#COVID19 Tuhuma kuwa viongozi wa kitaifa hawakuchanja chanjo zikanushwe na ufafanuzi utolewe, zinapotosha na kutia hofu Wananchi

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Hizi tuhuma zinaenezwa sana kupitia mitandao ya kijamii. Hii mitandao ya kijamii ina nguvu sana maana ndio source of information.

Wanaoeneza hizi tuhuma wameenda mbali na kudai kuda hata hawa viongozi walipokuwa wakionyesha umma kuwa wanapata chanjo manesi waliowadunga chanjo hawakuvuta dawa na ilikuwa ni bosheni.

Hizi tuhuma sio nzuri maana zinawaaminisha wananchi kuwa viongozi wa kitaifa ni waongo na walifanya hivyo kuhadaa wananchi.

Zikanushwe haraka mara moja na ufafanuzi ufanyike.
 
Wangefafanua kuhusu suala la chanjo je n maamuzi ya mtu kupitia serikali au maamuzi ya serikali kupitia mtu.

Hawawezi kuepuka hizo propaganda za kuwa walichomwa hewa au maji ya kawaida.

Corona ni mradi wa kikundi cha watu fulani kwa ajili ya watu fulani.

Hivi vitu vinapangaliwa na wadau fulani tu.

Chanjo sio kinga ya kutopata maambukizi bali yaweza kuwa mwanya wa kusambaza maambukizi zaidi.

Hatua za kujikinga na korona kama kunawa na maji tiririka,matumizi ya barakoa panapo bidi hasa kwenye makusanyiko.
 
Video mbona inaonesha nesi alivuta chanjo na kumswab rais na kudunga sindano, nadhani hakuna anayelazimishwa, ila tusuburi iko siku tutaitafuta hiyo chanjo kwa gharama zetu.
 
wakati dunia inatikiswa na corona na maelfu wanakufa tanzania wala hatukuwa na habari japo hatukufunga mipaka wala nini, leo corona imepungua dunia eti ndo ionekane tishio kwetu.

je, huko awali nani alituokoa?
 
Kwamba wanajifanya wao kuchanjwa kumbe ni kuigiza tu ili watu waseme;

"...aah, kumbe chanjo haina shida mbona mpaka Rais na viongozi wengine wamechanjwa..."

Kama madai haya ni ya kweli, basi serikali (Rais Samia Suluhu na wenzake) watakuwa wamefanya very serious and grievous offense, kosa la uhaini, kosa la ugaidi wa kula njama za kuua raia wa Tanzania.

Adhabu ya kosa hili ni kifo tu.
 
Sumu aliyomwaga Askofu Rashid Gwajima siyo ya kitoto,yaani bila kutia chumvi ni kwamba hakuna kiongozi yoyote wa CCM na Serikali anayeitetea chanjo anaweza kuaminika kwa wananchi. Gwajima kaupiga mwingi sana.
Lazima hatua zichukuliwe.
 
Back
Top Bottom