Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Mkuu Yericko Nyerere, mlengo tata usiotimilika, unapimika kwa specified time frame iliyowekwa, kama hiyo time haija lapse, huwezi sema usiotimilika, subiria time lapse ndipo ulizungumzie hili!.

Kuhusu ndoto, ni kweli, naweza kuwa naota ndoto mchana kweupe macho wazi na kidole kwenye keyboard, nayo pia ni ndoto!.
Pasco.

"i joined them" tangu ulipoweka wazi hili... siwezi kuhangaika na wewe
 
Misukule mnaamini kila kitu anachosema Paroko! Hamtaki kusikia kitu mbadala hata kidogo! Kaazi kwelikweli! Ngojeni wenzenu wapige hela nyie mnanyweshwa viroba na maandamano ya kutosha tu! Ha ha ha! Chezea chadema saccos wewe!
Tatizo lenu nawaambia kila siku. Sio kila anayeunga mkono utndaji wa Chadema au CCMbasi ana njaa au mnywa viroba. Nina uhakika kuwa wewe hufikii hata kidogo mapato ya watumishi nilioajiri mimi binafsi. Hivyo suala la sijui viroba usinitajie. Tujadili hoja tuu.
 
Mkuu Mimi baba, honestly nimeipenda objectivity yako kwenye post yako. Post yako, ya 175 ndio ya kwanza kuchangiwa humu ki great mind, japo kuna great mind wengine walichangia ila sio sio ki great mind.

Tukio likitokea, simple mind watawazungumzia wafanya tukio, Mwigamba, Pasco, Mbowe, Dr. Slaa etc.
Ordinary mind, watazungumzia event, ya Mwigamba kusimamishwa, kutumia pen name kupost ukweli mchungu!,
Great Mind wataulizia "the motive behind" kama ulivyofanya hapa!.

Kama unamfahamu vizuri Mwigamba, unasoma makala zake, utakubaliana na mimi he is bold na very brave!. Ukumuona shujaa wa vita anaingia chini ya uvungu wa kitanda kumkimbia panya, simple mind atamzungumzia shujaa, ordinary mind atacheka kwa kitendo cha shujaa kuingia uvunguni, great mind ata find out the reasons behind shujaa huyu kuogopa panya!.

Nilipolisoma tuu bandiko lake humu jf na mtu yoyote genuine, atakubaliana na mimi Mwigamba amesema kweli tupu!. Kwa ushujaa alionao, unajiuliza what is his motive behind?!, why aogope panya mpaka kujigeuza maskini kulima!. Ndipo nikaelewa Mwigamba was a "caged bird", ndege tunduni!. Chadema should " let the caged bird sing" na kwa walio ndani ya Chadema, nadhani ni Prof. Mwesiga Beregu na ZZK tuu ndio wenye ujasiri huo!. Mimi sio Chadema na kama unadhani ni CCM pia your wrong!.

Kuna wrong notion kuwa kila anayeishambulia Chadema, haitakii mema!. Nimezisima hoja za Mwigamba they are truth!, isipokuwa hili la uchakachuaji katiba ndilo mimi nimelipick kulitafuti`a ukweli, japo limeisha kanusha kuwa ni uwongo na uzushi, bado nasubiria uthibitisho!.

Ukinisoma baadhi ya mabandiko yangu mengi ni kweli naishambulia sana Chadema, kuwa kama ni kweli, inataka Watanzania tuiaminie tuikabidhi nchi come 2015, its seriously needs to change tangu juzi na jana na leo ndio mwisho, kesho might be too little too late!.

Kutokana na wengi humu kuwa na mapenzi makubwa na Chadema, karibu wote mnachelea kuiambia ukwel;i na kubaki kuiimbia nyimbo za sifa na mapambia as if all is well. Angalau Mzee Mwanakijiji hujitahidi tahidi kiaina, mimi huwa sikopeshi, ndiye niliyeanzisha kuwambia JK ni dhaifu, nikawaambia CCM Wamechokwa, nikawaambia Chadema hawajajipanga. If you dig deep into my threads utagundua the motive behind, ni maslahi ya taifa na sio chuki dhidi ya Chadema!. Kuweza kunisoma in beyween the lines, nako kuna hitaji level fulani ya uelewa, naamini Dr. na wachache humu, wananielewa fikawanajua fika ninaulizia nini na my motive behind iko open!. 2015, nchi haiwezi kukabidhiwa kwa Chadema kwenye kikombe cha chai!, kwa mwendo huu Chadema inaokwenda nao, naiona kabisa jinsi nchi tunavyoikabidhi tena CCM huku sisi tusio na vyama tumejinyamazia tuu!. Nimeamua kujitolea kuwaambia loud and clear, ili ikifika 2015, niwakumbushe nilicho waambia!.

Pasco.

Kwa sasa nipo Uganda kwa assignment ya Monitoring and Evaluation ya Transport Sector kama Individual Global Consultant wa World Bank. Ni fani ya uongozi na tathmini ya utendaji.

Nimetanguliza hilo kwa sababu Watanzania wenzangu tumenyimwa "tools" za uchambuzi. Ipo sababu; nayo ni kuwa Uongozi Tanzania ni bahati nasibu kwa njia ya ulaghai. Kwa mfano tunachanganya ahadi za uchaguzi na sera za chama. Nakupa changamoto ebu chomoa sera moja tu ya chama cha mapinduzi niambie yafuatayo "Lengo la Kitaifa", "Mkakati wa Utelezaji mnaita Mpango Mkakati" "Utekelezaji wake kitaifa" "Rasili mali za kutekeleza" "Je kuna mfumo Mrejesho?" mwisho kuna interventions zo zote?

Katiba, UDOM ni baadhi ya mifano ambayo CCM wamekurupuka kwa sababu ya kubakia madarakani lakini kwa gharama ya taifa kuangamia. Maswali kuna wajibu na uabikaji hapo?

Turudi kwenye mada nakubaliana na baadhi ya hoja zako. Hoja ya kwanza ninayokubaliana nawe ni kuwa wewe si mwanachama wa chama cho chote. Nisichokubaliana na hiyo ni kuwa kwa hiyo unaweza kuyumbishwa tu kwa sababu hivi vyama vina kitu inaitwa Itikadi ambayo inachora mstari kuwa mwisho wa ninachokiamini ni hapa, vinginevyo sikubali. Kwa taarifa yako Mwigamba nikimu tathmini mnakaribiana, yupo ngazi ya juu ya uongozi wa CHADEMA lakini misingi ya CDM kiitikadi ambayo ndiyo inaandaa utendaji haiamini na hajui utaratibu wa uwasilishaji wa mawazo na utekelezaji wa chama. HUO NDIO UMAMLUKI kwa sababu mishipa ya fahamu zake haina usimamzi wa kiitikadi ya chama. Kifupi ni msaliti na ndiyo maana kuna mjadala huu.

