakula Rushwa ameshindwa kuwakamata kisha anapiga kelele.
Hii maana yake ameshindwa kazi. NI sawa na polisi ameona mwizi badala ya kumkamata mwizi anasema jamani watu wanaiba.

Kuna wakati viongozi wetu wanatia aibu. wanamkamata wadogo wakubwa wanweka loudspika jamani eee acheni kula rushwa
 
Back
Top Bottom