Tufikirie Mbali: Mkutano wa Vyuo vikuu na Mashirika ya Oil, Gas na Madini ni Muhimu sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufikirie Mbali: Mkutano wa Vyuo vikuu na Mashirika ya Oil, Gas na Madini ni Muhimu sasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamundu, Sep 28, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Watanzania ni lazima tufikirie mbali ili nchi yetu iweze kuendelea!

  Imefikia wakati wa elimu ya juu kutolewa kutokana na matakwa ya uchumi wetu wa baadae. Kama Zitto alivyosema ni lazima tuelimishe Watanzania hasa vijana kwenye kazi ya baadae ambazo ni kwenye Oil, Gas na Madini.

  Je tutafanyaje

  Serikali au mashirika husika kama tume ya mipango ziweke mkutano wa Vyuo vikuu, Technical Schools na wawakilishi wa kampuni ambazo zitawekeza kwenye Oil and Gas ambazo ni nyingi. Mimi kwa uzoefu wangu wa kukaa hapa Houston, TX ambazo kazi nyingi ndogondogo ni za Oil and Gas ninaweza kuwaambia kwamba kuna kazi nyingi sana zinahitaji mafunzo kuanzia uchomiaji, umeme, kuendesha mitambo ya uchimbaji, safety, computer systems, usafirishaji n.k.

  Mfano vyuo vya Technical vinaweza kutoa mafunzo mengi na badala ya kufunza jinsi ya kufanya umeme wa vyumba pekee vilevile wafundishwe jinsi ya kuweka na kufanya utengenezaji wa umeme wa kwenye meli za uchimbaji.Hii itasaidia maana elimu sio kitu cha mwaka mmoja.

  Kama serikali haiwezi kufanya ni lazima viongozi wa vyuo vikuu waweze kwenye kwenye kampuni moja kwa moja badala ya kusubiri serikali kufanya kila kitu kama ilivyo kwenye nchi za wenzetu.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ngoja niongeze kwa Mfano mmoja:
  Nilienda Tanzania mwaka 2009 na nikakutana na Wamarekani vijijini wanaweka nguzo za umeme. Nikasimama na kuongea nao jamaa mmoja alikuwa ametokea Iowa akaniambia wanafanya kazi chini ya mpango wa Millennium Challenge Corp na wanalipwa $8,000 kwa mwezi na hakuna Tax na wanapewa malazi na chakula. Huu jamaa alikuwa fundi wa umeme huku hana hata degree yeyote na akaniambia kampuni anayofanya ilipewa tender na wasingeweza kuamini kirahisi Watanzania kuweza kufanya kazi kwa ufanisi kwasababu hawana mafunzo na uzoefu. Kazi kama hizi hazihitaji watu kutoka nje.
   
 3. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,165
  Likes Received: 1,169
  Trophy Points: 280
  Like x 100!, tunahitaji kubadili mfumo wa uongozi kwanza, huu tulonao hauwezi kukubali constructive ideas kama hizi, kwani tunayoyaona kama makosa kwao wanaona tija!
   
 4. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Viongozi wetu sio wasikivu kiasi hicho mkuu! Hawapo tayari uchumi wetu umilikiwe na waswahili. Wanapendelea wageni ili 10% iwahusu! Nakuhakikishia, ili rasilimali zetu ziwe na manufaa kwetu, ni lazima watanzania wazichimbe wenyewe! Nyerere aliliona hili na akasema tuyaache madini yetu hadi tutakapoweza kuwa na wataalam wazawa!!

  Hawa wezi/mafisadi wakamwona hana maana! Angalia, kila anaepewa wizara ya nishati na madini anakuja na mkakati wake wenye lengo la kujinufaisha yeye "personally". Ngoja tumsome Mhongo, may be anaweza kuwa mzalendo..
  By the way, ushauri wako ni mzuri sana.
   
Loading...