Tufanye je ili makabila yanayofuga kwa kuhamahama yatulie kufuga kwa tija? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanye je ili makabila yanayofuga kwa kuhamahama yatulie kufuga kwa tija?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andindile, Apr 18, 2009.

 1. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF kwa miongo mingi, makabila ya wafugaji kama wamang'ati, wamasai, Wairaqwi, n.k wamefanyiwa mambo mengi ya kuwalazimisha wabadili mfumo wa maisha yao ya ufugaji wa kuhamahama na usio na tija. Mambo waliyofanyiwa ni kama yafuayo.
  (i) maeneo yao ya kufugia ya asili kuchukuliwa na selikari either ya kikoloni au ya uhuru na kuyafanya kuwa hifadhi za Taifa. Kwa kufanya hivyo maeneo ya kufugia yalipunguwa sana na kusababisha uhaba wa malisho
  (ii) Selikari wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni zilihamasisha jamii ya wafugaji kuanza kujishugulisha na kilimo katika maeneo machache yaliyobakia ya kufugia. Ni kweli baadhi ya wafugaji wakaanza kulima katika maeneo ya kufugia. Jambo la kunote hapa ni kuwa, kwa ujumla maeneo mengi ya kufugia sio mazuri kwa kilimo hivyo hupoteza rutuba haraka na kutozalisha chakula cha kutosha. Hivyo hata wale walioamua kulima walilazimika kuendelea kufuga kwa sababu hawakuwa na uhakika wa kupata chakula cha kutosha.

  (iii) Pale migogoro ya wakulima na wafugaji inapotokea, wafugaji wakati wote wameonekana ndio waanzilishi wa migogoro hiyo linapokuja suala la kuchukuwa hatua tumeshuhudia wafugaji wakifukuzwa, kutozwa faini kubwa, kuporwa mifugo, au kuhamishwa bila maandalizi yoyote.

  Uhaba wa ardhi katika maeneo yao umesababisha wafugaji wengi kuhamia katika maeneo mengine na kujikuta katika migongano na jamii nyingine. Na migogoro inapotokea, tunawasikia baadhi ya viongozi na wenyeji wa maeneo husika wakiwataka warudi walikotoka. Njia hizi za kutatua matatizo ya wafugazi zimekuwa si endelevi kwa ustawi wa jamii za wafugaji na maendeleo ya watanzania kwa ujumla.

  Je wanaJF nini kifanyike ili kuboresha maisha ya wafugaji? Kama Botswana waliweza sisi ni kitu gani kimetuzuia? Tunapojadili hili, tukumbuke kuwa Tanzania ina ardhi tele ambayo inafaa kwa kilimo na kufugia mpaka tunataka kuwagawia wageni hekta 500,000. Na wengine tayari wameshajichukulia ardhi katika bonde la mto rufiji na kwenye vijiji ya Kisarawe Pia tukumbuke kuwa baadhi ya maeneo hayafai kwa kilimo cha mazao bali kwa ajili ya kufugia tu.

  Karibuni tujadili
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Juhudi zaidi kwanza ktk kuachana na ufugaji wa 47 na kuwa na ufungaji wa tija!
   
 3. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tufahamishe huyo anayetakiwa kufanya hizo juhudi.
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kuna dhana kuwa ufugaji wa kuhamahama ni mfumo wa kizamani ulio katika mpito ( transitory livelihood) na hivyo basi unapaswa kufutwa na kuingiza jamii hiyo kwenye mfumo wa kisasa "uliostaarabika".Huu ni upotoshaji mkubwa na bahati mbaya sana ndiyo mtizamo wa watu wengi hata serikali.Matokeo yake ni kwamba jamii hizi za wafugaji wa kuhama2 nao kwa sasa hivi wameamka na wameanza kwa kupitia asasi ( CSOs/CBOs) zao kuleta ajenda zao katika ngazi mbalimbali na kutetea haki yao kama haki ya wakulima na wengineo.

  Kinachotakiwa ni kuuelewa mfumo huu na kuupa support mbalimbali kama kuwawekea huduma na kuwapa nyenzo za kupambana na mazingira yao kule waliko.Kama tunavyojua mara nyingi mahitaji yao ya malisho yanakinzana na mipango mingine ya maendeleo - mfano mzuri ni Ngorongoro ambako kuna wanyama na utalii unapewa kipaumbele kwa maana ya sera na hata sheria.Nchi nyingi - Tanzania, Kenya, Uganda,Eritrea,Ethiopia, Somalia na hata Sudan wanazo program mbalimbali za kusaidia jamii hizi na kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuibua maswala muhimu yanayohusiana na mfumo huu wa maisha.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hatuna haki ya kuuhukum mfumo wao wa maisha kuwa ni wa kizamani usio na tija!
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  sasa ya nini kung'ang'ania mambo ya 47 ambapo hakuna tija?

  wapewe elimu na kulazimishwa kufanya kilimo cha kisasa!

  tuache nadharia za kusoma ktk vitabu!
   
 7. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tafiti zinaonyesha kuwa kumfuga Ngombe mmoja kwa miaka minne ndipo uje umuuze ni hasara kama tunataka kuzalisha kwa tija. Je wataalamu wa mifungo hawawezi kubuni namna ya kuboresha mifugo ya wafugaji hao (i) kwa kupunguza kipindi cha kumlisha ng'ombe mdogo ili awe mkubwa badala ya miaka minne na kuwa mmoja (ii) kuongeza uwezo wa hao ngombe kutoa nyama kwa wingi katika muda mfupi?
   
 8. F

  Felister JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hili swala si lakufanya kwa papara au adhoc niswala linalohitaji research na iwe participatory ikiwahusisha wahusika wenyewe kwani wana ample knowledge accumulated over a period of time ila kutokana na wao kukosa nguvu katika maamuzi yaliyo pelekea wao kuwa marginalised. Sasa mfano hypothetically mara nyingi baada ya kufanya analysis kama unataka kuwa transform hao minority waondokane na huo ufugaji lazima kuwe na integrating programs kwa mfano lazima u identify hao watakao endeleza huo ufugaji baada ya hao kuwa transformed maana si siri hiyo ina implication kwenye nutrition ya community ya tanzania ambayo hata pamoja na hiyo cheap labour ya wafugaji bado protein consumption iko chini kutokana na family nyingi kutokuwa na uwezo wa kununua nyama kama source of protein ambayo ni common to most of us hata kama frquency za ulaji zina vary.

  Sasa suppose hutaki hawa washamba wawe wafugaji its very easy unaweka surport price ya kuuza hao predetermined stock type say ng'ombe na unawapa mitaji enterprenuers let say veterinarian, animals scientist and agribussiness certificate owners. Condition ni kununua mifugo ya hao wafugaji for the st price na ili kulinda local spicies transformation of any how kwenye ranchi lazima kwa certificate maalum na tue given percentge of the total number given to you as quota to produce. Hao kwa utaalam wao watanzisha ranchi za kitaifa as identified na wizara husika za mifugo na ardhi through out agroecological zones. Hapo utaona unawawezesha hao wafugaji kuaanza maisha mbadala kwakuwapa capita ya kuanzia wakitaka watapeleka watoto wao shule au wata invest ila kuwe na education program ya kuwa guide on their decision though an individual would decide what is appropriate to them. Alafu ume creat ajira kwa graduate wetu na kuwa protect for watakao ruhusiwa kuendesha hizo shughuli ni wao tu ila kuwe na penalty kali kwa watakao fanya tofauti na projects documents zao au bussiness plan zao kwakuwa product watakayo pata wao ndo owners basi hapo huhitaji zaidi kwani wao ni wasomi wataendeleza sector profesionerly na asipofanya hivyo competition itamwondoa within themselves ila kulinda market internally hizo zinakuwa established strategically in several regions na siyo concentrated in one area. Hapo kwakuanzia na kuboresha through lessons learnt utakuwa umewatoa watanzania wengi kwenye umaskini kwani soko la nyama ni kubwa mno standards tu ndo hatuna huwezi sema eti tutakosa soko never I can assure you. Mabenki yanaweza toa mikopo kwa hao wakidhaminiwa na serikali na vyeti vyao ndo colateral.

  I sometimes wonder why are peple poor why and why we even dont need money from outside we need right ideas.
   
  Last edited: Apr 18, 2009
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hii siyo nadharia ya vitabuni.
  Ndiyo ukweli na hali halisi ya maisha yao - ni utamaduni wao na bahati mbaya sana wao hakuna mtu anataka kuwasikiliza au hata kuwaelewa.Na wao wanadhani kuwa " siye wenye mtizamo chanya kuwahusu2 ndio haswa tunastahilikuelimishwa. Nadhani tutapata wachangiaji wengine ambao watatupa maoni zaidi kuhusu hili jambo.Watu wengi tunajiuliza, kuna faida gani kuwa na maelefu ya ng'ombe ilahali watu wanaishi kwenye "umaskini" uliokithiri? Kwanini wasiuze ng'ombe wakabakiza wachache wanaoweza kuwa na tija? - wao watakuambia huo ndiyo utamaduni wao na wana haki kuwa na utamaduni na utambulisho wao.
   
 10. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tukumbuke kuwa mambo mengi yanabadilika. Ongezeko la watu, mabadiliko ya hali ya hewa, "ufinyu wa ardhi", kupanda kwa hali ya maisha n.k. Watu hawa pia watahitaji wapeleke watoto wao shule, hospitali, wapate huduma za maji, maeneo ya kutosha kwa ajili ya kufugia, wanunue chakula e.t.c. Wanaishi katika ulimwengu unaobadilika. Je tuboresheje maisha yao?
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  msilisema mnawapelekea pesa za EPA...LABDA WAKIONJESHWA NAO WATAACHA
   
 12. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nimekumbushia kuwa sio maeneo yote ya nchi hii yanafaa kwa kilimo cha mazao ya chakula au biashara bali kwa ajili ya kufugia tu. Pia kuna baadhi ya watu wanaskills za kufuga na si za kilimo kwa nini hizo skills tusiziendeleze katika maeneo yasilyofaa kwa mazao ya chakula?
   
