Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,726
Tabia ya Mkuu wetu kupenda watu wakariri takwimu ina pande mbili. Kwa upande wa mambo ya fedha , Mkurugrnzi (DED) kukariri takwimu yaweza kuwa dalili ya yeye kufuatilia mafungu. Wakurugenzi wa namna hii wanajulikana kwa ulaji wa fedha. Huidhinisha fedha na kuzifuata nyuma ili wazitafune. Na katika kukariri huwa wanahakikisha wanakula bila kumaliza na kwa hiyo wanatunza kumbukumbu. Ukiwa mwongo usiwe msahaulifu.
Upande wa pili kutokariri takwimu za fedha ukiwa mkuu wa taasisi, yaweza kuwa dalili ya udhaifu (si uzembe). Kwamba, unategemea mtu mwingine ajue fedha kuliko wewe. Hili si kosa la kumwondoa mtu katika nafasi yake.
Kwa hiyo kutumbuliwa kwa mama yule na baba yule, yawezekana tatizo si kushindwa kukariri. Yawezekana na masuala mengind ukitilia maanani kuwa Mkuu alitamka kuwa amewasamehe.
Nilipoiangalia ile clip kabla ya kutokea barua ya kuwatumbua, nilicomment kuwa "ningelikuwa mimi, ningempandisha cheo yule mama". Nilimwona ana msimamo mzuri na kusimamia anachokijua kuliko kukimbilia kumdanganya Mkuu. Je kuna tofauti gani kati ya Askari aliyemkatalia mke wa waziri fulani barabarani alipotaka kutumia nafasi ya mmewe kutolip faini ya trafic?
Yule mama alim-adress Mkuu wa heshima sana tofauti na kauli ya " huwezi kunijibu hivyo mimi".