Tufanyeje ili kurejesha imani ya wananchi kwa vyombo vya dola | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanyeje ili kurejesha imani ya wananchi kwa vyombo vya dola

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Jul 9, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mtu ukisikiliza vizuri kauli za wananchi unapata picha ya kuwa wananchi walio wengi hawana imani hata kidogo na vyombo vyote vya dola ikiwemo polisi, na kwa ujumla watumishi wote wa umma. Si hiyo tu hata mihimil mpngine ya dola kama mahakama na bunge nayo utendaji wake unawekewa mashaka.

  Lakini baya zaidi, hata ofisi ya rais nayo imeanza kuingizwa kwenye mkumbo huo. Haina budi ieleweka ya kuwa rais kama kiongozi mkuu wa serikali na mkuu wa nchi, ndiye mwenye kutoa taswira ya watanzania.

  Hivyo inapoanza kujengeka hisia ya kuwa hata rais ahaminiki, hii nchi itakuwa inaelekea wapi! Ombi langu kwa wote wenye dhamana ya kutuongoza; tafadhali tofautishieni nafsi zenu na ofisi mnazoongoza.

  Hizo ofisi zenu ni taasisi zina uhai wa pekee, hivyo ikiwa kuwepo kwenu katika ofisi hizo hivi sasa kutazidhohofisha kwa namna yeyote ile madhara yake yatahadhiri vizazi vingi vijavyo.
   
Loading...