Narudia kwenye dhamira yake kitaifa kiingereza tungesema "To pull down the CDM leadership and raze it" Kuuangusha uongozi wa CDM na kuuangamiza. Hilo kwa jinsi alivyofanya kwangu mimi pamoja kuwa naweza kuchambua nakuanika udhaifu wa taarifa yake msitari kwa msitari; kuna kitu kimoja ameshindwa kukiweka sawa. Kuwataka wanachama wa CDM wakubali mabadiriko ya lazima bila kutoa mbadala wa uwezekano wa ufikiaji wa anachokita; ni failure. Wanachama wana ngazi za maamuzi ambazo zinafika kwenye uongozi wa juu yeye akiwa mmoja wao. Kwangu mimi kibaya zaidi ni pale anapomhusisha Pasco (and the likes) kwenye mtandao ku"vent" frustration zake kweli najuta kuwa na kiongozi kama huyu.

Ok tukubali kwamba katiba ya CDM imechakachuliwa na "viongozi", wewe unatafuta ushahidi hutaupata kwa sababu haupo; lakini kwa nini mamlaka husika hazijaliona hili? Ni kwa sababu au niwazembe au kwa sababu hakuna kasoro.

Mimi naipenda CHADEMA labda kwa sababu nipo Arusha lakini zaidi ni kwa sababu nakubaliana na katiba na utekelezakji wa katiba. Sina cheo na sitaki cheo na sijawahi kufikiria kutafuta cheo kwa sababu fursa niliyo nayo ya kutekeleza yale ya kitaifa kutokana na chama hiki inatosha na nikitathmini naweza nikaianisha mafanikio. Ndiyo maana kamwe sitasuta mwanachama au chama cha CCM kwa sababu kina katiba, itikadi na utendaji ambao hainivutii.

Pamoja na heshima yote, uwe na chama usiwe nacho ebu uamini angalau kuwa CCM inakukuna na utajitahidi kutoa mchango wako bila kuisaliti. Hivyo amini kuwa kama mwigamba kwa ngazi aliyokuwa nayo kutokana na katiba hadi hapa, na imani kwa itkadi ya chama hangeishiwa hekima ya kufikisha ujumbe wake wenye kuzaa matunda Kwa sasa Mwigamba ni fursa iliyopotea; na CDM imesaidiwa sana kwa msaliti mwingine muhimu kujiengua mwenyewe. Mtandao wake ni mkubwa ndani ya chama usishangae ataondoka na wengi wa aina yake. Kama mpenzi wa CDM na waondoke tu kwa sababu sio wao wamejisaliti bali Mungu amewaangaza.
 
Wanabodi,

Uendeshaji wa vyama vya siasa nchini, unaongozwa na sheria, taratibu na kanuni. Ikithibitika pasipo shaka kuwa chama fulani, kinakiuka sheria, taratibu na kanuni, kinapaswa kuwajibishwa, kuadhibiwa hata kufutwa, kutegemeana na tuhuma halisi!.

Miongoni mwa masharti ya usajili wa vyama vya siasa, ni kwa vyama hivyo, kuwasilisha katiba yake iliyopitishwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, ikithibitika pasipo shaka kuwa katiba ya Chadema iliyowasilishwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni Katiba "Fake" na sio ile katiba halisi ilipitishwa na Vikao Halali vya Chadema!, hili ni kosa kubwa linaweza kupelekea chama kufutwa!.

Tuhuma yenyewe ni hii na ilitolewa rasmi jana humu jf na mwana jf huyu.

Mara baada ya mwajf huyu kuzishusha tuhuma hizi humu, uongozi wa Chadema umemsimamisha mmoja wa viongozi wake kwa kosa la kuutoa ukweli huu nje!.

Maswali ambayo ni lazima Chadema wayajibu ni haya!.

  • Jee ni kweli Chadema inaendeshwa kwa katiba fake na sio ile iliyopitishwa na vikao halali?!.
  • Jee ni nani alikinyofoa kipengele cha demokrasia ya ukomo wa uongozi ndani ya chama ili kutoa nafasi kwa uongozi wa kifalme na kisultani?.
  • Ikithibitika kuna mtu alikinyofoa kipengele hicho kwa makusudi, atachukuliwa hatua gani?.
  • Je mabadiliko ya "unyofoaji huo" yaliwasilishwa kwa Msajili wa Vyama?.
  • Ikithibitika pasipo shaka kuwa Chadema walikiuka sheria taratibu na kanuni, jee watafanywa nini? (Masajili)
Baada ya kushushwa tuhuma nzito kama hizi, dawa sio kumsimamisha uongozi mtoa tuhuma, bali kutoa majibu ya kina kuhusiana na tuhuma hizi.

Namna rahisi ya kuthibitisha ni kupatikana kwa miniti za kikao kilichopitisha kipengele hicho cha ikomo wa uongozi.
Kisha zipatikane miniti za kikao chochote halali kilichopitisha unyofoaji huo!.

Kisha kwenda kwa Msajili kuthibitisha mabadiliko hayo yalifanyika.

Naandika haya nikiwa ni mwananchi tuu wa kawaida asiye mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali mwenye mamlaka kamili kuhoji jambo lolote kuhusu chama chochote, na sababu ni mimi pia ndiye ninayegharimia fedha za uendesha wa Chadema kupitia kodi yangu inayolipwa Chadema kama ruzuku!.

Pia naelewa fika kinachowakuta wakosoaji wowote wa chama "kitakatifu" humu jf, ila kwa vile hoja zangu ni za kweli, nasimama kwenye kweli, na ni ukweli tuu ndio utakao kiweka huru Chadema na sio timua timua au fukuza fukuza!.

Angalizo wa wapenzi wa Chadema, sijasema chama chenu kinafutwa, nimetoa tuhuma, ambazo zikithibitishwa, Chadema mtaadhibiwa!.

Pasco.

Mkuu Dr. W. Slaa, kwanza, heshima yako!, maana ile kujibiwa tuu na mtu wa calibre yako pekee, ni heshima kwangu na kwa thread hii, hivyo majibu yako, nayaunganisha pale mbele ya thread as an authority.

Uwongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli. Sambamba na tuhuma hii, mtoa tuhuma pia ameweka tuhuma nyingine nyingi, zenye kuhitaji majibu ya kina kama haya uliyonijibu hapa.

Kwa vile CCM ndicho chama tawala, Chadema kiko kwenye mizani ya tukiaminie mwaka 2015 au bora kuendelea na CCM tuliyoizoea!, hivyo haya makando kando yoyote kuihusu Chadema, lazima yajibiwe ipasavyo kama hivi ulivyofanya hapa.

