Tuheshimiane jamani

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Wasalaam wana JF hasa wa Jukwaa hili.
Natoa wito wa kuzingatia utu na asiri ya ubinaadamu wetu katika Mijadara yetu humu ndani katika kuhakikisha kwamba hatuvunjiani au kujivunjia heshima.

Kutokana na sababu mbalimbali, baadhi yetu humu ndani wa/tumekuwa tukitumia lugha au manti hasi sana tunapozungumzia jinsia tofauti na zetu, baadhi ya wanawake wanatoa lugha zenye kuambatana na kashfa na dharau kubwa sana kwa jinsia ya kiume vile vile baadhi ya wanaume wanatoa wanafanya hivyo hivyo.

Haya yote yanafanyika huku lugha au mantiki zenye kubeba dhamira ya ushawishi wa hali ya juu sana dhidi ya jinsia nyingine hasa katika maswala la tabia,Uwezo wa aina mbalimbali, n.k kiasi cha kusababisha jinsia husika inayoshambuliwa ionekane ni ya hovyo na isiyo na maana hata kidogo.

Mimi naomba nikumbushe kitu kimoja, kwa upande wa wanawake, wakati mnaponda kwa ukali kabisa jinsia ya kiume, je huwa mnakumbuka kwamba mna baba? na kwamba japo unapotowaka namna hiyo kichwani kwako huwa unaamini kwamba baba yako hausiki kwa sababu tu haiwezekani kutokea mkawa kwenye mahusiano ya mke na mme na baba yako lakini unakumbuka kwamba wachangiaji wengine wanapofikia hatua ya kukubaliana na wewe wao kwao baba yako ni sawa na wanaume wengine wote wasio baba zao kitu kinachopelekea uwe unamtukanisha baba yako mzazi.

Achilia mbali baba yako? vipi kuhusu mwanao wa kiume? utajisikiaje anapotolewa lugha kali kali za kashfa? au kaka yako? n.k

vile vile kwa wanaume, huwa tunakumbuka kwamba indirectly, kauli, na agenda zetu za kuwadhalilisha wanawake huwa zinawarudia mama zetu, au dada zetu, au mabinti zetu?

naomba tuheshimiane jamani, maswala ya tabia ni maswala mapana sana, na sote tunamapungufu,na tunategemeana sana katika kujenga jamii yenye furaha na imara katika kila nyanja ya maisha yetu, Japo tukumbuke kwamba sisi wote ni kizazi cha Adamu na hawa? wote ni dugu moja.
 
Sangarara hii like nimekupa si kwasababu umenikosha roho hataa bali kwasabbu umetukumbusha juu ya kuheshimiana.

sasa mimi nakuja hapa nakuuliza?? hivi maneno ambayo nyie kaka zetu, wanaume huwa mnatumia juu ya jinsia ya kike ni sawa?? na je kwann hili liwe linawauma sana wanaume wakiambiwa kwa lugha ngumu lakin si tukiambiwa sisi wanawake??

kwa picha ya huu uzi wako naona kwamba umejaribu tu kuonyesha ile tabia ya kiume kwamba nyie mko superior kuliko sisi wanawake na kwamba hata iweje mnataka sisi tuwaheshimu hata kama nyie mtatutusi.

ili tuwe fair kaka tuambizane tu ukweli kwamba matusi, kashfa sio maneno mazuri kabisa na kama ndivyo kuliko kutoa lugha za namna hii basi ni vyema tukajenga logic kwenye mada husika.

mfano mzuri nenda kwenye uzi wa Zahra White wa leo utaona jins ambavyo baadhi ya wanajamvi (incluiding me of course) yametumika maneno makali ya kashfa na yenye kumdhalilisha hadi unajiuliza kweli sisi tunaochangia mada tuliwaza vyema??
 
Last edited by a moderator:
^^
Tusipozingatia haya wenye akili timamu watazidi kupungua !!
Tutakosa busara zao.
Jamvi litachanika na utabaki utoto tu.
^^
 
uzi wako unaonekana ulilenga upande fulani jap[o umejaribu kubalance. Jambo la kuheshimiana ni muhimu sana lakini tuanze kuheshimu wengine kwanza na kuwavumilia kwanza.
ukweli ni kwamba hata ukifanya reseach za nyuzi za hapa hasa jukwaa hili ni wazi wanawake wanavumilia sana.
 
Gfsonwin
Just to put the records in order.
Nimewasihi wanaume dhidi ya kauli na agenda za kudhalilisha kama nilivyofanya kwa wanawake dhidi ya wanaume.

Nadhani wanahitajika maadvocate wengi zaidi,probably moderators katika kuhakikisha kwamba heshima ya utu inapewa kipaumbele katika mijadara humu ndani.
 
Lakini jamani saa ingine sisi wenyewe tunajivunjia heshima. Sasa kama huo uzi wa Zahra White hivi kweli mtu mwenye akili timamu utaletaje uzi wa namna hiyo mbele ya kadamnasi, alafu ukitukanwa ulalamike? Hata kama watu wanafanya uozo lkn hawajitangazi mbele ya umma tena kwa kujisifia kana kwamba ni jambo jema.
Heshima unaijenga mwenyewe. Usipojiheshimu usitegemee jamii itakuheshimu.
 
queeny kuvumiliana ni chanzo cha kuheshimiana
 
ukitaka kumfahamu mtu vizuri
tulia usome maandishi yake (Naomba usisome yangu)
Mara nyingi majibu yetu yanabeba uhalisia wetu.

But asante tutajitahidi kujiweka sawa.
 
Lakini jamani saa ingine sisi wenyewe tunajivunjia heshima. Sasa kama huo uzi wa Zahra White hivi kweli mtu mwenye akili timamu utaletaje uzi wa namna hiyo mbele ya kadamnasi, alafu ukitukanwa ulalamike? Hata kama watu wanafanya uozo lkn hawajitangazi mbele ya umma tena kwa kujisifia kana kwamba ni jambo jema.
Heshima unaijenga mwenyewe. Usipojiheshimu usitegemee jamii itakuheshimu.

two wrongs never make it right. kweli Zahra White kaleta uzi mbaya lkn je sisi tutumie busara zetu vipi??
leo niliwaza sana juu ya majibu aliyokuwa kaiyapata na katika majibu yote sikuona jibu ambalo lilikuwa na nia ya dhati ya kumrekebisha zaid ya kumkashfu na kumwona mchafu kuliko sisi wengine wote jambo ambalo si sahihi
 
Last edited by a moderator:
Wanamme na wanawake, tunapendana sana ndio maana tunatamani tubembelezane hata sredini kwa maneno yasiyo makali. At the sama time tunachukiana sana kutokana na maumivu tunayosababishiana, ndio maana tunatumia maneno makali.

Ujue, kuna wakati mtu anachangia kwa lugha kali, si kwamba anamponda mtoa mada au mtoa comment bali hilo tukio linamkumbusha mahali fulani alikoumizwa na mtu wa jinsia hiyo. Anakuwa anatoa hasira zake za kihistoria.

You have a point, ila we can't be the same, it will be boring.
 
Gfsonwin
Just to put the records in order.
Nimewasihi wanaume dhidi ya kauli na agenda za kudhalilisha kama nilivyofanya kwa wanawake dhidi ya wanaume.

Nadhani wanahitajika maadvocate wengi zaidi,probably moderators katika kuhakikisha kwamba heshima ya utu inapewa kipaumbele katika mijadara humu ndani.
mkuu wangu ukirudi kwenye post namba moja umewashutumu jinsia ya kike tu. sasa if you want to play it fair go and edit kwanza ndipo mada inoge kujadiliwa.
 
two wrongs never make it right. kweli Zahra White kaleta uzi mbaya lkn je sisi tutumie busara zetu vipi??
leo niliwaza sana juu ya majibu aliyokuwa kaiyapata na katika majibu yote sikuona jibu ambalo lilikuwa na nia ya dhati ya kumrekebisha zaid ya kumkashfu na kumwona mchafu kuliko sisi wengine wote jambo ambalo si sahihi

tatizo uzi haukukaa kama wa mtu anayetaka kurekebishwa bali umekaa kikujisifia zaidi na kuonyesha kana kwamba hayo ndo maisha. So watu wamerespond accordingly
 
Last edited by a moderator:
mkuu wangu ukirudi kwenye post namba moja umewashutumu jinsia ya kike tu. sasa if you want to play it fair go and edit kwanza ndipo mada inoge kujadiliwa.

Dada Yangu,Mama Yangu,Mwanangu soma para ya pili kutoka mwisho,au kwa vile nimetumia maneno machache,I have honestly said this to both us the male man and female man,I can not be such mean in a presentation like this to leave my male egocentrism exposed such openly.
 
tatizo uzi haukukaa kama wa mtu anayetaka kurekebishwa bali umekaa kikujisifia zaidi na kuonyesha kana kwamba hayo ndo maisha. So watu wamerespond accordingly

Huo uzi unatatitle gani?
 
Wanamme na wanawake, tunapendana sana ndio maana tunatamani tubembelezane hata sredini kwa maneno yasiyo makali. At the sama time tunachukiana sana kutokana na maumivu tunayosababishiana, ndio maana tunatumia maneno makali.

Ujue, kuna wakati mtu anachangia kwa lugha kali, si kwamba anamponda mtoa mada au mtoa comment bali hilo tukio linamkumbusha mahali fulani alikoumizwa na mtu wa jinsia hiyo. Anakuwa anatoa hasira zake za kihistoria.

You have a point, ila we can't be the same, it will be boring.
You mean,disgracing each other is interesting?
 
ukitaka kumfahamu mtu vizuri
tulia usome maandishi yake (Naomba usisome yangu)
Mara nyingi majibu yetu yanabeba uhalisia wetu.

But asante tutajitahidi kujiweka sawa.
Do not take it personal my dear.
 
sasa umu tunafundishana o tunatukanana na kupeana kashfa?
Nadhani jibu la wengi ni TUNAFUNDISHANA,
Sasa basi kama kunamtu anatoa maneno ya kashfa na ma2si hamna haja ya kujibu alicho andika,
Cha maana sana tumwache ajirekebishe
 
Wanaoharibu jukwaa ni wale waletao mada zisizo na tija...
Huwezi kuweka jambo la kipuuzi kwa kuwa tu wewe ni muumini wa fikra hizo, halafu usitarajie ukinzani...
Humu kuna watu huwa wanakuja na mada za kujisifia kuwa wana uume mkubwa, wengine sijui wanapenda waume za watu n.k n.k...
MMU sio uwanja wa matangazo, bali ni jukwaa la elimu lenye kumulika muktadha wa Mahusiano, Mapenzi na Urafiki...
 
kumekucha watoa ushauri nasaha!!
Mkimaliza kutema povu mje jacaranda mshushie na ndovu
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom