Tuhabarishane:Maisha Plus East Africa-2016

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Leo ndio uzinduzi wa Msimu wa kipindi cha Maisha Plus East Africa 2016

Kwa wale wadau na wapenzi wa kipindi hiki,tunaweza kukutana hapa kwa muda wa hizo wiki 8 ambazo washiriki watakuwa ndani ya Kijiji cha Maisha Plus.

Mwaka huu washiriki wanatoka katika nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi.Washiriki kutoka Tanzania ni 14,wakati washiriki kutoka nje ya Tanzania ni 16.Haijulikani haswa kijiji kipo maeno gani hapa Tanzania,lkn kwa udodoso wa mambo wakati akitangaza Masoud Kipanya alijisahau ni kusema ili ufike inabidi uvuke daraja la Mto Wami.Hivyo haieleweki haswa uelekeo wa kijiji ulipo.

Washiriki watakaa week mbili za mwanzo bila kuwa na mchunjo.Baada ya week hizo mbili ndipo mtoano utakapoanza.Washiriki watatakiwa kujijengea nyumba za kuishi na watakuwa wanapata mkopo wa shilingi elfu moja kwa siku toka kwenye "bank" ya kijiji na mahitaji toka duka la kijiji.Ujenzi wa nyumba zao na vyoo vya kutumia wataupata kwa kuchimba shimo la udongo la futi sita.Mwisho wa siku mshindi kupata milioni 30.

Kutoka hotel waliyofikia,watakuja kijijini wakiwa wamefungwa vitambaa usoni ili kutojua mahali wanapoenda na mahali walipo.Katika week hizo nane,ni mpambano na mtifuano ndani ya kijiji.
image.jpeg

Tanzania inawakilishwa na washiriki kutoka Mbeya,Mwanza,Iringa,Mtwara,Dodoma na Kilimanjaro.
Kupitia JF...Wale "wapenzi" wa Maisha Plus,tujuzane vibweka,vitimbi na matukio ya Kijiji cha Maisha Plus.
 
vijana wa nchi za Wenzetu wanaonekana wanauelewa wa mambo hawa wa kwetu hata wakihojiwa kwa kiswahili wanashindwa kujieleza na kujibu maswali inavyotakiwa....anyway tupo pamoja mkuu
 
Aisee hawa maisha plus naona wameleta kisu cha kinyarwanda ni sheeda!! kama naona kaka zangu wa kibongo watakavyopiga kura kwa fujo ili asitoke

Bado wako live mpaka sasa?
 
Aisee hawa maisha plus naona wameleta kisu cha kinyarwanda ni sheeda!! kama naona kaka zangu wa kibongo watakavyopiga kura kwa fujo ili asitoke
Yule Mganda yule...Nafikiri ni wale Waganda wa Kaskazini!!Banyankole,kabila la mke wa Mseveni
Ni hatari sana pale...Kavaa skini tait ya ile timu ya kwenye mafuriko!Pale ni lawama pale,maana hata Masoud anamuongelea sana

Huyu dada alisema hawezi kukaa nusu saa bila kujimix na deodorant...Sasa huko chaka atanuka mpaka ajikimbie
 
kumbe ni mganda? amefanana na wa kwa kagame
 
Yule Mganda yule...Nafikiri ni wale Waganda wa Kaskazini!!Banyankole,kabila la mke wa Mseveni
Ni hatari sana pale...Kavaa skini tait ya ile timu ya kwenye mafuriko!Pale ni lawama pale,maana hata Masoud anamuongelea sana

Huyu dada alisema hawezi kukaa nusu saa bila kujimix na deodorant...Sasa huko chaka atanuka mpaka ajikimbie
Japo sina Tv na siangalii kipindi, huyo mganda atakuwa anatoka kwenye kabila la Wahima
 
Back
Top Bottom