Asante sana kwa hili.

Kwa vile maelezo haya yako ni ya upande mmoja, nasubiri verification ya data toka kwa msajili, then niufunge rasmi huu mjadala.

Nashukuru tena.

Pasco.

Pasco nimesoma mjadala ulioanzisha na majibu ya Dr Slaa. Kabla ya kusoma mjadala huu, niliitikia mwito wa Mtoi kwenye Jukwaa la Wanamabadiliko na nikaandika kwa kirefu kuhusu suala hili ambalo mimi nilishiriki kwa karibu sana nikiwa sehemu ya timu zote tatu zilizohusika na mchakato wa kukusanya maoni ya wanachama kwa ajili ya kuandika katiba, kanuni, itifaki na maadili ya chama pamoja na miongozo ya mabaraza ya chama. Naomba Mods muuweke waraka huo ambao nitawatumia kwa barua pepe au mnaweza kuuchukua kutoka huko. Nimekubaliana na katibu mkuu kuna marekebisho kwenye majibu yake ya awali, katiba ya mwaka 2004 iliondolewe katika orodha ya katiba alizozitaja. Suala la kwamba kuna kipengele kiliondolewa kinyemela halina ukweli, na kilichofanyika 2006 ni kuandika katiba upya kama ambavyo nimeeleza kwenye majibu hayo. Baada ya majibu hayo kusomwa, kama kuna masuala yanahitaji ufafanuzi wa kichama kuhusu suala hili la katiba na mengine au maoni yangu binafsi nitafanya hivyo leo kati ya saa 9 mpaka 10 Jioni. Niko kwenye kikao, baada ya hapo nitakuwa kwenye mkutano. Nikihitajika baadae nitarejea tena. Mjadala mwema. JJ
 
Ok tukubali kwamba katiba ya CDM imechakachuliwa na "viongozi", wewe unatafuta ushahidi hutaupata kwa sababu haupo; lakini kwa nini mamlaka husika hazijaliona hili? Ni kwa sababu au niwazembe au kwa sababu hakuna kasoro.
Katiba ni mali ya chama husika na sio mali ya mamlaka husika!. Baada ya chama husika, kuitunga katiba yake na kuipitisha kwenye mkutano mkuu wake, huipeleka kwa Msajili wa vyama vya siasa, ili isajiliwe, kazi ya msajili sio kuiingilia katiba bali kuhakikisha haiendi kinyume cha masharti, malengo na katiba ya nchi.

Chadema ilipeleka katiba fulani mwaka 2004 ambayo mpaka sasa sijafanikiwa kuipata. Ndani ya katiba hiyo, inadaiwa kulikuwa na kipengele cha ukomo wa uongozi kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Mwaka 2006 wakafanya mabadiliko ya katiba yao kihalali kabisa, katika mkutano huo mkuu, walifanya marekebisho mengi, ila kati ya marekebisho hayo yote, kifungu cha ukomo wa uongozi, hakikujadiliwa wala kufanyiwa mabadiliko yoyote!, lakini katiba iliyopelekwa kusajiliwa kwa msajili, ikawa imenyofolewa kifungu hicho kinyemela!.

Kama ni kweli, katiba ya 2004, kipengele hicho kilikuwepo, na wamefanya mabadiliko ya kukiondoa rasmi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, then its ok!. Lakini kama ni kweli kifungu hicho kilikuwepo, mabadiliko ya kifungu hicho hayakuletwa kwenye mkutano mkuu kujadiliwa, wala kubadilishwa, then all over a sudden, kikanyofolewa kinyemela, then katiba hiyo ya 2006 is "fake" kwa sababu kwa mujibu wa muundo wa Chadema, hakuna kikao chochote chenye mamlaka ya kunyofoa kifungu cha katiba bila bila mkutano mkuu kujadili na kuridhia!.

Kinachosubiriwa hapa ni kuipata tuu hiyo katiba ya 2004 kuudhibitisha uongo wa Mwigamba.

Pamoja na heshima yote, uwe na chama usiwe nacho ebu uamini angalau kuwa CCM inakukuna na utajitahidi kutoa mchango wako bila kuisaliti.
Hili la CCM kunikuna nalo neno!, hebu unisome hapa jinsi ninavyoisifia CCM, kama uthibitisho huku ndiko kukunwa kwenyewe,

CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!
Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015 ...
Mapungufu ya JK: Ni Rais Daifu"-Weak President!.

Ila tatizo langu kubwa mimi ni realist, sio dreamer wala wishful thinker wa I wish, this and that, ukiwa realist, unaukubali ukweli jinsi ulivyo, kwa mwendo huu Chadema inaokwenda nao, uchaguzi wa 2015, naiona CCM ikirudi madarakani kwa ulaini kwa sababu Chadema is not doing the right thing, na hata pale inapofanya the the right thing, it doesn't do it right! na mkiambiwa mnakuja juu!.
Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Pasco.
 
Pasco nimesoma mjadala ulioanzisha na majibu ya Dr Slaa. Kabla ya kusoma mjadala huu, niliitikia mwito wa Mtoi kwenye Jukwaa la Wanamabadiliko na nikaandika kwa kirefu kuhusu suala hili ambalo mimi nilishiriki kwa karibu sana nikiwa sehemu ya timu zote tatu zilizohusika na mchakato wa kukusanya maoni ya wanachama kwa ajili ya kuandika katiba, kanuni, itifaki na maadili ya chama pamoja na miongozo ya mabaraza ya chama. Naomba Mods muuweke waraka huo ambao nitawatumia kwa barua pepe au mnaweza kuuchukua kutoka huko. Nimekubaliana na katibu mkuu kuna marekebisho kwenye majibu yake ya awali, katiba ya mwaka 2004 iliondolewe katika orodha ya katiba alizozitaja. Suala la kwamba kuna kipengele kiliondolewa kinyemela halina ukweli, na kilichofanyika 2006 ni kuandika katiba upya kama ambavyo nimeeleza kwenye majibu hayo. Baada ya majibu hayo kusomwa, kama kuna masuala yanahitaji ufafanuzi wa kichama kuhusu suala hili la katiba na mengine au maoni yangu binafsi nitafanya hivyo leo kati ya saa 9 mpaka 10 Jioni. Niko kwenye kikao, baada ya hapo nitakuwa kwenye mkutano. Nikihitajika baadae nitarejea tena. Mjadala mwema. JJ
Asante sana JJ. Mnyika, nitajitahidi kutembelea kule ili kujiridhisha, ila kwa vile mzizi wa fitna kwenye uzi huu ni katiba ya 2004, kama unayo, nitashukuru tukiipata, tukaufunga huu mjadala rasmi.

