Tufunge mikanda Januari hii jamani Desemba bado haijakamilisha hesabu yake

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,568
2,000
Jana nililala kwa huzuni sana.

Wale wa kazi wa Mbezi Tangibovu to Rainbow walioona hii ajali naamini kama mzazi wamesikitika sana.

Kijana mmoja akitokea Tangibovu Puma kwenda Rainbow

Alipopita Junction akaona pikipiki zinaenda polepole azipitea, akakuta gari moja inatoka Rainbow kwenda Tangibovu kijana nahisi alishapata maji ya baraka pale Ilalaa, akaliingiza gari mtaroni na speed yake ya schumaker akatoka dirishani.

Hamadi gari ikazunguka na kupitia kichwa chake ubongo ukamwagika na kupoteza maisha.

Kwa mara ya kwanza jana nimewaheshimu sana Madaktari mnasomea vitu hatari sana

Yaani vitu vilivyotoka kichwani huwezi amini vyote vinaenea kule ndani.

Tujitahidi kufunga mkanda jamani Desemba haijakamilisha mahesabu yake. Tuwe makini sana sana

Poleni wafiwa wote kijana amekufa mdogo wazazi wakitarajia makubwa juu yake huko mbeleni

R.I.P Bro.
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
37,572
2,000
R.I.P

Hamna sheria naiheshimu Kama kuvaa mkanda sijawai kupigwa faini kisa mkanda na sitakaa. Mkanda unaumuhimu Sana. Pia speed kubwa sio nzuri. usiendeshe gari ukiwa umelewa.

Gari inahitaji Discipline ya hali ya juu sana!! watu wanaendesha magari wakiwa TUNGI ,Speed kubwa hata ikitokea emrgency kidogo ukikwepa lazima gari iingie mtaroni.
 

Agenda1

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,678
2,000
Waliosema do not drink and drive hawakuwa wajinga! kimsingi ukishalewa ama kuonja kilevi kuna asilimia kadhaa za umakini zinaondoka, hivyo ktk mazingira hayo lolote linaweza kutokea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom