Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kama kuna jambo linalonisumbua akili na kuniuma sana ni kuona kila Ijumaa ndugu zetu masikini wa mji wetu wa Dar wakijipanga kwenye maduka ya Wahindi na Waarabu kupewa msaada aidha ya kifedha au mali, wengine hukaribishwa kwenye Matempo ya Wahindi na Misikiti ya Waarabu na kupewa chakula!
Hii ni aibu na fedheha kubwa kwetu sisi Watanzania weusi ambao ndiyo wenyeji wa nchi hii, kwa nini hawa masikini ambao ni wetu wasijipange kwenye maduka na maofisi yetu?
Sijaanzisha hii mada kumlaumu yoyote yule kwani naelewa sababu ni kukosa Elimu Dunia ambayo jamii nyingine za nje ya Afrika, Kusini mwa Sahara wanayo na hii hufundishwa yaani kusaidia masikini na hivyo basi hupasishwa ktk kizazi hadi kizazi, hivyo ningeiomba Serikali yetu kwa kushirikiana na Taasisi za Dini ianzishe programu maalumu ya kutufundisha jinsi ya kusaidia masikini wetu, tusiwapite tu na kuwaona kama watu baki bali tuwaone kama ni sehemu yetu na tuna jukumu la kuwasaidia ningependelea wasiende tena kwa Wahindi na Waarabu bali waje kwetu sisi kwa msaada wa hali na mali!
Hongera sana Mzee Mengi kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kutenga siku moja kwa mwaka kula na hawa ndugu zetu masikini, Mungu akuzidishie na ningependa kwa kuwa wewe umeelewa maana ya Maisha hapa Duniani basi uwe mstari wa mbele kutufundisha jinsi ya kusadia masikini wetu au niseme ndugu zetu ambao hawajabahatika kama sisi!