Kama unachosema wewe ndio right, kuwa ile katiba ya 2006 sio marekebisho ya katiba ya 2004, bali ni katiba mpya, hata kama ni kweli, katiba ya 2004 ilikuwa na kipengele tajwa, na katiba ya 2006 ikawa haina, then at this juncture, I put my hands down, mjadala umekwisha, kwa sababu katiba ya 2006 ni mpya, na kwa vile ni kitu kipya, then its ok kama haina kipengele hicho!. Hii inamaanisha hata ikipatikana hiyo katiba ya 2004, its immaterial, ila for interest, bado naitafuta hiyo Katiba ya 2004, "kuona ni kuamini.

Pasco.
 
Katiba ni mali ya chama husika na sio mali ya mamlaka husika!. Baada ya chama husika, kuitunga katiba yake na kuipitisha kwenye mkutano mkuu wake, huipeleka kwa Msajili wa vyama vya siasa, ili isajiliwe, kazi ya msajili sio kuiingilia katiba bali kuhakikisha haiendi kinyume cha masharti, malengo na katiba ya nchi.

Chadema ilipeleka katiba fulani mwaka 2004 ambayo mpaka sasa sijafanikiwa kuipata. Ndani ya katiba hiyo, inadaiwa kulikuwa na kipengele cha ukomo wa uongozi kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Mwaka 2006 wakafanya mabadiliko ya katiba yao kihalali kabisa, katika mkutano huo mkuu, walifanya marekebisho mengi, ila kati ya marekebisho hayo yote, kifungu cha ukomo wa uongozi, hakikujadiliwa wala kufanyiwa mabadiliko yoyote!, lakini katiba iliyopelekwa kusajiliwa kwa msajili, ikawa imenyofolewa kifungu hicho kinyemela!.

Kama ni kweli, katiba ya 2004, kipengele hicho kilikuwepo, na wamefanya mabadiliko ya kukiondoa rasmi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, then its ok!. Lakini kama ni kweli kifungu hicho kilikuwepo, mabadiliko ya kifungu hicho hayakuletwa kwenye mkutano mkuu kujadiliwa, wala kubadilishwa, then all over a sudden, kikanyofolewa kinyemela, then katiba hiyo ya 2006 is "fake" kwa sababu kwa mujibu wa muundo wa Chadema, hakuna kikao chochote chenye mamlaka ya kunyofoa kifungu cha katiba bila bila mkutano mkuu kujadili na kuridhia!.

Kinachosubiriwa hapa ni kuipata tuu hiyo katiba ya 2004 kuudhibitisha uongo wa Mwigamba.

.
Pasco, Pamoja na marekebisho niliyoeleza kuhusu majibu ya Dr Slaa kwamba katiba ya 2004 iondolewe kwenye orodha kama nilivyochangia hapo awali. Katiba ya mwaka 2004 haiwezi kuwa ushahidi wa hayo madai yasiyokuwa ya kweli. Katiba ya mwaka 2004 mimi ninayo hapa nilipo, kwenye kifungu cha 6.3.2 kina kipengele cha 'muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja'. Hata hivyo, huu sio ushahidi wa kwamba kipengele hiki kimeondolewa 'kinyemela'. Hii ni kwa sababu tatu; Mosi, 2006 hatukuwa tunafanya marekebisho ya katiba kwa maana ya kuondoa au kuacha kifungu cha katiba ya mwaka 2004. Tuliandika katiba upya, ndio maana tarehe 13 Agosti 2006 pale PTA tukafanya uzinduzi wa katiba mpya ya CHADEMA. Kwenye mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya na hatimaye maandalizi ya rasimu ya katiba mpya, hili suala halikuingia kabisa. Halikupitishwa kwenye mapendekezo ya sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na hata mkutano mkuu kwa kadiri ya kumbukumbu zangu. Hivyo huwezi kuzungumzia 'kuondoa kinyemela' kipengele ambacho hakikuingia. Pili, ushahidi wa jambo hili kuwa kimeondolewa kinyemela ni kuleta hapa rasimu ya katiba kama ilivyopitishwa na kupelekwa kwa msajili, katiba mpya ya 2006 (Dr Slaa amekupa changamoto ya kwenda kukagua) au kumbukumbu za mkutano mkuu husika au toleo la kwanza la katiba ya mwaka 2006 ambalo wanachama wanalo nakala zake. Uonyeshe kwamba kifungu kilikuwa hivi sasa kinyemela kikaondolewa vile. Imewekwa humu katiba ya mwaka 2006, haina hicho kipengele cha ukomo. Tatu, kama suala hili lingekuwa hivi kwa ukubwa wake na katiba imetumika toka mwaka 2006 kwenye chaguzi za ndani za marudio maeneo mbalimbali, uchaguzi mkuu wa mwaka 2009 wa ndani ya chama nchi nzima lingeshaibuka kwa maana ya watu kuwawekea pingamizi waliokaa vipindi viwili au kulalamikia kifungu hicho kuondolewa. Haijaibuka kwenye chaguzi zote za marudio za ndani 2012 na hata kwenye uchaguzi mkuu wa ndani ya chama ulioanza nchi nzima toka mapema mwaka 2013, linaibuka sasa kuelekea uchaguzi mkuu wa taifa mapema mwaka 2013. Kuna maswali ya kujiuliza. Kuna tofauti kati ya kutoa maoni ya kutaka marekebisho kifungu hicho kiwepo na kutoa madai kwamba kiliondolewa kinyemela. Hoja hii watuhimiwa wa kwanza hawawezi kuwa Mbowe na Dr Slaa walioendesha vikao vya maamuzi, watuhumiwa wakuu tutakuwa kamati tulizohusika na suala la katiba mpya ya ndani ya chama ambayo upande mmoja ni mimi na Profesa Baregu kwa upande wa kurasa za falsafa na itikadi na upande mwingine ni muasisi wa chama Mzee Kimesera, Mkurugenzi Benson Kigaila na mimi kwa upande wa maeneo mengine ya kwenye katiba. Majibu niliyotoa Jukwaa la Wanamabadiliko yana maelezo ya ziada. JJ
 
Mkuu Samson Moses, katiba za vyama ni mali za vyama, hata ikitamka kiongozi ni kipindi chote cha uhai mpake afe, msajili atairidhia!.

Hoja yangu ni kuwa ku na katiba ya Chadema ya 2004 inadaiwa iliweka bayana muda wa uongozi ni vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Hii ndio katiba halali, kisha chama kina haki ya kuibadili wakati wowote ila mabadiliko haya yaliza yapitie process ya kichama na kuwasilishwa kwa msajili, ukishawasilisha katiba mpya, ile ya zamani inabatilishwa automatically.

