Tugutuke: Waosha magari (Carwash) hawana dhamana; Janga likikupata usishangae sana Trafiki na bima wakiamua kukugeuzia kibano wewe mmiliki

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Iko hivi...
Wenye magari wengi tunapopeleka magari hayo kwa waosha magari (Carwash)!

Haina maana sheria za usalama barabarani zinakoma ukiwa eneo la Carwash!

Sheria inampa mamlaka traffic kuingia hata Carwash kukamata magari yanayosogezwa na waosha magari wasio na leseni ya udereva!

Tufahamu kwamba maombi ya kazi ya kuosha magari (Carwash) hayahitaji leseni wala Curriculum Vitae ya Maandishi (CV), Cha zaidi sana muombaji kazi hubeba kitauro begani au Tambala tu kama CV!

Mbali na kuendesha, Mtu ambaye hana leseni ya udereva hatakiwi kabisa hata kukaa siti ya dereva kama tahadhari!

Hivyo tunapowaachia vijana kusogeza magari kosa au janga lolote likitokea tufahamu kuwa bima haiwezi kukulipa wala Mwenye Carwash hawajibishwi kulipa uharibifu wa aina yoyote!

NB; Kwenye Carwash zenye winchi au mahandaki Janga lolote la Winchi ya kunyanyulia magari ikifeli na kuua muosha gari, Gari lako linatakiwa kushikiliwa kwa mda usiojulikana kwa kosa la Mauaji wakati upelelezi ukiendelea!

GARI SIYO NGUO KWA DOBI, TUSIJISAHAU SANA!

Mfano;
expand...
KATIKA KUSOGEZA GARI IKATOKEA YULE KIJANA WA CARWASH AKAGONGA MAGARI MENGINE NANI ATALIPA? AU IKITOKEA GARI AKALIANGUSHA AU KUGONGA UKUTA NANI ATALIPA?
 
Ina maana pale ndani ya car wash Hapana management responsible ya kujua nani ana endesha gari na ni kwa minajili ipi?
 
Wapange hivyo kwa leseni gan? Ya kuosha gari au ya udereva?

Mwenye car wash ana manage, and manager anakuwa na leseni na yeye tu ndo anawajibika Kusogeza Magari....

Ila kama unaenda car wash mshenzy hapo ni sawa, ila car wash zote zinazojielewa they take responsibility!

Kumiliki leseni ni jambo la kawaida sana, na watu wengi, Hata wauza mkaa wanazo! Sasa sio kwamba wewe mwenye gari ndo peke yako una leseni!
 
Aliyekwambia mwenye Carwash anatakiwa kuwa na leseni ya udereva nan? Hujui kuwa MTU yoyote anaruhusiwa kuwa na Carwash almradi Tu awe na eneo na azingatie miundombinu ya usafiwa mazingira?
Na siyo lazima mwenye Carwash awepo wakati wa kuoshwa magari
 
Soma vizuri sana kila nilichoandika utaelewa ninachosema! Siku njema!
 
Back
Top Bottom