Tuhamasishe saini 1,000,000 endapo Spika hataitisha Bunge la dharura! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhamasishe saini 1,000,000 endapo Spika hataitisha Bunge la dharura!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Apr 25, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kuna kila dalili hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ikazimwa. Silaha pekee itakayobaki ni kwa wabunge wetu kutahamasisha zipatikane saini zaidi ya milioni moja kutoka kwa wananchi ili kumshinikiza Rais kuvunja baraza la mawaziri na ikiwezekana kuvunja bunge!

  Nashauri po pote walipo wana JF kuanzisha harakati hizi ili ukombozi upatikane haraka!

  Freedom is coming now!
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii ni kwa mujibu wa kanuni ipi? Maana kuna katiba, sasa isije ikawa extension ya fools day.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Tufafanulie mkuu sahihi mil 1 kivipi? Au nayo huku ni 20% ya watanzania?
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ileje hebu dadavua sahihi miliion moja zipo kwa mujibu wa kifungu kipi cha katiba na mchakato wake umekaaje?
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Halafu!?
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mambo hayaendi kwa utaratibu huo, kama kila mtu atakuwa na katiba yake nini kitafuatwa? Umeshasoma katiba ya nchi namna gani Rais anaweza kuondolea madarakani?
   
 7. k

  kaka h Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  funguka zaidi jamaa
   
 8. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ileje una wazo zuri.tatizo tutakwama kwenye kanuni,na mambo ya magamba mtiti.
   
 9. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Viongozi wetu wa vyama vya upinzani wamedhamiria kuishitaki serikali kuitisha maandamano nchi nzima ili kufanyike mabadiliko. Hoja hii ya kutaka mabadiliko katika serikali pia inaungwa mkono na wabunge wengi wa CCM.

  Hivyo ili kufanikisha shitaka hili inabidi kuwe na takwimu halisi zinazounga mkono mabadiliko haya kutoka kwa wananchi kwa kuwa maandamano peke yake hayawezi kuionyesha serikali uhalisia wa kukubalika kwa hoja.

  Hivyo kwa kutumia Katiba ibara ya 8(1) a-c ambavyo vinasema:

  (a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
  itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
  wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
  (b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
  (c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
  (d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
  kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

  Kutokana na ibara hiyo wabunge wataweza kutumia ibara ya 46A kumshitaki Rais kwa kushindwa kutumia madaraka yake vizuri kuzuia wizi na mali na rasilimali za taifa. Watafanyi hivyo wakiwa na imani kuwa wanaungwa mkono wa wapiga kura wengi. Kura zaidi ya milioni moja ni mtaji mzuri.
   
 10. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kama kifungu hiki kipo hakuna haja ya kuvumilia ngumi ile hali una panga mkononi.
   
 11. m

  muislamsafi Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wasalaaam bandugu naona tunaelekea kuzuri
   
 12. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ok ngoja nimtumie huu ujumbe mb wangu.
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  BAsi tumshawishi Pinda ajiuzulu ili kulinda heshima yake ambayo JK amedhamiria kumdhalilisha kila wakati. Tuone kama serikali haijabadilishwa.
   
 14. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Aliyeanzisha mada hii na wachangiaji wote vichwa maji!
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mkuu katiba imeshachakachuliwa, kilichobaki kwa viongozi wetu ni kutukomoa na hiyo katiba unayodai ipo.

  Namshangaa mtoa mada anataka saini mil.1. hata angehitaji sain za watu mil.35 zingepatikana.

  JK anatulazimisha tuanze kuagiza AK47 kwa lazima.
   
 16. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  peoplezzzzzzzzz......power, hapo ndipo signature 1,000,000, zitakapotoka:shut-mouth:
   
 17. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Sioni kifungu kinachowapa mamlaka wananchi kuiadhibu serikari inaposhindwa kutekeleza majukumu
  Adhabu pekee ni kwenye sanduku la kura. ilitoka hapo hatuna ujanja tena nguvu yote tunakuwa tumeikasimu kwa wabunge wetu. kama hao wabunge wanashindwa kufanya hiyo kazi ya kuiwajibisha sherikali basi na wao pia hawatufai maana wao ndio kiungo kati ya wananchi na Serikali.

  Wao wabunge wakiamua wanaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na spika, waziri mkuu au hata rais mwenyewe.

  Kuja kuishitaki serika kwa wananchi ni kupoteza muda tu, sisi wananchi hatuna nguvu hiyo ya kuikoromea serikali labda tushawishiwe kuingia mstuni tu. tusidanganyane hapa jamani. Nguvu yetu ni kwenye sanduku la kura full-stop.
   
 18. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kabla ya hayo hebu tujaribu kutumia hoja ya wingi wetu tunaotaka mabadiliko!
   
 19. ZWANGE

  ZWANGE Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Ustarabu ni jambo dogo tu kuwa mstarabu basi jamani ......... hayo hadi humu ndani tena mmmmhh!!!!!!

   
 20. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Saini 1000000 kwa kigezo kipi? Nafikiri suala hapa ni kuangalia, kama wananchi tunaweza kuwajibisha serikali kivipi. Kifungu kinachozungumzia wananchi bahati mbaya hakija sema technicality zake. ila Bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na raisi, na lenyewe hua linavunjwa (Mtego huu). Kama wanaogopa kutia dole gumba watakubali kurudi majimboni? Sisi tumepewa nguvu ya ya kupiga kura ya kuchagua tu, na sio kuondoa.

  Naona wanasheria watusaidie. Mimi naona njia ya Zitto ndio ya kuanzia. Baada ya siku 14 basi tushinikize bunge likutane. kama wakikataa. sasa hapo hata mimi sijui. Maana pressure itapanda. Ngoja niwaachie vijana wamalizie.
   
Loading...