Tufanye hivi watanzania kuwasaidia vijana wetu.....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanye hivi watanzania kuwasaidia vijana wetu.....!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, Oct 27, 2011.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wanajamii niko Pretoria, South Africa kikazi katika moja ya mambo yaliyonivutia hapa ni habari za kuwepo kwa chama cha wanafunzi wa elimu ya juu kilichotimiza umri wa miaka 20 jana october 26. Hiki si chama cha kisiasa ni chama kilichoanzishwa ili kutetea masilahi ya wanafunzi wote wanaosoma katika vyuo vya elimuya juu bila kujali ni vya umma au binafsi. lengo la kuazishwa kwake ni kutokana na matukio ya muda mrefu ambapo serikali kupitia taasisis iliyoazisha kusimamia utoaji wa ada kwa wanafunzi wa elimu ya juu kuwa ya kibabaishaji. Chama hiki kinafanya mawasiliano ya moja kwa moja na serikali kuhusu mikopo na maslahi mengine wanayostahili upata wanafunzi wa elimu ya juu.

  Ninachojua huko kwetu limekuwa ni donda sugu kwa bodi yetu ya mikopo ya elimu ya juu kutotimiza kile ambacho wanafunzi walitarajia kama kutotoa mikopo kwa wakati, viwango vya mikopo kutokidhi nk....Na kiukweli kabisa hiki chama cha wanafunzi hapa kina nguvu ya ajabu maana kama leo asubuhi walifanya mkutano Johannesburg baadae maandamano makubwa kabisa na wanapanga kukutana na serikali ili kuzungumzia kuongeza kiwango cha mikopo kwa wanafunzi kwani idadi ya wanafunzi wanaoingia vyuo vya elimu ya juu inaongezeka kila siku...
   
Loading...