Tufanye yafuatayo ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika bandari yetu ya Dar es Salaam (TPA)

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
3,221
3,751
Ukusanyaji wa mapato katika Bandari ya Dar es Salaam umekuwa ni changamoto tangu taifa letu lipate uhuru, tatizo hili limesababisha kufanyika mabadiliko ya wakurugenzi wa bandari (TPA) kila inapobidi kufanya hivyo tukidhani kwamba ndio dawa ya kutibu tatizo hilo.

Lakini kwa wakati mwingine imekuwa ikisaidia sana kutibu tatizo hasa inapotokea mkurugenzi aliyeteuliwa hakuwa mwadilifu.

Yafuatayo ni matatizo yanaikabili TPA tangu uhuru mpaka sasa:

1. Kutokuwepo kwa uadilifu kwa wakurugenzi wanaoteuliwa.

2. Mfumo wa zamani wa uendeshaji wa bandari (non-digitalized) or non-smart

3. Kutokuwepo kwa uadilifu kwa wafanyakazi wengine wa bandari.

Ili kutatua matatizo hayo serikali inaweza kufanya yafuatayo:
1. Serikali itumie taasisi hizi mbili (PCCB na TISS) vizuri ili kuwatambua na kuwagundua wafanyakazi au watumishi wanaokula rushwa, kufanya ufisadi au kuhujumu mapato ya bandari. Kama ikibidi serikali inaweza kuvunja TISS na PCCB na kuunda nyingine mpya ili tu kuongeza ufanisi na kuleta mabadiliko.

Wakati mwingine mkurugenzi anaweza kuzungukwa na wafanyakazi wa chini yake, na mara nyingi wakurugenzi wengi hawana mbinu za kuwagundua wanaohujumu mapato, swala hili linahitaji wachunguzi wa siri kutoka nje yaani ofisi ya Rais, TISS na PCCB.

Hivyo, serikali inapaswa kuwa macho sana wakati wa kuchunguza mambo yanayoendelea bandarini ili kufanya madiliko kwa wakati inapoonekana ofisi ya mkurugenzi haifanyi vizuri.

2. Serikali itengeneze au kuongeza coordination au ushirikiano kati ya taasisi zote zinazofanya kazi bandarini. Bandarini kuna taasisi nyingi Kama TRA, TASAC, clearing Agents na Mamlaka ya Bandari yenye dhamana ya kusimamia upakuaji na upakiaji wa mizigo, utunzaji wa mizigo nk. lakini bado menejimenti ya bandari wanakwama katika kukusanya kile ambacho serikali inategemea.

Hivyo, ili kuleta coordination, nashauri taasisi zote ziwe kwenye jengo moja ili zimalize kazi kwa pamoja na kwa wakati. Kuna muda mwingine huduma za bandarini zinatolewa bila kulipia wharfage na storage charges, au mizigo iliyohifadhiwa inatolewa kabla TRA hawajatoza ushuru wa forodha. Kukaa kwenye jengo moja kunaweza kutatua tatizo hilo.

3. Serikali ikiziunganisha taasisi zinazofanya kazi bandarini kwenye jengo moja ijaribu pia kuweka mifumo inayosomana kati ya taasisi na taasisi ili kurahisisha operations za kitaasisi kwa madhumuni ya kuleta ufanisi.

4. Serikali idigitolaizi mfumo mzima wa kuendesha bandari kuanzia physical operations hadi ukusanyaji wa mapato. Serikali ipunguze kabisa kutumia paper docs zinaongeza uvujaji wa mapato. (DIGITALIZATION ni muhimu)

Let's make our port smart to collect revenues smart.

Ni mimi
Meneja wa Makampuni.
Kwa ushauri zaidi
Karibu PM
au
email: menejawamakampuni@gmail.com
 

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,488
li imrudishe Injinia Kakoko. Ndugu huyu alipaisha sana mapato ya TPA.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
28,336
31,259
Hii bandari tumpe mchina atupatie Tshs 1.5 Trillion kwa mwezi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom