Tufanye nini basi wakati huu wa dhiki kuu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanye nini basi wakati huu wa dhiki kuu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlangaja, Feb 15, 2011.

 1. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kutokana na hali ngumu ya maisha kuendelea kuongezeka kila siku katika nchi yetu nimeonelea nami nijitose na kutoa angalau mawazo machache kuhusu nini cha kufanya.
  Kihistoria watu walioanzisha mbio za kupigania uhuru wa nchi hii ni wafanyakazi na wanafunzi wa kipindi kile cha ukoloni. Hawa walijitoa bila kujibakiza, walikuwa tayari kufa ili Watanganyika wapate uhuru wao. Na kwa kweli watu wengi walikufa na wengine waliwekwa magerezani na familia zao kusambaratika. Ni kutokana na jitihada hizo Watanganyika tuliweza kupata uhuru mwaka 1961.
  Katika siku za karibuni Watanganyika tumeingia katika hali ngumu sana ya maisha, tumekosa umeme, bei za vitu zimepanda, nauli zimepanda, rushwa imeongezeka kwa kasi kubwa na zaidi sana viongozi wetu wamezidi kuvumba kama madebe matupu huko bungeni. Viongozi wetu yaani wabunge wanajilipa fedha nyingi na hivyo kufanya hali yetu izidi kuwa mbaya zaidi. Ukitoa wachache ambao wanatutetea wengi wao wamekuwa waasi kabisa. Mfano kujilipa shilingi milioni 90 kwa ajili ya ununuzi wa magari wakati taifa likiingia katika mgao mkubwa kabisa wa umeme ni ishara wazi kwamba viongozi wetu wameamua kuasi nchi yetu.
  Kwa hivyo basi mimi nashauri wafanyakazi wote na wanafunzi nchini waamke na kushinikiza serikali ifanyie kazi kwa haraka suala la umeme, rushwa, na mfumuko wa bei. Kama masuala haya hayatafanyiwa kazi na serikali, hii itaonesha wazi kwamba serikali yetu imeshindwa kutekeleza wajibu wake hivyo itapidi itoke na viongozi wengine wenye uwezo waingie kuiongoza nchi hii.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Jibu mbona liko wazi mkubwa, hivi Tunisia, Misri, Algeria ziko sayari gani? Mbona uwezo uko mikononi mwetu, hawa manyang'au wanaotuumiza mbona wepesi tu tena waoga ndiyo maana wanakimbilia kutumia polisi na jeshi, lakini mambo yakiiva askari nao wataunga mkono nguvu ya umma kwani nao ni wahanga wa mabaradhuli waliopo madarakani.
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  We deserve it, kwa kuwa tulishindwa kuchukuwa hatua katika muda muafaka.Na bado tutalia na kusaga meno.
   
Loading...