 13. F

  Felister JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Napenda kukuhakikishia tena ntakupa hata research tulizowahi kufanya wafugaji percapita income yao ni juu mara zaidi ya elfu moja ya wakulima in their local areas. Unachoona si umaskini bali ni utamaduni wao maana sisi tunacho sema ni maendeleo tunaangalia mavazi na shelter lakini hata kwakuangalia expenditure tu yao ni kubwa kuliko hata waajiriwa serikalini. Ni mawazo tu kusema kuwa wafugaji ni maskini ofcourse kwa international standards yes but kwa purchasing power parity they are ahead of many of us. Mimi ningekuwa na hold power kwenye maeneo waliopo wafugaji wananchi wa hapo hakuna hata moja atakuwa maskini nakuhakikishia maana sioni possibility ntakacho fanya nikuunda system itakayo saidia kureduce inequality kwenye income distribution basi.
   
 14. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hiyo system inaundwaje? hayo ndio majibu tunayatafuta (au jibu lako ni blue print lenye hati miliki?
   
 15. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  taabu pia ukame ukitokea hawa wafugaji mifugo hufa en mass!

  Saa ingine hawa wafugaji ni liability kuliko faida!

  hatuwezi kusema waendelee tu!!!!!!!! hivyo hivyo basi!

  A draconian move is needed: waamue moja je wanabadilika au vipi vipi..hadi kieleweke. hii pia ni kwa wakulima wa jembe la mkono na wale wanaolima robo eka!

  Yaani waamue tu moja: you cant transform the society ya watu wanaishi enzi za 1800's kwa kuwabembeleza!
   
 16. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wao hawajaamua. Sisi tunaoona kuwa kuna umuhimu wa wao kubadilika ili waendane na hali halisi ya mabadiliko tunawasaidiaje ili waamuwe kutransform jamii zao?
   
 17. F

  Felister JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  No siyo hati miliki maana nilisoma kwa kodi ya watanzania wote na knowledge yangu ntatoa bure pale ntakapo hitajika maana umaskini wa binafsi naamini mungu amenipa uwezo wa ubongo wangu kuuondoa bila hata hati miliki ya knowledge niliyo nayo.

  Ni hivi mkulima na mfugaji wakiishi kwa symbiotic relationship comparative advantage yao ya ku produce more than each producing independently, so production of them both cooperating ni kubwa zaidi ya wao ku compete with each other on land resource. Sasa mimi nikiliweka hili katika lugha wanayo elewa na kuwa na transparency katika whatever each is receiving ni one step ahead kwa sehem ambazo hawana hiyo opportunity. Then it for me to loby to the graduate kuanzisha miradi ambayo itafanya value addition kutokana na products from crops let say mahindi tunauza unga badala ya mahindi kutoka hiyo local area yetu na meat products instead of live animals ili ku maximize profit na ku raise efficiency. Na mambo mengine ni mpaka niwe hapo na kuangalia what are the problems of those local people and decide them on our way forward.
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  wandugu bado naona tuko ktk nadharia zaidi!!

  Kuna gap kubwa kati ya nadharia na hali halisi!

  hakuna watu waliowahi kundelea kwa kubembelezana!
   
 19. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hakuna kubembelezana tunakubali. Sasa hiyo njia ya kutokubembela ni ipi na itawasaidiaje wafugaji kuboresha maisha yao?
   
 20. F

  Felister JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hawahitaji kubembelezwa ni haki yao na wakuwapatia maisha mbadala ni wewe walikouwezesha kusoma kwa kodi yao. Sasa usiwalaumu wao jilaumu wewe ambaye walikuamini wao wakaona unawazidi upeo wakachagua kuendelea kulima kwa mkono ili wewe kwakuwa ulionyesha upeo wa juu wakupe kodi zao walizo pata kwa ku toil ili utakapomaliza uwaelekeze jinsi ya ku transform so kubali hiyo responsibility nao watakuitikia na wakisha transform watakupa kodi kubwa zaidi ili uishi kama uko peponi zaidi ya hapo ulipo sasa. Ukikataa wataendelea kuwa mzigo kwako na kamwe hutafurahia hayo maisha maana kwa bahati mbaya wanajina linalofanana na lakwako 'watanzania' popote watakapo onekana majuha jua na wewe included labda ujilipue lakini na huko watakuambia tu African from where? Je unakata haki yako ya kuzaliwa?

  truth is like a bitter pil many like but few taste it
   
Loading...