Tufanye Nini Ili Serikali Itekeleze Majukumu Yake Ipasavyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanye Nini Ili Serikali Itekeleze Majukumu Yake Ipasavyo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TANURU, Feb 16, 2010.

 1. T

  TANURU Senior Member

  #1
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Habari za leo?

  Katika HOJA mbalimbali hapa tumejadili kwa kina kuhusu matatizo mbalimbali yanayoikabili nchi yetu bila kusahau ufisadi uliovuka mipaka.

  Kama ni kweli kuwa CCM itaendelea kushinda katika uchaguzi wa mwaka huu na kuunda Serikali, Nini hasa Wananchi wa nchi hii tunatakiwa tufanye ili kuhakikisha Serikali ijayo ya CCM inawajibika ipasavyo kwa Wananchi watakaokuwa wameiweka madarakani na kuhakikisha kuwa nchi hii na watu wake wanapata maendeleo kadri ya mategemeo na matarajio yao.
   
 2. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nguvu tuliyonayo ni kwenye kupiga kura tu!
  Inatakiwa watu wahamasishwe wasichague serikali dhalimu tena, hapo ndo tunaweza kuiamrisha serikali na ikafanya vile tunavyotaka sisi wananchi!

  Wanasiasa wakishaona kuna uwezekano wa kutochaguliwa, watafanya yale yanayopaswa kufanyika kwa manufaa ya nchi.

  Tofauti na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura hatuwezi kuiamrisha serikali kwa lolote.
   
 3. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,457
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Binafsi naona hata msipoipigia kura CCM bado chama hicho kitashinda tu, kumbuka uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 1995.

  Kitu pekee kinachoweza kuilazimisha serikali kufanya kazi yake ipasavyo (as per public interest) ni KUGOMA KULIPA KODI. Kila mmoja wetu akigoma kulipa kodi iwe individuals or corporates iwe PAYE or VAT or Customs duty or import duty....Hapo wana wa nchi tunaweza kufaidi matunda ya nchi yetu, tukigoma kwa muda wa miezi 3 tu, basi wakuu watanyooka tu.

  Hapo kuanzia mh. rais mpaka afisa wa chini wote watakuwa ni watumishi wetu!!
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,699
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  1. Mhakikishe mnapata wabunge wengi wa Upinzani
  2. Mawaziri wasiwe wabunge
  3. Ma CEO wa makampuni ya umma wapatikane kwa ushindani
  4. Elimu kwa uraia... mtendaji wa kila siku wa Serikali ni Waziri Mkuu sio Raisi
  5. Mtenganishe siasa na proffesional kama uhandisi etc...
  6. Punguzeni kuongoza nchi kisiasa...
  7. Kimbizeni Serikali kuhakikisha makampuni ya miundo mbinu yanakuwa imara mfano, TANESCO, TRL, TTCL, TPA, ATCL, etc... haya yakishakuwa njema biashara/kaz zitafanyika kodi zitakusanywa... na huduma kama maji, afya, elimu zitapatikana kwa urahisi zaidi...
  8. Fumua mfumo ya employment compensation wa serikali, kuhakikisha wafanyakazi wajuu wa serikali wasikae kutengeneza safari na seminar... pay them well, but no gain in seminar & travels.
  9.
  10.
   
 5. T

  TANURU Senior Member

  #5
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Brooklyn,

  Nakubaliana na wewe kuhusu huo mkakati.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,933
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180

  Kasheshe upo sahihi kabisa, hilo la wabunge wa upinzani kuwa wengi ni dhahiri kabisa, umeona hapo akina slaa na Zito walivyoliendesha puta bunge sasa kukiwa na wengine wengi mahihri wa upinzani nadhani haya mambo ya kulindana ya CCM yatakwisha
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,933
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180

  Kasheshe upo sahihi kabisa, hilo la wabunge wa upinzani kuwa wengi ni dhahiri kabisa, umeona hapo akina slaa na Zito walivyoliendesha puta bunge sasa kukiwa na wengine wengi mahiri wa upinzani nadhani haya mambo ya kulindana ya CCM yatakwisha
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Unauliza swali kana kwamba mfumo wa sasa wa kiuongozi ni impecacable flani hivi. which is NOT.

  As long as tunaendelea kuuabudu, kuutukuza na kuukumbatia mfumo wa sasa wa kujitawala (including the so called uchaguzi), I can tell now, and even if I would be reincarnated 1000 years later I will tell the same thing, kwamba this system is bound to fail and it will continue to do so. Huezi kupanda chelewa ukachipua mnazi.

  Hivo bana, solution ni kutafuta mfumo mpya wa kujitawala ambao utakuwa free from siasa, opinions and subjectivity.
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mkuu haya yatakuwa magumu kuyatekeleza - yanahitaji muda kidogo (tatizo la kimfumo) ila hili la huyu mdau Brooklyn - nafikiri ni la kuanza nalo kuonyesha kuwa tushachoka kulipa kodi watu wanazichezea chezea tu pesa zetu.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...