Tufanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufanyaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rabin, Jun 25, 2010.

 1. Rabin

  Rabin Senior Member

  #1
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa nikifuatilia siku zote mambo mbalimbali yanayohusu nchi yetu hii kwa namna au njia mbalimbali iwe kwa kupitia vyomba vya habari au kwa kushuhudia mwenyewe, tuko wengi na mambo ni mengi, mengi ya mambo hayo ni yale yanayomhusu mtanzania wa hali ya chini kabisa awe ana elimu nzuri au hana.Tangu kuzaliwa kwangu miaka ya sabini nimeshuhudia mambo mengi na mpaka leo mengi ya mambo hayo bado nayashuhudia. inaumiza na inasikitisha sana kuona watanzania tumekuwa kama watazamaji tu wa kila kinachofanyika ndani ya nchi yetu, tumejiweka katika hali ya unyonge na tumekubali kuwa ni wa watu wa kuambiwa tu na si kutenda, inauma kuona maisha yetu bado ya kubahatisha kwa kila kitu na kila siku wengi wetu tumejihakikikshia maisha hayo (ya kubahatisha) baada ya kuona hata tufanyaje baada ya miaka yoyote ijayo hatutegemei mabadiliko bali tutashuhudia mabadiliko ya watu wachache, ndiyo jamii kubwa ya watanzania ilivyo.

  Inauma sana katika nchi yenye umri wa miaka zaidi ya arobaini na mitano bado hatuko imara kiuchumi, kisiasa, na katika nyanja zote muhimu ambazo kutokuwa kwake imara kunapelekea kukuosekana kwa huduma muhimu kwa mtanzania huyu wa chini kabisa, mahali ambapo huduma hizo zinapatikana basi ni kwa kiasi fulani lakini bado hazitimizi mahitaji ya mahali hapo husika.Ukifuatilia kwa makini utakuta siasa ndio chanzo kikubwa cha kuharibu mipango yote ya serikali kwani hata watendaji wa serikali wako kisiasa zaidi na hasa kaitka mambo yanayohitaji maamuzi yasiyo ya kisiasa, inauma sana na si kwamba watanzania hawajui, wanajua ila kwa sababu tumekuwa watazamaji tu, tutafanya nini.

  Swali langu: Watanzania tufanye nini ili tuweze kuondokana na kuwa watazamaji tu na kulalalmika na mambo yanavyokwenda katika nchi yetu? ni nani wa kufanya vitendo?
   
Loading...