ukhuty
JF-Expert Member
- Oct 9, 2016
- 16,851
- 41,924
Wakuu kuna utafiti nafanya wenye lengo la kufahamu mtizamo wa vijana na nini kifanyike kuhakikisha vijana wengi wanaingia kwenye social entrepreneurship. Nahitaji msaada wa mawazo yenu.
Mjasiriamali wa kijamii ni nani? Huyu ni mtu anayeanzisha biashara kwa kusudi la kutatua matatizo ya kijamii au athari chanya katika mabadiliko ya kijamii.
Zaidi ya vijana milioni 75 duniani wanaelezwa kuwa hawana ajira, vijana milioni 279+ kwenye nchi za kusini mwa jangwa la Sahara wanaelezwa nao kuwa hawana ajira na hakuna mikakati madhubuti iliyowekwa kwaajili ya kuwatengenezea vijana hawa mazingira ya kujiajiri na kuajiriwa kwenye sekta za umma na sekta binafsi.
Je, tufanye nini ili vijana wengi waingie kwenye Ujasiriamali wa Kijamii?