Hoja ya Mwigamba ni kuwa katika kupitisha katiba mpya ya Chadema ya 2006, kuna kipengele cha ukomo, kilinyofolewa kinyemela, hivyo katiba iliyopelekwa haina kipengele hicho!.

Kitendo cha kufanya mabadiliko ya katiba, bila kukizungumzia kipengele fulani, au kukifuta rasmi na badala yake kukichomoa kinyemela, ndiko kunakopelekea, katiba hiyo kuwa fake!.

Bado naisubiria katiba ya Chadema ya 2004 ili kulithibitisha hili!.

Pasco.

Mkuu Pasco,si Samson Mosses bali ni Sammosses naomba nirekebishe hapo kidogo,kama Mwigamba amesema katiba ilinyofolewa kipengele cha ukomo kabla ya kupelekwa kwa mlezi wa vyama yaani Msajili wa vyama vya siasa nchini angethibitisha na kutoa kauli hiyo ndani ya vikao halali kwa kuwakilisha katiba iliyokubaliwa na ikiwa na ukomo ikiambatanishwa na katiba iliyochakachuliwa ili ukweli ujulikane.Lakini kama kinachotafutwa ni fitina basi fitina imemgeuka.

Chokochoko ni nyingi sana ambazo kama hazitafanyiwa umakini katika kuzitafutia uvumbuzi juhudi zote za kukiimarisha chama zitakuwa zinagonga mwamba.Mamluki wa siasa wapo ambao wamegeuka kuwa malaya wa kisiasa,ni bora kuondoa mwiba ulio ndani ya mguu kulio kusubiri mguu kuota tende.

Lakini kama kuna ukweli wowote ule uliofanywa kwa mujibu wa Mwigamba wote waliohusika wanastahili wasisubiri chama kuwawajibisha maana kama kweli tumeamua wote kuwa katiba tunataka iwe hivi nyuma ya pazia watu wengine wanageuka maana yake nini?tunapoteza umakini katika kusimamia ukweli na haki itakiwayo.
 
Mimi leo niko taaban baada ya mbio za OCEAN ROAD CANCER leo asubuhi. nikasema nijinyooshe nikiamka nitakuta katiba ya 2004 iliyoombwa lakini hakuna kitu.

JJ hebu lete hiyo katiba humu watu tupumzike. How hard is it ku attach hiyo katiba?
 
Pasco, Pamoja na marekebisho niliyoeleza kuhusu majibu ya Dr Slaa kwamba katiba ya 2004 iondolewe kwenye orodha kama nilivyochangia hapo awali. Katiba ya mwaka 2004 haiwezi kuwa ushahidi wa hayo madai yasiyokuwa ya kweli. Katiba ya mwaka 2004 mimi ninayo hapa nilipo, kwenye kifungu cha 6.3.2 kina kipengele cha 'muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja'. Hata hivyo, huu sio ushahidi wa kwamba kipengele hiki kimeondolewa 'kinyemela'. Hii ni kwa sababu tatu; Mosi, 2006 hatukuwa tunafanya marekebisho ya katiba kwa maana ya kuondoa au kuacha kifungu cha katiba ya mwaka 2004. Tuliandika katiba upya, ndio maana tarehe 13 Agosti 2006 pale PTA tukafanya uzinduzi wa katiba mpya ya CHADEMA. Kwenye mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya na hatimaye maandalizi ya rasimu ya katiba mpya, hili suala halikuingia kabisa. Halikupitishwa kwenye mapendekezo ya sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na hata mkutano mkuu kwa kadiri ya kumbukumbu zangu. Hivyo huwezi kuzungumzia 'kuondoa kinyemela' kipengele ambacho hakikuingia. Pili, ushahidi wa jambo hili kuwa kimeondolewa kinyemela ni kuleta hapa rasimu ya katiba kama ilivyopitishwa na kupelekwa kwa msajili, katiba mpya ya 2006 (Dr Slaa amekupa changamoto ya kwenda kukagua) au kumbukumbu za mkutano mkuu husika au toleo la kwanza la katiba ya mwaka 2006 ambalo wanachama wanalo nakala zake. Uonyeshe kwamba kifungu kilikuwa hivi sasa kinyemela kikaondolewa vile. Imewekwa humu katiba ya mwaka 2006, haina hicho kipengele cha ukomo. Tatu, kama suala hili lingekuwa hivi kwa ukubwa wake na katiba imetumika toka mwaka 2006 kwenye chaguzi za ndani za marudio maeneo mbalimbali, uchaguzi mkuu wa mwaka 2009 wa ndani ya chama nchi nzima lingeshaibuka kwa maana ya watu kuwawekea pingamizi waliokaa vipindi viwili au kulalamikia kifungu hicho kuondolewa. Haijaibuka kwenye chaguzi zote za marudio za ndani 2012 na hata kwenye uchaguzi mkuu wa ndani ya chama ulioanza nchi nzima toka mapema mwaka 2013, linaibuka sasa kuelekea uchaguzi mkuu wa taifa mapema mwaka 2013. Kuna maswali ya kujiuliza. Kuna tofauti kati ya kutoa maoni ya kutaka marekebisho kifungu hicho kiwepo na kutoa madai kwamba kiliondolewa kinyemela. Hoja hii watuhimiwa wa kwanza hawawezi kuwa Mbowe na Dr Slaa walioendesha vikao vya maamuzi, watuhumiwa wakuu tutakuwa kamati tulizohusika na suala la katiba mpya ya ndani ya chama ambayo upande mmoja ni mimi na Profesa Baregu kwa upande wa kurasa za falsafa na itikadi na upande mwingine ni muasisi wa chama Mzee Kimesera, Mkurugenzi Benson Kigaila na mimi kwa upande wa maeneo mengine ya kwenye katiba. Majibu niliyotoa Jukwaa la Wanamabadiliko yana maelezo ya ziada. JJ
Mkuu JJ. Mnyika, hoja zako zimeufunga rasmi huu mjadala, kiukweli nimemuelewa vizuri sana Mwingamba, ingawa ni kweli he is wrong kuwa kipengele hicho kimeondolewa kinyemela, he was very right kuwa kilikuwepo kwenye katiba ya 2004, na kwa vile kilikuwepo by specific intentions, na kwenye katiba ya 2006 hakikuletwa kabisa, kitendo cha ule mkutano wenu mkuu kutokukisoma na kukipitisha, kulitafsiriwa na Mwingamba ndio kunyofolewa kwenyewe kinyemela!.

Nakubaliana na wewe, 100%, kuwa kama katiba ya 2006 ni mpya na sio marekebisho, mko right, Mwigamba is wrong!.

Mimi sio mwanachama wenu ni raia tuu wa Tanzania, nawaombeni sana, mkae chini, Mwigamba sio wa kupuuzwa, mzipangue tuhuma za Mwigamba moja baada ya nyingine!, msiendeleze ule mtindo wa kufukuzana bila kufuata taratibu na kanuni zenu kama mlivyowafanya kina Shonza, fuateni taratibu, ili kuendeleza imani kuwa kweli Chadema ni chama makini.

nakuomba nitumie scanned copy ya hicho kipengele, mjadala umefungwa.

Asate tena,

Pasco.
 
Katiba ni mali ya chama husika na sio mali ya mamlaka husika!. Baada ya chama husika, kuitunga katiba yake na kuipitisha kwenye mkutano mkuu wake, huipeleka kwa Msajili wa vyama vya siasa, ili isajiliwe, kazi ya msajili sio kuiingilia katiba bali kuhakikisha haiendi kinyume cha masharti, malengo na katiba ya nchi.

Chadema ilipeleka katiba fulani mwaka 2004 ambayo mpaka sasa sijafanikiwa kuipata. Ndani ya katiba hiyo, inadaiwa kulikuwa na kipengele cha ukomo wa uongozi kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Mwaka 2006 wakafanya mabadiliko ya katiba yao kihalali kabisa, katika mkutano huo mkuu, walifanya marekebisho mengi, ila kati ya marekebisho hayo yote, kifungu cha ukomo wa uongozi, hakikujadiliwa wala kufanyiwa mabadiliko yoyote!, lakini katiba iliyopelekwa kusajiliwa kwa msajili, ikawa imenyofolewa kifungu hicho kinyemela!.

Kama ni kweli, katiba ya 2004, kipengele hicho kilikuwepo, na wamefanya mabadiliko ya kukiondoa rasmi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, then its ok!. Lakini kama ni kweli kifungu hicho kilikuwepo, mabadiliko ya kifungu hicho hayakuletwa kwenye mkutano mkuu kujadiliwa, wala kubadilishwa, then all over a sudden, kikanyofolewa kinyemela, then katiba hiyo ya 2006 is "fake" kwa sababu kwa mujibu wa muundo wa Chadema, hakuna kikao chochote chenye mamlaka ya kunyofoa kifungu cha katiba bila bila mkutano mkuu kujadili na kuridhia!.

Kinachosubiriwa hapa ni kuipata tuu hiyo katiba ya 2004 kuudhibitisha uongo wa Mwigamba.

Hili la CCM kunikuna nalo neno!, hebu unisome hapa jinsi ninavyoisifia CCM, kama uthibitisho huku ndiko kukunwa kwenyewe,

CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!
Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
Yametimia!, CCM Imechokwa!, Chadema Njia Nyeupe 2015 ...
Mapungufu ya JK: Ni Rais Daifu"-Weak President!.

Ila tatizo langu kubwa mimi ni realist, sio dreamer wala wishful thinker wa I wish, this and that, ukiwa realist, unaukubali ukweli jinsi ulivyo, kwa mwendo huu Chadema inaokwenda nao, uchaguzi wa 2015, naiona CCM ikirudi madarakani kwa ulaini kwa sababu Chadema is not doing the right thing, na hata pale inapofanya the the right thing, it doesn't do it right! na mkiambiwa mnakuja juu!.
Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If ...
Pasco.

Mkuu naona umepata majibu ya authority za CHADEMA i.e JJ. Mimi bado nina wewe tuache utani wewe unaipenda CCM ambayo si dhambi. Hizo nukuu ulizoweka nilizisoma baadhi nilizijibu. Labda mjadala sasa ubadirike kwa sababu mwenzangu wewe ni mwanasheria tujiulize NAFASI YA KATIBA ZA VYAMA TUNAPOELEKEA KWENYE KATIBA YA NCHI KUNA UTAIFA KIASI GANI?

Dondoo

1. Utekelezaji wa sera ya mali asili

2. Tunu za Taifa

3. Demokrasia na haki za kibinadamu

4. Maadili ya Uongozi

5. Haki ya huduma za kijamii

6. Haki za kibinadamu na Msaada wa Kisheria

7. Sera ya Mambo ya nje

8. Ongezea

Mimi naona haziko exhaustive kwa vyama vote, kwa sababu Katiba ya Kitaifa haipo na haiwadai wadau yaani vyama vya kisiasa kuzingatia hayo. Niliyoyaainisha hapo juu ni kuwa kukiwepo mabadiriko ya chama tawala kuna mambo ya kitaifa hayatakiwi kubadirika
 
website ya Chadema imefungwa kwa wasio members. Hivyo hatuwezi kuipata hiyo katiba

Tazama hapa:

attachment.php

Democracy at work....
 
Mkuu naona umepata majibu ya authority za CHADEMA i.e JJ. Mimi bado nina wewe tuache utani wewe unaipenda CCM ambayo si dhambi. Hizo nukuu ulizoweka nilizisoma baadhi nilizijibu. Labda mjadala sasa ubadirike kwa sababu mwenzangu wewe ni mwanasheria tujiulize NAFASI YA KATIBA ZA VYAMA TUNAPOELEKEA KWENYE KATIBA YA NCHI KUNA UTAIFA KIASI GANI?

Dondoo

1. Utekelezaji wa sera ya mali asili

2. Tunu za Taifa

3. Demokrasia na haki za kibinadamu

4. Maadili ya Uongozi

5. Haki ya huduma za kijamii

6. Haki za kibinadamu na Msaada wa Kisheria

7. Sera ya Mambo ya nje

8. Ongezea

Mimi naona haziko exhaustive kwa vyama vote, kwa sababu Katiba ya Kitaifa haipo na haiwadai wadau yaani vyama vya kisiasa kuzingatia hayo. Niliyoyaainisha hapo juu ni kuwa kukiwepo mabadiriko ya chama tawala kuna mambo ya kitaifa hayatakiwi kubadirika

Naomba scanned copy ya Katiba ya chadema ya 2004 please
 
Dr. W. Slaa, nimekuona upo online, kwenye majibu yako na JJ.Mnyika, mmetofautiana kidogo kuhusu kipengele hicho chenye utata, wewe umesema hakijawahi kuwepo kabisa, Mnyika amesema kilikuwepo kwenye katiba ya 2004 ila ya 2006 hakikuletwa.

As a mater of interest, unaweza kunijulisha tuu kwa kifupi original intention ya kukiweka hapo mwanzo, ili ku justify ni kwa nini hakikurudishwa kwenye katiba ya 2006 hivyo kuifuta kabisa dhana ya kunyofolewa kinyemela?.

Pasco.
 
