Tugawane Umasikini, inaleta maana maredio kuishupalia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tugawane Umasikini, inaleta maana maredio kuishupalia?

Discussion in 'Entertainment' started by jimba, Mar 25, 2009.

 1. j

  jimba Member

  #1
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari wana JF,
  Naomba kupata ufafanuzi kuhusu tabia ya baadhi ya maredio kusimamia kazi za wasanii, ninavyofahamu Air time yoyote ya radio inacost amount fulani. Kuna ulazima wowote wa kukomalia mapato ya album ya msanii wa kibongo kwa baadhi ya redio zetu kuweka matangazo mengi yahusuyo show ya msanii mhusika? Mwisho wa ziara ni nani atakaeneemeka na kazi iliyofanyika kati ya msanii na Radio? Naombeni mawazo yenu!!
   
 2. senator

  senator JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ni kweli hii imekuwa ni Tabia ya vituo vingi vya radio kuwafanyia promo za nguvu hawa wasanii wenye majina.Nachojua kuna baadhi ya watangazaji wanaukaribu na yule mwanamuziki tena huenda ni mabest kabisa,hivyo inakuwa rahisi kumrusha mshikaji wake akiwa kwenye kipindi chake.
  Kwa namna nyingine promo zinakuwa nyingi thru radio kutokana nawadhamini especially haya makampuni ya simu ambayo yanapata faida lukuki kila kukicha yanaweza yakalipia kila kipindi kuwe na tangazo la show ya huyo mwanamuziki especially kwenye siku za kuelekea weekends ndo balaa!!
  Kwa upande wa Tv pale inakuwa ni kama habari zingine zinazooneshwa, wadhamini mbali mbali wanakuwa wamechangia..Radio nyingi zimejaa ushikaji na uswahiba inakuwa ishu ndogo kumfagilia msela wao....ingawa kuna tetesi kuwa kuna baadhi ya mastar huwa wanatoa japo kitu kidogo kwenye kuitangaza album yake iwe inarushwa kwa radio mara kwa mara
  Huo ni mtazamo wangu tu!.
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Tatizo langu ni hiyo theme ya kugawana umaskini. Hii inaonyesha jinsi tulivyoathirka psychologically na hamna hata dalili ya kupambana na umaskini. Theme inatujenga kukumbatia umaskini as if ni kitu cha kujivunia.

  Na hizo radio haziwezi kuwashauri hao Mbaongo Fleva kuhusu theme kama hizi? .

  Japokuwa kweli sisi ni maskini , Lakini ni jambo linalotuchukiza wote na hatupendi litutawawale zaidi maana ndio adui yetu mkubwa.

  Msanii kujivika umaskini na akitaka kugawane nae kwangu ni upuuzi mtupu, wala hamu ya kununua hiyo single haiji. Otherwise wafafanue wana maana gani katika hii theme though kwa jinsi wanavyofikri hawatakuwa na la maana zaidi ya Umaskini .I am not prejudicing.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  somo la hakimili linakuja sooon humu.
  wizi mtupu
   
 5. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Huwa inakuwaje kwani, au wewe ungependa iweje?
  Halafu naomba kufafanuliwa maana ya "kukomalia mapato ya album", umeniacha njiani mkuu.
   
 6. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Hata mimi ningependa kupata maoni zaidi kuhusu hiyo dhana ya kugawana umasikini.

  Mfamaji, msanii akiteta jambo kwenye wimbo kwa mfano, anafanya hivyo kwa niaba ya kundi la watu fulani. Si lazima awe anazungumza kwa nafsi yake (kama yeye).
   
 7. j

  jimba Member

  #7
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  I doubt hata hii migawanyiko ya wasanii kwenye makundi yao inatokana na mashinikizo ya haya maredio pamoja na wadhamini wachache wenye uchu na mapato yatokanayo na kazi za hawa wasanii kwani wakiwa kama group mapato ya hawa wanyonyaji yanakuwa machache, kwa akili yangu ya kijinga na sijui kama italeta maana ni hii "Msanii kichwa kutoka kundi fulani akitoka kama solo artist atafagiliwa sana na maredio kabla ya makampuni kumbeba katika kivuli cha bidhaa zao ili wamtafune wakati show zake atakazofanya haziuzi hizo bidhaa" nina maanisha kwamba, kama ni makampuni ya pombe basi zitauzwa pombe na hata sent haitamfikia msanii huyo wakati mapato yatakayopatikana mlangoni yanamilikiwa na hao wadhamini. Mnataka kuniambia makampuni ya simu huwa yanauza voucher kama income yao kwenye show? Na baada ya hiyo show huyo msanii ataweza kurudi kundini na wenzake wakampokea kama zamani? Na vipi kundi likiamua nalo kutoka kama kundi bila ya huyo msanii, maredio huwa yanasemaje kwenye show zao wakati yalimbeba huyo mpotevu? Kuna kaswali huwa kanatawala sana kwenye interview za wasanii na mapresenter kuwa "Inasemekena kitaani kuwa una bifu na msanii fulani fulani, hebu elezea!!!" sasa kwa hapo si kujenga mazingira ya kutoelewena baina ya kambi moja na nyingine?? Tafakarini tuyachange kwa faida ya wasanii wana JF.
   
