Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
Wasalaam wana JF hasa wa Jukwaa hili.
Natoa wito wa kuzingatia utu na asiri ya ubinaadamu wetu katika Mijadara yetu humu ndani katika kuhakikisha kwamba hatuvunjiani au kujivunjia heshima.
Kutokana na sababu mbalimbali, baadhi yetu humu ndani wa/tumekuwa tukitumia lugha au manti hasi sana tunapozungumzia jinsia tofauti na zetu, baadhi ya wanawake wanatoa lugha zenye kuambatana na kashfa na dharau kubwa sana kwa jinsia ya kiume vile vile baadhi ya wanaume wanatoa wanafanya hivyo hivyo.
Haya yote yanafanyika huku lugha au mantiki zenye kubeba dhamira ya ushawishi wa hali ya juu sana dhidi ya jinsia nyingine hasa katika maswala la tabia,Uwezo wa aina mbalimbali, n.k kiasi cha kusababisha jinsia husika inayoshambuliwa ionekane ni ya hovyo na isiyo na maana hata kidogo.
Mimi naomba nikumbushe kitu kimoja, kwa upande wa wanawake, wakati mnaponda kwa ukali kabisa jinsia ya kiume, je huwa mnakumbuka kwamba mna baba? na kwamba japo unapotowaka namna hiyo kichwani kwako huwa unaamini kwamba baba yako hausiki kwa sababu tu haiwezekani kutokea mkawa kwenye mahusiano ya mke na mme na baba yako lakini unakumbuka kwamba wachangiaji wengine wanapofikia hatua ya kukubaliana na wewe wao kwao baba yako ni sawa na wanaume wengine wote wasio baba zao kitu kinachopelekea uwe unamtukanisha baba yako mzazi.
Achilia mbali baba yako? vipi kuhusu mwanao wa kiume? utajisikiaje anapotolewa lugha kali kali za kashfa? au kaka yako? n.k
vile vile kwa wanaume, huwa tunakumbuka kwamba indirectly, kauli, na agenda zetu za kuwadhalilisha wanawake huwa zinawarudia mama zetu, au dada zetu, au mabinti zetu?
naomba tuheshimiane jamani, maswala ya tabia ni maswala mapana sana, na sote tunamapungufu,na tunategemeana sana katika kujenga jamii yenye furaha na imara katika kila nyanja ya maisha yetu, Japo tukumbuke kwamba sisi wote ni kizazi cha Adamu na hawa? wote ni dugu moja.