Mkuu naona umepata majibu ya authority za CHADEMA i.e JJ. Mimi bado nina wewe tuache utani wewe unaipenda CCM ambayo si dhambi. Hizo nukuu ulizoweka nilizisoma baadhi nilizijibu.
Mkuu Mimibaba, ni kweli majibu haya ya authority yamefunga mjadala, natumaini umenote tofauti ya majibu ya JJ.Mnyika na Dr. Slaa kuhusu kipengele husika, mjadala umefungwa ila bado naitafuta hiyo katiba ya Chadema ya 2004, kuona ni kuamini!.

Hili la katiba tulitafutie muda muafaka.

Pasco.
 
pasco naomba ukocpy hii image ya yaliyotusibu tulipokwenda kwenye website ya CAHDEMA kutazama hiyo copy ya katiba kisha iweke kwenye majumuisho yako kwenye first thread.

attachment.php

Mimi bado naendelea na swali langu hiyo scanned copy ya katiba ya 2004 iko wapi?
 
Wanabodi,

Uendeshaji wa vyama vya siasa nchini, unaongozwa na sheria, taratibu na kanuni. Ikithibitika pasipo shaka kuwa chama fulani, kinakiuka sheria, taratibu na kanuni, kinapaswa kuwajibishwa, kuadhibiwa hata kufutwa, kutegemeana na tuhuma halisi!.

Miongoni mwa masharti ya usajili wa vyama vya siasa, ni kwa vyama hivyo, kuwasilisha katiba yake iliyopitishwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, ikithibitika pasipo shaka kuwa katiba ya Chadema iliyowasilishwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni Katiba "Fake" na sio ile katiba halisi ilipitishwa na Vikao Halali vya Chadema!, hili ni kosa kubwa linaweza kupelekea chama kufutwa!.

Tuhuma yenyewe ni hii na ilitolewa rasmi jana humu jf na mwana jf huyu.

Mara baada ya mwajf huyu kuzishusha tuhuma hizi humu, uongozi wa Chadema umemsimamisha mmoja wa viongozi wake kwa kosa la kuutoa ukweli huu nje!.

Maswali ambayo ni lazima Chadema wayajibu ni haya!.

  • Jee ni kweli Chadema inaendeshwa kwa katiba fake na sio ile iliyopitishwa na vikao halali?!.
  • Jee ni nani alikinyofoa kipengele cha demokrasia ya ukomo wa uongozi ndani ya chama ili kutoa nafasi kwa uongozi wa kifalme na kisultani?.
  • Ikithibitika kuna mtu alikinyofoa kipengele hicho kwa makusudi, atachukuliwa hatua gani?.
  • Je mabadiliko ya "unyofoaji huo" yaliwasilishwa kwa Msajili wa Vyama?.
  • Ikithibitika pasipo shaka kuwa Chadema walikiuka sheria taratibu na kanuni, jee watafanywa nini? (Masajili)
Baada ya kushushwa tuhuma nzito kama hizi, dawa sio kumsimamisha uongozi mtoa tuhuma, bali kutoa majibu ya kina kuhusiana na tuhuma hizi.

Namna rahisi ya kuthibitisha ni kupatikana kwa miniti za kikao kilichopitisha kipengele hicho cha ikomo wa uongozi.
Kisha zipatikane miniti za kikao chochote halali kilichopitisha unyofoaji huo!.

Kisha kwenda kwa Msajili kuthibitisha mabadiliko hayo yalifanyika.

Naandika haya nikiwa ni mwananchi tuu wa kawaida asiye mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali mwenye mamlaka kamili kuhoji jambo lolote kuhusu chama chochote, na sababu ni mimi pia ndiye ninayegharimia fedha za uendesha wa Chadema kupitia kodi yangu inayolipwa Chadema kama ruzuku!.

Pia naelewa fika kinachowakuta wakosoaji wowote wa chama "kitakatifu" humu jf, ila kwa vile hoja zangu ni za kweli, nasimama kwenye kweli, na ni ukweli tuu ndio utakao kiweka huru Chadema na sio timua timua au fukuza fukuza!.

Angalizo wa wapenzi wa Chadema, sijasema chama chenu kinafutwa, nimetoa tuhuma, ambazo zikithibitishwa, Chadema mtaadhibiwa!.

Pasco.
Update !.

Mkuu Dr. W. Slaa, kwanza, heshima yako!, maana ile kujibiwa tuu na mtu wa calibre yako pekee, ni heshima kwangu na kwa thread hii, hivyo majibu yako, nayaunganisha pale mbele ya thread as an authority.

Uwongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli. Sambamba na tuhuma hii, mtoa tuhuma pia ameweka tuhuma nyingine nyingi, zenye kuhitaji majibu ya kina kama haya uliyonijibu hapa.

Kwa vile CCM ndicho chama tawala, Chadema kiko kwenye mizani ya tukiaminie mwaka 2015 au bora kuendelea na CCM tuliyoizoea!, hivyo haya makando kando yoyote kuihusu Chadema, lazima yajibiwe ipasavyo kama hivi ulivyofanya hapa.

Asante sana kwa hili.

Kwa vile maelezo haya yako ni ya upande mmoja, nasubiri verification ya data toka kwa msajili, then niufunge rasmi huu mjadala.

Nashukuru tena.

Pasco.
Update 2: JJ.Mnyika.

[/FONT][/FONT]
Asante sana JJ. Mnyika, nitajitahidi kutembelea kule ili kujiridhisha, ila kwa vile mzizi wa fitna kwenye uzi huu ni katiba ya 2004, kama unayo, nitashukuru tukiipata, tukaufunga huu mjadala rasmi.

Kama unachosema wewe ndio right, kuwa ile katiba ya 2006 sio marekebisho ya katiba ya 2004, bali ni katiba mpya, hata kama ni kweli, katiba ya 2004 ilikuwa na kipengele tajwa, na katiba ya 2006 ikawa haina, then at this juncture, I put my hands down, mjadala umekwisha, kwa sababu katiba ya 2006 ni mpya, na kwa vile ni kitu kipya, then its ok kama haina kipengele hicho!. Hii inamaanisha hata ikipatikana hiyo katiba ya 2004, its immaterial, ila for interest, bado naitafuta hiyo Katiba ya 2004, "kuona ni kuamini.

Pasco.

I have always admired your
intellectual acuity when it comes to
objective reasoning; much respect to
you, and remain blessed.
 
Mkuu Pasco naona umetia varangati mpaka uzi wako umefunguliwa, hongera zako. Saa nyingine nashangazwa sana na maamuzi ya kufunga threads. Sijui hata kwa nini hii waliamua kuifunga. Wewe Mkuu upo katika nafasi ya kuweza kufanya utafiti wa kina kuhusu ukweli wa habari husika kabla hujashuka nayo hapa jamvini. CHADEMA kuna akina Shibuda (Shibuda ni msamiati mpya wa wanafiki unaotumika hapa JF) wengi sana. Hawa akina Shibuda ndani ya CHADEMA wako pale kuganga njaa tu na pia kutafuta habari zinazohusu CHADEMA na Viongozi wake ili waweze kuwachafua viongozi wa juu wa CHADEMA katika juhudi za kuaribu credibility ya chama. Kwa hiyo hata kama ni habari toka kwa kiongozi mwandamizi ndani ya CHADEMA lazima uichukulie juu juu na kuifanyia utafiti wa kina. Pale msajili wa vyama naamini kuna watu makini ambao kabla hawajaruhusu chama kuanza rasmi kujishughulisha na mambo ya siasa nchini huhakikisha kwamba chama hicho kimezifuata na kuzitimiza taratibu zote za uanzishaji wa chama cha siasa ikiwemo kuwa na katiba ya chama. Nenda kwa msajili wa vyama atakusaidia zaidi katika kutimiza lengo lako.

Aliyetoa tuhuma hizi sio mimi, ni kiongozi mwandamizi wa Chadema, mimi nimetoa tuu angalizo kama ni kweli, what might hapenkwa Chadema!. Kwa sasa ni kweli huu ni upuuzi usio na kichwa wa miguu, ila utakuwa umenisaidia sana kama utanipatia hiyo katiba ya 2004!.
Pasco.
 
Wanabodi,

Uendeshaji wa vyama vya siasa nchini, unaongozwa na sheria, taratibu na kanuni. Ikithibitika pasipo shaka kuwa chama fulani, kinakiuka sheria, taratibu na kanuni, kinapaswa kuwajibishwa, kuadhibiwa hata kufutwa, kutegemeana na tuhuma halisi!.

Miongoni mwa masharti ya usajili wa vyama vya siasa, ni kwa vyama hivyo, kuwasilisha katiba yake iliyopitishwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, ikithibitika pasipo shaka kuwa katiba ya Chadema iliyowasilishwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni Katiba "Fake" na sio ile katiba halisi ilipitishwa na Vikao Halali vya Chadema!, hili ni kosa kubwa linaweza kupelekea chama kufutwa!.

Tuhuma yenyewe ni hii na ilitolewa rasmi jana humu jf na mwana jf huyu.

Mara baada ya mwajf huyu kuzishusha tuhuma hizi humu, uongozi wa Chadema umemsimamisha mmoja wa viongozi wake kwa kosa la kuutoa ukweli huu nje!.

Maswali ambayo ni lazima Chadema wayajibu ni haya!.

  • Jee ni kweli Chadema inaendeshwa kwa katiba fake na sio ile iliyopitishwa na vikao halali?!.
  • Jee ni nani alikinyofoa kipengele cha demokrasia ya ukomo wa uongozi ndani ya chama ili kutoa nafasi kwa uongozi wa kifalme na kisultani?.
  • Ikithibitika kuna mtu alikinyofoa kipengele hicho kwa makusudi, atachukuliwa hatua gani?.
  • Je mabadiliko ya "unyofoaji huo" yaliwasilishwa kwa Msajili wa Vyama?.
  • Ikithibitika pasipo shaka kuwa Chadema walikiuka sheria taratibu na kanuni, jee watafanywa nini? (Masajili)
Baada ya kushushwa tuhuma nzito kama hizi, dawa sio kumsimamisha uongozi mtoa tuhuma, bali kutoa majibu ya kina kuhusiana na tuhuma hizi.

Namna rahisi ya kuthibitisha ni kupatikana kwa miniti za kikao kilichopitisha kipengele hicho cha ikomo wa uongozi.
Kisha zipatikane miniti za kikao chochote halali kilichopitisha unyofoaji huo!.

Kisha kwenda kwa Msajili kuthibitisha mabadiliko hayo yalifanyika.

Naandika haya nikiwa ni mwananchi tuu wa kawaida asiye mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali mwenye mamlaka kamili kuhoji jambo lolote kuhusu chama chochote, na sababu ni mimi pia ndiye ninayegharimia fedha za uendesha wa Chadema kupitia kodi yangu inayolipwa Chadema kama ruzuku!.

Pia naelewa fika kinachowakuta wakosoaji wowote wa chama "kitakatifu" humu jf, ila kwa vile hoja zangu ni za kweli, nasimama kwenye kweli, na ni ukweli tuu ndio utakao kiweka huru Chadema na sio timua timua au fukuza fukuza!.

Angalizo wa wapenzi wa Chadema, sijasema chama chenu kinafutwa, nimetoa tuhuma, ambazo zikithibitishwa, Chadema mtaadhibiwa!.

Pasco.
Update !.

Mkuu Dr. W. Slaa, kwanza, heshima yako!, maana ile kujibiwa tuu na mtu wa calibre yako pekee, ni heshima kwangu na kwa thread hii, hivyo majibu yako, nayaunganisha pale mbele ya thread as an authority.

Uwongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli. Sambamba na tuhuma hii, mtoa tuhuma pia ameweka tuhuma nyingine nyingi, zenye kuhitaji majibu ya kina kama haya uliyonijibu hapa.

Kwa vile CCM ndicho chama tawala, Chadema kiko kwenye mizani ya tukiaminie mwaka 2015 au bora kuendelea na CCM tuliyoizoea!, hivyo haya makando kando yoyote kuihusu Chadema, lazima yajibiwe ipasavyo kama hivi ulivyofanya hapa.

Asante sana kwa hili.

Kwa vile maelezo haya yako ni ya upande mmoja, nasubiri verification ya data toka kwa msajili, then niufunge rasmi huu mjadala.

Nashukuru tena.

Pasco.
Update 2: JJ.Mnyika.

[/FONT][/FONT]
Asante sana JJ. Mnyika, nitajitahidi kutembelea kule ili kujiridhisha, ila kwa vile mzizi wa fitna kwenye uzi huu ni katiba ya 2004, kama unayo, nitashukuru tukiipata, tukaufunga huu mjadala rasmi.

Kama unachosema wewe ndio right, kuwa ile katiba ya 2006 sio marekebisho ya katiba ya 2004, bali ni katiba mpya, hata kama ni kweli, katiba ya 2004 ilikuwa na kipengele tajwa, na katiba ya 2006 ikawa haina, then at this juncture, I put my hands down, mjadala umekwisha, kwa sababu katiba ya 2006 ni mpya, na kwa vile ni kitu kipya, then its ok kama haina kipengele hicho!. Hii inamaanisha hata ikipatikana hiyo katiba ya 2004, its immaterial, ila for interest, bado naitafuta hiyo Katiba ya 2004, "kuona ni kuamini.

Pasco.

kama hili likidhibitika basi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nayo iwajibike pia hiki ndio kipindi ambacho chadema wanatakiwa kuwa makini pamoja na ushirikiano kwani wanapitia katika wakati mgumu.
 
Back
Top Bottom