 8. j

  jimba Member

  #8
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  LAZYDOGY,

  Utakuta msanii akitoa album kama yeye basi ziara zinaandaliwa kila pembe lakini mwisho wa show zote income kwa redio ni almost 70% na msanii anaambulia 30% ya mapato. Nadhani umenielewa maana ya kukomalia mapato ya album from the beginning!!!
   
 9. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,280
  Likes Received: 4,283
  Trophy Points: 280
  Huo ni ukiritimba wa CLOUDS FM hawa jamaa huchukua baadhi ya wasanii ni kuwaandalia matamasha na kupiga nyimbo zao ,ukigombana na hawa jammaa utakoma
  nyimbo zako hazipigwi,hupati mialiko kwenye show na hili limesababisha wasanii kuwapigia magoti
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,189
  Trophy Points: 280
  Katika uchumi wa Tanzania, kutegemea na msanii anayezungumziwa, na stage yake katika career, na popularity yake, hii inaweza kuwa free advertisement kwa msanii ambaye hajajulikana sana.

  Lakini karibu mara zote wasanii wanaopata airtime namna hii wameshajulikana na pengine hawahitaji msaada huu, na mara nyingine mtu anaweza kusema hii ni namna fulani ya over exposure.

  Wenzetu wanachofanya ni kwamba kwa kila wimbo unaopigwa redioni kisheria kunatakiwa kuwa kiasi kidogo cha royalty.Hii system ingekuwepo Tanzania ingesaidia wote, watangazaji wangeweza kuchukua sehemu ndogo ya mapato ya matangazo ya biashara na kuwalipa royalties wasanii kadiri wanavyopiga nyimbo zao, na hii ingeweza kuhamasisha wasanii zaidi.

  Clouds FM wana business model yao na watapiga nyimbo wanazotaka, kama mtu hapendi style yao anaweza kubadilisha stesheni.Mimi siwafagilii.
   
 11. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Jimba nimekuelewa sasa. Kiranga amekwisha elezea nilichotaka kusema.

  Je, wapo wasanii waliolalamikia hali hii? Naamini COSOTA wanaweza kusimamia haki za msanii husika, labda pale anapoanzisha ugomvi na Clouds FM :)
  Kwa upande mwingine, wasanii wangapi wana ma-meneja au walezi wa ma-group yao?
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakuunga mkono kabisa...
  Mimi nilivyosikia Clouds wakishabikia sana kugawana umaskini I was really put off. Hivi kweli watanzania tumekubali kwenda that low? Nilitaka sana kuleta hoja hii tuijadili hapa jamvini lakini nikatingwa na mambo mengine. Nashukuru huyu mkuu ameanzisha hii thread. Wakati tuna MDGs zikitaka tuuage umaskini na pia Dira ya nchi ( vision 2025 ) inasema tuwe tumepunguza umaskini by half ifikapo 2015 na kuufuta kabisa ifikapo 2025... kuna watu wanataka kujigubika umaskini bado! Wakati kuna watu wachache wanagawana utajiri wetu lukuki tuliojaliwa na mola ( maliasili) na ule tuliokusanya kwa maana ya rasilimali kama fedha ( EPA etc) ati kuna watu wanautukuza umaskini na kuanza kuhamasishana kuugawana! Kibaya zaidi media kama taasis yenye ushawishi mkubwa kwa wananchi walio wengi - wasomi na wasiosoma, walio nacho na wasio nacho, wazee kwa vijana, wanawake kwa wanaume... wameona hiyo ndio theme muhimu sana kuipigia debe wiki nzima! Kweli watanzania tuna safari ndefu katika kujikwamua kutoka shimo lisilo na kina la umaskini!
   
 13. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sijapata kusikia huo ushabiki wa Clouds na wala sifahamu walau vipande vichache vilivyomo kwenye wimbo wa "Tugawane umaskini".
  Kuna mwenye lyrics ya huo wimbo hata kama ni ya kuunga-unga?

  Bado ninaamini lengo la mtunzi ni kuchokonoa fikra zetu kwenye hili la umaskini. Bila shaka atafanikiwa sana kufikisha ujumbe kwa jamii.

  Hebu tumwagieni basi!
   
