Tugeuze uwanja wa ndege Chato kuwa Chuo cha Urubani

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,887
Wengi tunafahamu kuwa kujenga uwanja wa ndege Chato lilikuwa ni jambo la ajabu kiuchumi na ukanda mbaya sana. Jambo lisilopaswa kutokea tena.

Lakini uwanja ule tusiuache uoze, ni pesa nyingi zimetumika. Napendekeza tuufanye kuwa chuo cha urubani. Serikali na watu binafsi wajenge shule za urubani maeneo hayo. Nchi inahitaji marubani, kuanzia ndege ndogo za kunyunyiza dawa mashambani na kuua nzige hadi wa kurusha dreamliner.

Naona hilo litakuwa ni matumizi mazuri ya uwanja ule.
 
Situlikubaliana kuwa tuwaachie wana Chato waanikie Michembe, Udaga, Mafuru, Mahindi Na Mazao mengine yanayohitaji jua kukaushwa??

BTW wazo lako Ni super sana Mkuu naamini wa husika wameshali note Na wataenda kuli table kwenye vikao vyao
 
Endapo uwanja utafanywa kwa matumizi ya ku train pilots,changamoto itakuwa mahala pa kuwaweka hao pilots ie accomodation,best hotels za Chato ni sawa na guest hse za Sinza na Magomeni.
Want rubani Ni lzm alale kwenye fiv hotel as long ni mwanafunzi atala hostel za chato ..acha kukwamisha mawazo ya mwezako et accommodation ndio unachokiwaza wew
 
Huyu mleta mada anataka sisi wananchi wa Chato tukose sehemu ya kuanikia nafaka.
Kama vyandarua tulioletewa na mabeberu tulivigeuza ngao ya vifaranga dhidi ya mwenye, tulisokotea kamba za kufungia ndama, tulibebea mazao kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakati wa mavuno.

Sembuse hiki tulichoachiwa na mwenzetu, tutakitumia kwa matumizi yote tutakavyo. Matumizi yatakuwa yanageuka kulingana na msimu
 
Wengi tunafahamu kuwa kujenga uwanja wa ndege Chato lilikuwa ni jambo la ajabu kiuchumi na ukanda mbaya sana. Jambo lisilopaswa kutokea tena.

Lakini uwanja ule tusiuache uoze, ni pesa nyingi zimetumika. Napendekeza tuufanye kuwa chuo cha urubani. Serikali na watu binafsi wajenge shule za urubani maeneo hayo. Nchi inahitaji marubani, kuanzia ndege ndogo za kunyunyiza dawa mashambani na kuua nzige hadi wa kurusha dreamliner.

Naona hilo litakuwa ni matumizi mazuri ya uwanja ule.
Umewaza kama mm
 
Kama vyandarua tulioletewa na mabeberu tulivigeuza ngao ya vifanga dhidi ya mwenye, tulisokotea kamba za kufungia ndama, tulibebea mazao kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakati wa mavuno.

Sembuse hiki tulichoachiwa na mwenzetu, tutakitumia kwa matumizi yote tutakavyo. Matumizi yatakuwa yanageuka kulingana na msimu
Ile vile vyandarua vya msaada vina kazi sana. Wanazuia kuku wasile bustani, wanabebea makopo na kamba zake ngumu balaa na haichafuki kirahisi.
 
Back
Top Bottom