 14. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wazee kuna aliyeusikiliza huo wimbo wa kugawana umasikini atuwekee lyrics hapa?
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wimbo sijausikia lakini hiyo ni Falsafa mufilisi toka mwanzo, kwa nini tugawane umaskini wakati utajiri tunao na unamilikiwa na wachache????? Ingeleta maana kama falsafa ingekuwa tudai tulichoibiwa na kunyang'anywa na kukigawa sawa kwa wote. Kwanza umaskini ni hali ya kutokuwa na kitu itawezekanaje mgawane kitu msichokuwanacho ??????
   
 16. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mzee hadi tusikie yeye hiyo tungo ndio unaweza kusema kwamba ni mawazo muflisi lakini kama yametumika katika falsafa ya kutoa changamoto yanaweza yasiwe muflisi....
   
 17. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  [​IMG]


  BongoCelebrity: Nimekutafuta kwa ajili ya kutaka kujua kitu kimoja; hivi karibuni umetoa albamu ambayo umeiita Tugawane Umasikini. Baada ya kutoka kwa albamu hiyo kumekuwepo na tafsiri mbalimbali kuhusu “kugawana umasikini”. Wengine wanasema kugawana umasikini ni pamoja na kugida maji kwa sana, ngono(zikiwemo zembe) na kwa ujumla kuamua tu kuishi bila kufanya kazi kwa juhudi kwa sababu tayari wengi wetu tu masikini na hivyo hakuna la kufanya. Je, wewe ulimaanisha nini haswa ulipotaka kuzungumzia “kugawana umasikini”?


  Juma Nature: Ahahahaha, labda hapo naweza kusema hiyo ni kazi nzima ya fasihi kwamba kila mtu anaweza kuupokea ujumbe atakavyo au apendavyo na wote wakawa sahihi!....  (Nimeweka kwa ufupi kwa makusudi; Kwa maelezo zaidi bofya hapa:
  http://www.bongocelebrity.com/2009/04/21/%E2%80%9Ctugawane-umasikini%E2%80%9D-maana-yake-nini/ )

  Comment by JeRRy on April 21st, 2009 10:57 am

  Nature hakika umeanza kukomaa mzee, tafsiri uliyoitoa imekaa sawa na inamaanisha ulikuwa unafahamu unachokifanya wakati ukitipa albamu yako jina hilo, Big up mzee. Wasanii wengine igeni mfano huu maana imekuwa kawaida kusoma mahojiano ya wasanii na waandishi na kukuta majibu yao yanatofautiana na maswali wanayoulizwa.  Comment by Muddy Nice on April 22nd, 2009 2:09 am

  Dah dogo naona kidogo anaanza kuelewa anachokifanya. Unajua tatizo hawa madogo wanakula sana Ndumu (Baghi) hivyo kuna kipindi kazi zinawashinda kabisa, nakumbuka huyu dogo alialikwa South Africa lkn alishindwa kuperform kwa sababu ya kilaji, alichapa sana pombe. Tatizo hapa Tanzania wasomi wanajitenga na hawa kina Juma Nature (wasiosoma), lkn kama tungekuwa makini hawa madogo wangezalisha sana pesa na watu kibao wangepata ajira kupitia kwao. Hawa wanataka management tu, hivi wewe embu angalia wale jamaa wanaocheza mieleka kule Marekani, wale ni watu walioshindikana kwa utukutu, lkn watu wamewatengenezea mchezo ambao wenyewe wana enjoy na wamemekewa mameneja, madaktari, wahasibu na system nzima imekalika na watu wanakula mingo nyuma ya migongo yao. Sasa hata hawa walevi wetu kina Nature kama watu wangekuwa makini hawa madogo wangezalisha tu kwasababu wanakubalika. Sasa we angali mtu kama Juma Nature Kiroboto leo anaendesha Benzi we hauoni kama ni maajabu hayo, kutokea anaishi Temeke sehemu duni na ngumu kabisa mpaka kuja kuendesha gari la thamani na lakuheshimika hapa Tz sio mchezo. Hawa madogo wanalipa.

  Nihayo tu wakuu tusijengeane bifu ila mi najaribu kuyaweka mambo sawa kutoka na experiance yangu ndogo ya biashara.

  Muddy  Comment by ngumiji on April 22nd, 2009 7:43 am

  tang nikufaham nature sasa hivi ndo umeanza kuimba vitu ambavyo vinaweza kumfanya mtu akakaa na kukusikiliza kwa makini kuliko ambavyo wewe unafikiria.

  ujue umeanza kuimba vitu ambavyo kila binadamu hai vinamgusa.

  watanzania walio wengi ni masikini sana kiasi ambacho imefika kipindi ambacho ninyi wasanii mnapaswa kukaa chini na kutafuta namna ya kuwasaidia kimawazo.

  “nafurahi umekuwa WA KWANZA” Endelea kutupa vitu mtu wetu.
   

  Attached Files:

Loading...